Shirika la ndege la Uganda kuanza kupata faida 2029

nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,430
5,769
Haaa uuwiii eti shirika la ndege litaanza kupata faida baada ya miaka 10,hii ni baada ya kufufuliwa,mbona sisi ATCL imepiga faida ya 29 billions ndani ya mwaka mmoja tena hayo maneno yamesemwa na Rais wetu kipenzi ambaye ni msemakweli mpenzi wa Mungu.Mje TZ mjifunze jinsi faida zinavyopigwa,serikali kwani inapataga hasara?
Capture.PNG
 
FB_IMG_1558610052612.jpg

Imeelezwa kwamba Shirika lilofufuliwa la ndege la Uganda linatarajiwa kuanza kutengeneza faida mwa 2029.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Cornwell Muleya, shirika hilo litahitaji kujenga imani ya wateja wake ili waweze kuliamini.

Pamoja na kufufuliwa, kupata ndege mpya na kupewa ruzuku na serikali ya Rais Yoweri Museveni, bado litahitaji kipindi cha miaka kumi ili kuweza kujiendesha lenyewe. #BigData
 
ATCL imekufa ikiwa imeacha madeni, imefufuliwa kwa kununuliwa ndege mpya kadhaa. Ripoti ilotolewa inaonesha ATCL imepunguza deni. Maanake ATCL ina operate kwa faida, mana kama ingekuwa inapata hasara, deni lingeongezeka.
 
Umewahi pewa mchanganuo wa operational cost ukajua na faida yao?

Ukiweza kulipa madeni yako na biashara yako isiathirike basi maana yake unapata faida. Vyenginevyo deni lingeongezeka. Wewe wamekupa mchanganuo wa operational cost unipe niuone?
 
Na ATCL ikifa kabla ya ilo la Uganda uje hapa chaaap uanzishe uzi kama huu, kukurupuka na hizi njaa kubaya sana..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom