Shirika la ndege Fastjet lanunua ndege za "mapangaboi" (AT72) ili kuongeza ushindani wa usafiri wa anga Tanzania

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.png


Shirika la ndege la fastjet linatarajia kupokea ndege yake aina ya ATR72-600 hivi karibuni. ATCL wakae chonjo

Kwa mujibu wa mtandao wa Skyliner Aviation, ndege hiyo inaonekana ikiwa tayari imeshapakwa rangi za fastjet, na taarifa zinasema inatarajiwa kusajiliwa Tanzania na kuanza kazi katika mwezi wa Januari 2018.

Fastjet wanasema ATR itawawezesha kutua katika maeneo ambayo ndege aina ya jet haziwezi kutua.

Kwa maana hiyo sasa fastjet wataweza kutua katika viwanja kama vile Mtwara, Kigoma, Tabora, Arusha na kwingine kule ambapo ATR72 inaweza kutua kwa usalama.Maeneo haya kwa sasa inatua "bombandia" ya ATCL tu na ATR za Precision.

Ndege za ATR si ngeni hapa nchini kwani shirika la ndege la Precision Air linamiliki kiasi kikubwa cha ndege hizo, takribani ndege 9 zikiwa ni ATR72 na ATR42, na ni miongoni mwa mashirika yanayo ongoza barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya ATR, na pia ina karakana yake ya ufundi ambayo imebobea katika ufundi na matengenezo ya ndege hizi za ATR.

ATR72 ina uwezo wa kubeba abiri kati ya 72 hadi 78.

Tutarajie kuona ushindani zaidi katika soko la usafiri wa anga jambo ambalo linaweza leta unafuu kwa watumiaji wa usafiri huo na pia kuwa ni chachu ya kuongeza ajira na maslahi kwa wafanya kazi ktk sekta hii.

Picha kwa hisani ya mtandao wa Skyliner.
 
Mimi kama Cyrus sina imani na FASTJET tena, wamekuwa wakituweka uwanjani kwa mda mrefu mara ndege haipo mara ihairishwe.

Story hiuzi za ndege mpya zilikuwepo tangu awali, mara kunda ndege mbilki mpya uwanja wa ndege Dar zikiwa zinasubiri kusajiliwa na vibali.

Sitamani tena FASTJET.... nilichelewa mkutano wangu wa ARUSHA ikiwa ndege ya kuondoka DAR kuelekea Kilimanjaro kuhairishwa toka asubuhi mpaka saa kumi jioni?

They are not serious. kuamini kwangu mpaka nione mwenyewe
 
Mkuu Barafu,

Heri ya Noel na mwaka mpya.


Asante kwa huu uzi. Sijui in Mimi tuu au hata wenzangu wanaliona. I have never trusted government as a trusted partner in busness. Kiukweli ingawa natamani ATCL ifike mbali Kama credible competitor kwenye usafiri WA anga ndani na nje ya Tz, lakini nina wasiwasi watashindwa. Naona JPM katumia nguvu nyingi lakini sidhani Kama alifanya utafiti ni nini kiliua ATC ya awali. Na shirika lina mikakati gani kutorudia makosa.

Kama Fastjet wakianza kuruka viwanja korofi siioni ATCL ikipambana kutoa huduma bora. Hata website yao bado ni mbovu. I wish huyu CEO WA ATCL abadirike......lakini naona lack of oversight na accountability ikiwa kikwazo. It is unfortunate hela za serikali wengi tunaamini hazina mwenye. Sad!
 
Yaani fastjet anataka aanze tua dodoma, musoma, mtwara.....
Kale kashirika ketu vipi?
Afu fastjet mwaka huu wameleta Embraer na mwakani atr
 
Pangaboi za Magu zinawakimbiza sana kwenye mwendokasi. Mara kadhaa nimeshuhudia pangaboi likitangulia kutua kabla ya fast jet na precision japo lilikuwa la mwisho kuruka.
Una hitilafu kubwa kwenye sehemu fulani ya ubongo
 
Fastjet must change kama wanataka kuongeza mtandao wa huduma zao na kujenga imani ya wateja wao. Siku za karibuni wamekuwa hawaaminiki ktk ratiba yao ya kila siku na sbb zao nying si za msingi.
 
Pangaboi za Magu zinawakimbiza sana kwenye mwendokasi. Mara kadhaa nimeshuhudia pangaboi likitangulia kutua kabla ya fast jet na precision japo lilikuwa la mwisho kuruka.
Wewe unawakilisha sifa za watanzania walio wengi. Unahitaji tuzo
 
Mimi kama Cyrus sina imani na FASTJET tena, wamekuwa wakituweka uwanjani kwa mda mrefu mara ndege haipo mara ihairishwe.

Story hiuzi za ndege mpya zilikuwepo tangu awali, mara kunda ndege mbilki mpya uwanja wa ndege Dar zikiwa zinasubiri kusajiliwa na vibali.

Sitamani tena FASTJET.... nilichelewa mkutano wangu wa ARUSHA ikiwa ndege ya kuondoka DAR kuelekea Kilimanjaro kuhairishwa toka asubuhi mpaka saa kumi jioni?

They are not serious. kuamini kwangu mpaka nione mwenyewe
Wasamehe bure mkuu wanajipanga. Hata mi walinicheleweshaga kwenye mkutano muhimu sana, lakini nilivogundua wana ndege moja tu, tena ya kukodi, nikawasemehe bure. Kwa ndege moja wanajitahidi kwa kweli.

Wakija kupata angalau ndege 2 au 3 watakuwa reliable sana. Na hapa ndo watarudisha imani yangu kwao.

Lakini kwa sasa nimehamia bombadia, and so far hawajaniangusha kusema kweli, though nauli zao ni kubwa relatively.
 
Nategemea kusikia watu wakiponda pangaboi tena....biashara zina mbinu zake ATCL waliona hilo sasa FJ nao wamefuata.
Watu walikuwa wanaponda sana pangaboi za Magu, kumbe ndo zinafaa kwa soko letu. Na zinawakimbiza sana kina Fastjet na Precision hawapumui. Ni very reliable, mpya na zinamvuto
 
Back
Top Bottom