Shirika la chakula duniani, WFP limesitisha shughuli ya kugawanya chakula cha misaada kwa wakimbizi nchini

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Shirika la chakula duniani, WFP limesitisha shughuli ya kugawanya chakula cha misaada kwa wakimbizi nchini Uganda.

Hii ni baada ya madai kuibuka kuwa watu wawili wamefariki na wengine zaidi ya mia mbili kulazwa katika hospitali ya Karamoja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo baada ya kutumia unga wa uji unaodaiwa kuwa na sumu.


Vifo hivyo vilitokea baada ya watu hao kunywa uji wenye lishe maalum waliotayarisha kutokana na msaada wa unga uliotolewa na shirika la chakula duniani WFP.

Shirika la msalaba mwekundu limeripoti kuwa waathiriwa wanaonesha ishara za kuugua ugonjwa wa akili pia.

Tangu Ijiumaa iliyopita, watu kadhaa wamelazwa hospitali katika eneo la Karamoja wengi wao wakilalamikia kuumwa na tumbo.

Kwa mujibu washirika la WFP familia za waathiriwa zilipokea ungao huo wa msaada wiki iliyopita.


Lengo la msaada huo ni kuboresha lishe miongoni mwa akina mama waja wazito na wale wanaonyonyesha, watoto walio kati ya umri wa miezi sita hadi miaka mitano ili kuepusha hali ya wao kutostawi kimwili.

''Walikua hawafahamu kitu wanachofanya, walikuwa na dalili za punguwani, wanataka kukimbi wanakamatwa na watu wao, baadaye wakapelekwa kituo cha afya daraja la pili na huko wakaambiwa wanazidi uwezo wao ndipo wakapelekwa hospitali ya wilaya ya Amudat kaskazini mashariki mwa Uganda'' alisema mwandishi wa habari wa kujitegemea katika mkoa wa Karamoja, Edwar Emino.

Msemaji wa wa wizara ya afya nchini Uganda Emanuel Aine Byoona amesema wizara hiyo imechukua sampuli ya watu walio kula chakula hicho kwa uchunguzi zaidi:

''Kwa sasa tunasubiri uchunguzi wa maabara ya samuli zilivyochukuliwa kutoka kwenye chakula kupelekwa mahabara ya taifa ya uchunguzi Wandegeya.''

Bwana Byoona pia amesema vipimo vya damu ya wagonjwa waliolazwa vimepelekwa katika mahabara kuu ili kubaini ikiwa wameathiriwa na chakula kilichotolewa na Shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

''Mpaka sasa tunafahamu mtu mmoja ndiye amefariki kutokana na tuhumu hizo za chakula, yote itajulikana baada ya ripoti ya uchunguzi kutolewa ya sumu ya chakula.''


Hatua nyingine ambayo WFP imechukua ni kwenda kwenye makazi ya waliopewa unga huo warudishe ule waliobakisha huku wakiwahimiza watu kupitia kwa viongozi mashinani wasiendelee kuutumia.

Akina mama wanaonyonyesha wameshuriwa wasiendelee kuwanyonyesha watoto wao.

Uganda inawahifadhi zaidi ya wakimbizi milioni moja wengi wao wanawake na watoto kutoka nchini Sudan kusini.

Visa vyote vimeripotiwa katika eneo la Karamoja ambalo siku za nyuma limekuwa likiadhiriwa na ghasia, ukame na umasikini ambao umeziacha jamii katika eneo hilo kutegemea chakula cha misaada.

BBC
 
Mavyakula yao hawayachunguzi wanayaleta makusudi alafu saivi wanajitia kukataza watu wasendelee kutumia wakati wanaleta walitaka nini kama sio kutufyekelea mbali wote
 
shirika la chakula WFP isisitishe kutowa cha msaada wa chakula
IMG_20190204_123745.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom