SHIRIKA la kutetea haki za Wasichana na Wanawake KIVULINI mkoani Mwanza, limeendelea kupambana na maambukizi ya virusi vya corona

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Watumia mwanya wa COVID 19 kufanya vitendo vya ukatili

SHIRIKA la kutetea haki za Wasichana na Wanawake KIVULINI mkoani Mwanza, limeendelea kuunga jitihada za serikali za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona (Covid 19).

Shirika hilo, jana limekabidhi vifaa vya kupimia wingi wa joto mwilini pamoja na dawa za kutakasa mikono ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona vinavyoitesa dunia kwa sasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Yassin Ally amekabidhi vifaa hivyo kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella kwa ajili ya kuvigawa katika taasisi mbalimbali hususani zinazohudumia idadi kubwa ya wanawake ikiwemo dawati la jinsia la polisi.

Yassin amesema Shirika hilo limetoa vitakasa mikono pamoja na mashine za kupima wingi wa Joto mwilini vipatavyo 18 vyenye thamani shilingi milioni 6.3 ambavyo vitakapelekwa maeneo hayo ili kutoa huduma kwa wananchi hususani wanawake.

Amesema kutokana na janga hili la Corona, Kivulini imeamua kuanzisha kampeni ya kuelimisha wananchi namna ya kujikinga na Corona, itakayofahamika kama "CORONA IKO MLANGONI MWAKO" ambapo kampeni hiyo itafanyika katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Mara na Mwanza.

Amesema wanafanya hivyo, kutokana na kipindi hichi cha Corona kuibuka ukatili mkubwa ikiwemo ukatili wa watoto kulawitiwa pamoja na mwanamke mmoja aliyefungiwa ndani kwa madai mwanamke huyo ataleta corona nyumbani kwao.

"Katika kipindi hiki cha COVID 19 tumeshuhudia wimbi la ukatili, mfano hivi karibuni kuna mtoto wa miaka tisa alilawitiwa na mzee wa miaka 97 akiwa ameenda kuchezea maeneo ya mabatini, sasa hii ni hatari kubwa sana lazima tuchukue hatua.

"kuna mwanamke mmoja alifungiwa ndani siku mbili na mme wake ambaye ni Dereva bodaboda kwa madai ya kwamba mke wake huyo ataleta nyumbani corona wakati yeye ndiye anaefanya kazi itakayosababisha Corona, mwanamke huyo aliposikia njaa akaomba kufunguliwa mwanaume huyo alipasua chupa na kumnyoa kichwani kwake," amesema Yassin.

Yassin pia ameiomba Wizara ya elimu kuja na mbinu za namna ya kuwasaidia watoto (Wanafunzi) ambao kwa sasa wapo nyumbani, ya namna kupata mazoezi ya masomo yao, katika kipindi hiki cha Corona hatua ambayo itasaidia kupambana na janga hili kwa kuwa kuna watoto wengi waliopo mtaani.

Akipokea vifaa hivyo, Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza, amelipongeza shirika hilo kwa kutoa msaada wa vifaa hivyo katika mkoa wake kwa kuwa bado kuna uhitaji mkubwa.

Mongella katika hatua nyingine, amewakumbusha wananchi kuendelea kumuomba mungu kwa kuwa yeye ndiye mwenye uwezo wa kuumaliza ugonjwa huo, pamoja na kuchukua hatua za kujikinga na maambukizi ya COVID 19.

IMG20200428154220.jpg
IMG20200428154220.jpg
IMG20200428154223.jpg

Mwisho
 
Wakati mwingine matangazo haya yanahitaji sympathy ya wasomaji ili waweze kutoa misaada kwa hizi NGO. Ila tatizo huzidisha chumvi katika maelezo yao. Hebu fikiria mzee wa miaka 97 akimlawiti mtoto wa miaka tisa! Imekaaje hiyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom