Shirika la ndege la South Africa (SAA) liko hoi lakaribia kuwa mufilisi - Tanzania tuna jambo la kujifunza?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,137
18,746
Shirika la ndege la ndege la South Africa, lenye jumla ya ndege karibu 50 kubwa, za kati na ndogo, liko katika hali mbaya kiuchumi kiasi linakaribia kuwa mufilisi.

Shirika hili kwa miaka mingi limekuwa likijiendesha kwa kutegemea ruzuku za serikali bila kuwa na uwezo wa kusimama kwa miguu yake. Kwa miaka saba iliyopita limeripoti hasara ya mabilioni ya shilingi.

(SAA) wana network ya karibu safari 40 kwenda nchi 26 duniani, wakitumia ndege za Airbus pekee kubeba abiria, kutia ndani Airbus 340-600 ambazo ziko tisa, wakiwa na mpango wa kukodisha ndege mpya nne za Airbus 350-900 kuanzia mwezi huu December. Katika ndege 50 walizonazo, 2 ni Boeing 737-300 ambazo ni cargo planes.

Jambo ambalo Watanzania tunapaswa kukazia ni uendeshaji wa shirika hili katika karibu miaka 20 iliyopita. Kwa kiasi kikubwa, shirika limeendeshwa kisiasa na kiupendeleo, hasa katika uteuzi wa wakurugenzi wake.

Kulikuwa na kasi ya kutaka kubadilisha wazungu ili nafasi zao zichukuliwe na watu weusi, hata pale ambapo watu weusi walikuwa hawana sifa zinazostahili, katika kile kilichaitwa Black Economic Empowerment (BEE) na Affirmative Action employment.

Inasemekana mwaka 2007 na 2008 (SAA) walipopata hasara, uongozi wa kizungu ulirudishwa, ambao uliiwezesha (SAA) kurudi kupata faida mwaka 2009 hadi 2011.

Baada ya faida ya miaka mitatu mfulilizo, uongozi wa kizungu uliondolewa tena na kuwekwa wazalendo weusi, na shirika likarudi kwenye hasara tena kuanzia 2012 hadi leo 2019!

Mara nyingi wakurugenzi wazalendo weusi walipoteuliwa walifanya ufujaji wa kutisha wa fedha, kutia ndani ticket za bure kwa ndugu, jamaaa na marafiki na matumizi ya starehe ya fedha za shirika.

Kwa mfano, kuna mkurugenzi mmoja alikuwa akienda kazini na kurudi nyumbani kwa helikopta ya kukodi akidai kukwepa msongamano wa magari asubuhi na jioni, na kumpa mke wake tenda ya huduma ya chakula cha kwenye ndege. Aliachishwa kazi kwa haya makosa.

Na pia uteuzi wa viongozi wa juu wa (SAA) mara nyingi umegubikwa na vivuli vya uteuzi wa kisiasa na upendeleo bila kuangalia uwezo.

Wakati fulani kulikuwa na tuhuma kwamba Mwenyekiti wa SAA aliyekuwa mwanamke aliteuliwa kwa kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na raisi wa nchi hiyo.

Je, Tanzania tuna jambo la kujifunza kutokana na yale ambayo SAA inakabili? Je wazungu wanatuzidi katika mambo ya ku-manage mashirika? Tulete wazungu kutuendeshea ATCL kwa faida?

Reference: Desperation time for SAA
 
Unataka tujifunze kwa waliofeli? Kwanini usiseme tujifunze kwa Ethiopian Airlines?
Mkuu, tunaweza kujifunza kwa mashirika yenye mafanikio, lakini mara nyingine mtu unajifunza kutokana na kufeli kwa wengine ili usipitie hatua walizopitia.

Ndege za leo ni salama sana kusafiri nazo kwa kuwa mainjinia wamejifunza kutoakana na zile zilizoanguka na kuua watu, sio zile ambazo hazijawahi kuanguka.
 
Tanzania hatuna la kujifunza sababu kila kitu ni siri
Sawa kabisa. Hata ukaguzi wa mahesabu ya hili shirika hautafanywa. Kwa hiyo ATCL ikiamuriwa iahirishe safari ya Mumbay ili ipeleke mashabiki wa Chama fulani Mwanza, mtu asiulize ikiwa kulikuwa na malipo kwa ukodishaji huo!
 
ATCL apewe Bongozozo
Mie naona tuwape wazungu watuendeshee shirika. Angalau wana kiburi cha kumtolea nje waziri akiomba ndege icheleweshwe kwa kuwa bado anafungua kinywa kachelewa kuamka!

Kwa hawa viongozi wazalendo, unakuta waziri aliyependekeza jina lake awe mgurugenzi ndio huyo anamwambia hebu icheleweshe ndege kidogo kwa sababu za "kiufundi" maana bado sijapata breakfast, nitakuja airport nikimaliza.
 
Mkuu, tunaweza kujifunza kwa mashirika yenye mafanikio, lakini mara nyingine mtu unajifunza kutokana na kufeli kwa wengine ili usipitie hatua walizopitia.

Ndege za leo ni salama sana kusafiri nazo kwa kuwa mainjinia wamejifunza kutoakana na zile zilizoanguka na kuua watu, sio zile ambazo hazijawahi kuanguka.
Tunajifunza mafanikio ya wenye mafanikio, na pia tunajifunza mafanikio ya waliofeli.
 
Nilichogundua ngozi nyeusi ndio tatizo katika kuendeleza biashara
 
Shirika la ndege la nchi fulani ya Afrika mashariki likikaribia kuwa mufilisi data zitafichwa!
 
Tunaliteka soko la SADC sasa hv...
ila tusiwe wavivu kwenye management tuweke watu wanaojua figisu figisu za flights.....
sio lazima awe mbongo.....
 
Back
Top Bottom