Shirika la ndege lipi lina nauli nafuu zaidi kutoka Dar Es Salaam kwenda New York,Boston au Washington DC

Sijui umemaanisha nini uliposema ''moja kwa moja'' lakini nakukumbusha kuwa hakuna ndege inayoondoka Dar To USA moja kwa moja. Pili unaposema ni shirika lipi lenye bei nafuu sidhani kama kuna jubu la moja kwa moja. Mimi nitakuambia inategemea. Leo unaweza kukuta tiketi ya wiki ijayo ya KLM iko cheap zaidi ya Emirates na keshokutwa ukakuta vise versa. Mimi ni msafiri mkongwe wa ndege na kitu nachoweza kukuambia ni kuwa ukishaamua safari yako ni siku fulani basi ingia kwenye kila website ya shirika husika uangalia bei. Huachajiwi chochote kwa ku-kusearch nauli. Kingine jaribu kutumia ''search engine'' ya kusafiri kwa ndege. Hii hukuletea nauli ya kila shirika na wewe unaamua utanunua tiketi gani. Ziko search engine nyingi kama Momondo nk. Kwa mfano jaribu kuingia hapa https://www.momondo.fi/ u-search utaona ninachomaanisha. Jambo jingine la kuzingatia ni kuwa usiangalia tu urahisi wa bei bila kuzingatia conditions za tiketi. Kuna tiketi nyingine ukiugua siku ya safari na ukashindwa kusafiri basi imekula kwako. Nyingine unakuta wanakuruhusu kubadisha tarehe ya safari. Na nyingine unakuta gharama ya kubadilisha ni kama kununua tiketi mpya. Haya yote ni ya kuzingatia.
Asante mkuu barikiwa sana,hope na wengine watanufaika na haya maelezo
 
Back
Top Bottom