Shirika la Afya Duniani (WHO) lapendekeza kutumia chumvi gram 5 kwa siku

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema matumizi makubwa ya Chumvi husababisha Kiharusi na magonjwa mengine.

Wamesema vifo milioni 2.5 vingeweza kuzuilika ikiwa watu wanatumia gram 5 za chumvi kwa siku ambayo ni sawa na kijiko kimoja cha chai.

Watu wengi duniani hutumia gram 9 hadi 12 za chumvu kwa siku ambayo ni mara mbili ya kiwango kinachopendekezwa na WHO.

Katika wiki hii ya kukuza uelewa wa chumvi, WHO imesema Nchi Wanachama wamekubaliana na kiwango cha gramu 5 kutumika na mtu mzima huku watoto wakitakiwa kutumia chini ya hapo.

=====

High sodium consumption (>2 grams/day, equivalent to 5 g salt/day) and insufficient potassium intake (less than 3.5 grams/day) contribute to high blood pressure and increase the risk of heart disease and stroke.

The main source of sodium in our diet is salt, although it can come from sodium glutamate, used as a condiment in many parts of the world.

Most people consume too much salt—on average 9–12 grams per day, or around twice the recommended maximum level of intake.

Salt intake of less than 5 grams per day for adults helps to reduce blood pressure and risk of cardiovascular disease, stroke and coronary heart attack. The principal benefit of lowering salt intake is a corresponding reduction in high blood pressure.

WHO Member States have agreed to reduce the global population’s intake of salt by a relative 30% by 2025.

Reducing salt intake has been identified as one of the most cost-effective measures countries can take to improve population health outcomes. Key salt reduction measures will generate an extra year of healthy life for a cost that falls below the average annual income or gross domestic product per person.

An estimated 2.5 million deaths could be prevented each year if global salt consumption were reduced to the recommended level.

1615536254588.png
 
Mimi niko bize kujikinga na corona.

Kwanza shuleni tulifundishwa kula chumvi nyingi ni kuishi miaka mingi hawa mabeberu wanataka nile gram tano tu kwa siku nyambafu mimi sio fala.
 
achana na mabeberu hao, chumvi nyingi unapata safura

btw, niko bize najifukiza
 
Tuache utani jamani,chumvi nyingi ni hatari sana mwilini hasa kama mtu anamatatizo mengine km ya kisukari na figo.Siku mtu anaebeza akipata haya magonjwa ndo ataelewa.
 
Nita neutralise kwa Maji mengiii, tusipangiane cha kula.
 
Huku kwenye uchumi wa kati hali ni ngumu, kuna wakati tunashindwa kumudu bei ya chumvi tunakula chakula hivyo hivyo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom