Shinyanga: Wakinababa wadaiwa kuwaozesha watoto wao wadogo kwa pombe

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,545
Jambo hili lilibainishwa jana katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto,yaliyofanyika katika kijiji cha Penzi kata ya Mondo kupitia Shirika lisilo la kiserikali la World Vision chini ya mradi wa Enrich.

IMG-20191208-WA0130.jpg

Taarifa inaeleza kuwa, wanawake wanawashutumu kinababa wa kijiji hicho kuwaozesha watoto wao wa kike bila kuwajulisha kwa kubadilishana na jagi moja ya pombe wawapo vilabuni au mifugo aina ya ng’ombe.

katika kufafanua zaidi suala hilo, Angelina Suleimani ambaye ni Mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa kulingana na mila na desturi za Kisukuma hawaruhusiwi kuhoji inabidi wakubali mwanawe aolewa japo anasoma na makubaliano yanakuwa yamefanyika kwenye vilabu wakati wanakunywa pombe na wanapokataa wanaambulia kipigo.

Kwa upande wake Maria Emmanuel alisema kuwa, wakati mwingine unakuta mtoto anafanya vizuri kwenye masomo yake lakini baba yake anamtaka kufanya vibaya kwenye mitihani yake kwa kisingizio hala fedha ya kumsomesha na unapofuatilia unakuta ameshakula mahali.

Aidha, Ofisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale alisema,ili kukomesha vitendo hivyo,wameanzisha utaribu wa mtoto wa kike anaefanya vizuri kwenye masomo, mzazi anatakiwa kufunga mkataba na mwalimu mkuu wa shule anayosomea na atakapofanya vibaya mzazi atawaajibika kisheria.

Pia Ngwale aliongeza, hakuna ndoa yoyote itakayofungwa kuanzia ngazi ya kijiji, kata hadi wilaya bila yakuwa na cheti cha kuzaliwa ambacho kitaonesha umri wa anakwenda kuolewa na akiwa chini ya miaka 18 wazazi wa pande mbili watashitakiwa.

“Kwasasa mmebuni mbinu mpya ya kuwaozesha watoto wenu, mnamuozesha binti mwenye umri wa kuolewa mchana na usiku ukifika mnampleka mtoto wenu kwa mlengwa,hii mbinu tunaifahamu na tunaifuatilia na lazima tuwabaini na kuwafungulia mashitaka"alisemaNgwale.

Naye Ofisa Jinsia na utetezi wa mradi wa Enrich kutoka shirika la World Vision Magreth Mambali alisema, wamekuwa wakitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili ikitokea ukatili watambue wapi wanatakiwa kwenda kupata msaada.

Hata hivyo alisema kuwa,waendesha baskeli na bodabonda wamekuwa chanzo kikubwa cha kusababisha mimba za utotoni kwa watoto wakike na kutoa wito kwa wadau na serikali kusogeza huduma za kishule hasa elimu ya sekondari karibu na makazi ya watu.

Chanzo: IPP Media
 
Wasukuma Ni watu wa ajabu kabisa, tatizo lao Ni kuabudu miungu mitatu, walwa, nyoo na nyama.
Yaani pombe, zinaa (uke) na nyama

 
 
Watani zangu wacheni tuwaite watu wa hovyo tu kwani saa nyingine munastahili.
 
Kwa upande wake Maria Emmanuel alisema kuwa, wakati mwingine unakuta mtoto anafanya vizuri kwenye masomo yake lakini baba yake anamtaka kufanya vibaya kwenye mitihani yake kwa kisingizio hala fedha ya kumsomesha na unapofuatilia unakuta ameshakula mahali.

Nilifundishwa kuwa ni mahari sijui mwalimu alikuwa mkweli au aliniingiza chaka!!
 
Back
Top Bottom