Shinyanga washangilia Masele kutakiwa kuwajibishwa!

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
3,004
2,000
Wadau,leo nilikuwa nafuatilia Bunge kupitia TBC Tv,kwenye baa moja,maeneo ya Bus Stand Shinyanga mjini! Kutokana na maeneo mengi kutokuwa na umeme,basi hapo kulikuwa na watu wengi,kwa ajili ya kufuatilia Bunge hilo.
Katika hali ya kushangaza,sehemu kubwa ya umati niliokuwa naangalia nao,walilipuka kwa kelele ya furaha,mara tu Mheshimiwa Filikunjombe alipo taja jina la naibu waziri wa Nishati na Madini Bw Stivin Masele kuwa naye aachie ngazi,kutokana na kuguswa na suala la ESCROW!
Hata baada ya hapo,watu wengi niliokuwa nakutana nao,nao walikuwa wanadai wamefurahi,kwani nafasi aliyonayo ya Ubunge ilikuwa ni ya dhuruma!
Inaonyesha wengi wa wakazi wa Shinyanga,hawajasahau na kumsamehe,kutokana na yaliyotokea kwenye uchaguzi wa 2010.
Kwenye uchaguzi ule,bwana Masele alitangazwa amemshinda mgombea wa Chadema Bw Sherembi kwa kura 1,ambaye alipinga mahakamani,kwa madai kuwa yeye (mgombea wa Chadema) alimzidi Bw Masele kwa kura zaidi ya 200. Hata hivyo,kesi ikikaribia kwisha,na dalili zikionyesha Bw Masele kushindwa,Bw Sherembi akafariki ghafla! Na huo ukawa mwisho wa hiyo kesi!!
 

RockSpider

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
6,863
1,500
R.I.P Kamanda Sherembi... anaeishi kwa upanga shurti afe kwa upanga! Masele dhambi zake zitamuandama hadi kaburini na Jehanam ya moto mkali ...
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,933
2,000
Alifariki ghafla? Isije ikawa ni sumu maana haya Maintarahamwe yanaweza kufanya lolote lile ikiwemo kuua ili kuendelea kung'ang'ania madarakani.
 

Chizi Fureshi

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,718
1,500
Mawili, la kwanza ni kura moja ya tofauti. La pili umri wa Masele hautakiwi kuwa na maswali pia mazonge pembeni yake. Mwenzao Zitto anachomoka asee
 
Last edited by a moderator:

Pukudu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
3,132
2,000
Pamoja na kujipendekeza kwa Stand Utd!! Hatumtaki hata wana CCM wenzake hawampendi!! Kama vile namuona Gaki na Mama Mshandete walivyofurahi.
Na yule mpuuzi mwingine wa Kishapu Nchambi anaacha kushabikia timu ya jimboni mwake Mwadui FC. Anajipendekeza Stand!! Mzunguko wa pili hatuwataki mshatuletea gundu la kutosha
 

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
35,710
2,000
Alimpiga ndumba Shelembi,anampiga ndumba Kamanda Rachael Mashishanga,sasa aipige ndumba kamati tuone
 

MTENGETI

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,420
2,000
Mkuu sio sumu hiyo ni hayati bin zuluz yaan kwa kiswahili sayansi ya gizani hiyo
Alifariki ghafla? Isije ikawa ni sumu maana haya Maintarahamwe yanaweza kufanya lolote lile ikiwemo kuua ili kuendelea kung'ang'ania madarakani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom