Shirika la ndege lakatazwa kutowabadilishia viti wanawake Israel

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,521
2,000
Shirika la ndege la Israel EI AI limepigwa marufuku kutowaomba wanawake kubadilisha viti iwapo mwanamume wa kiyahudi atakataa kukaa karibu nao ,mahakama imeamuru.

Abiria Renee Rabinowitz ambaye ana umri wa miaka 80 aliwasilisha kesi dhidi ya shirika hilo la ndege baada ya kutakiwa kuondoka katika kiti ambacho angekaa na mwanamume wa kiyahudi.

Jaji wa Jerusalem alisema kuwa maombi kama hayo ni ya kibaguzi.
Hatahivyo shirika hilo la ndege linasema kuwa haliwalazimishi abiria kubadilishana viti.

Bi Rabinowitz ambaye ni manusura wa Holocaust alikuwa akisafiri kutoka Newark nchini Marekani kuelekea Tel Aviv 2015 wakati alipoombwa na mfanyikazi mmoja wa ndege kubadilisha kiti.

Alisema alihisi kuaibishwa.
Wanaume walio na msimamo mkali kuhusu dini na utamaduni nchini humo hujaribi kujizuia kuwagusa wanawake isipokuwa wake zao pekee ili kutovutiwa na uhusiano wa ziada.

Makundi ya kupigania haki za kibinaadamu nchini Israel ambayo yalikuwa yakimwakilisha bi Rabinowitz katika kesi hiyo walisema kuwa ushindi huo ulikuwa mkubwa katika vita virefu dhidi ya ubaguzi wa kijinsia.

bbc swahili
===========

Nilikuwa sijui kama hawa binadamu wenzangu ugomvi wao umefikia mpaka hatua ya kutokaa kiti kimoja kwenye vyombo vya usafiri.

Ngachoka kabisaa
 

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
17,417
2,000
Wanawake wa Mashariki ya kati wana kazi kubwa sana. Huko Saudi Arabia walikatazwa hata kuendesha Magari.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,861
2,000
Duh! Kumbe Uyahudi ni Uislamu zaidi kuliko Ukristo. Ndio nimejua leo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom