Shipping from usa to Tanzania, Ipi ni njia rahisi ama best shipping company?

Micky55

Member
Sep 2, 2016
69
50
Nahitaji kufanya shipping ya Parcel(spare parts ya simu. screen display+ battery) kutoka texas usa kuja bongo kwa mwenye uzoefu. Ipi ni njia rahisi ama best shipping company ambayo naweza kutumia ili mzigo wangu ufike salama na kwa mda mfupi??
Gharama zake zikoje?
 
salama na muda mfupi ni dhl, gharama sina uhakika kuja ila kutoka ni 85,000 flat rate.
 
Inategemea na uzito, USPS ndo cheapest nadhani hii ndo POSTA ya marekani, mzigo utafikia kwenye PO Box yako. DHL ni gharama zaidi na kuna uwezekano mkubwa zaidi wa extra fees/taxes pia PO box hauwezi kutumia last time I checked ni physical address tu.
 
Ukitaka fasta lazima ukutane na Magufuli mzee wa hapa kazi tu na maana lazima ulipe kodi uwe na tin namba ila ni bora zaidi maana ni fasta kama upo Dar ni siku tano hadi nne tumia Aramex au DHL.Tofauti na hapo hiyo item ikiwa ni free shipping basi ni siku 21 hadi mwezi.
 
Duh Aramex wajinga sn utakumbana na kodi hutokaa usahau wana vighalama vya ajabu ajabu mara clearing agent fee mara swissport fee tra assessment utakuta charges zinazidi bei ya mzigo
 
Ipi ni njia rahisi ama best shipping company ambayo naweza kutumia ili mzigo wangu ufike salama na kwa mda mfupi??
Kwa kuwa umeweka vigezo nitakujibu kama ifuatavyo.

- Njia rahisi -
Kwa muktadha wa ghalama ndogo, tumia USPS , Mzigo utaupokelea posta, Itachukua siku kati ya 14 - 35 mzigo kufika.

- Mzigo ufike Salama -
Njia yeyote utakayo chagua mzigo wako utafika salama

- Muda mfupi-
Hapa kampuni kama DHL, ARAMEX, UPS, FEDEX etl zinahusika.
Mzigo utafika kati ya siku 5 - 14 labda swali la msingi ni hili.

Je ipi kampuni sahihi ya kuchagua kati yahizo tajwa.
- Ni vigumu kuchagua kampuni sahihi bila kuwa na kigezo, maana zote zinasafirisha nakufikisha mizigo kwa wakati, na zote ghalama zinalingana na kutofautiana kidogo.
- Kati ya hizo zote chagua DHL sababu pekee ya kuifanya DHL iwe bora ni kuwa wao Hawana hizi charges hapa chini, Utapewa hesabu ya kodi unayotakiwa kulipa tu.

Charges utakazo kutana nazo kwenye kampuni zingine ni hizi, hususani kwa mzigo unaotakiwa kulipiwa KODI
1. Swissport Charges TSH 27,000
2. Assesment fees TSH 60,000
upload_2017-1-24_18-53-50.png

Na kwa kampuni zingine wana hadi
3. Agent fees TSH 155,000

Iwapo mzigo wako una uzito mkubwa ni vyema ukawatumia ARAMEX, ili kupata nafuu ya ghalama ya usafirishaji, ila uwe tayari kulipia charges no.1 na no.2

KARIBU
 
View attachment 463443
Na kwa kampuni zingine wana hadi
3. Agent fees TSH 155,000

Iwapo mzigo wako una uzito mkubwa ni vyema ukawatumia ARAMEX, ili kupata nafuu ya ghalama ya usafirishaji, ila uwe tayari kulipia charges no.1 na no.2

KARIBU

Mzigo wangu umefika, sasa uko held customs ndo nakumbana na charges nyingi sana mkuu. Niliusafirisha by FedEx.

Una ufahamu wa clearing agent yeyote anayeweza kunitolea mzigo huo?
 
Kwa kuwa tayari mzigo umefikia hatua hiyo, Hakuna kinachoweza kufanyika zaidi ya kufanya malipo yanayotakiwa kufanyika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom