Ghiti Milimo
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 4,344
- 6,403
Wadau,leo nilikuwa nafuatilia Bunge kupitia TBC Tv,kwenye baa moja,maeneo ya Bus Stand Shinyanga mjini! Kutokana na maeneo mengi kutokuwa na umeme,basi hapo kulikuwa na watu wengi,kwa ajili ya kufuatilia Bunge hilo.
Katika hali ya kushangaza,sehemu kubwa ya umati niliokuwa naangalia nao,walilipuka kwa kelele ya furaha,mara tu Mheshimiwa Filikunjombe alipo taja jina la naibu waziri wa Nishati na Madini Bw Stivin Masele kuwa naye aachie ngazi,kutokana na kuguswa na suala la ESCROW!
Hata baada ya hapo,watu wengi niliokuwa nakutana nao,nao walikuwa wanadai wamefurahi,kwani nafasi aliyonayo ya Ubunge ilikuwa ni ya dhuruma!
Inaonyesha wengi wa wakazi wa Shinyanga,hawajasahau na kumsamehe,kutokana na yaliyotokea kwenye uchaguzi wa 2010.
Kwenye uchaguzi ule,bwana Masele alitangazwa amemshinda mgombea wa Chadema Bw Sherembi kwa kura 1,ambaye alipinga mahakamani,kwa madai kuwa yeye (mgombea wa Chadema) alimzidi Bw Masele kwa kura zaidi ya 200. Hata hivyo,kesi ikikaribia kwisha,na dalili zikionyesha Bw Masele kushindwa,Bw Sherembi akafariki ghafla! Na huo ukawa mwisho wa hiyo kesi!!