Shinyanga: Vurugu zazuka kwenye mkutano wa baraza la madiwani kati ya madiwani wa CCM na CHADEMA

LTN USU WA MADOSO

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
1,193
859
madiwani wa ccm na chadema wapigana ngumi manispaa ya shinyanga kwa kisa cha kugundulika madiwani wa ccm wanatumia pesa za miradi ovyo kwa manufaa yao ikiwa ni kununua pikipiki zao na kufanyia anasa zingine madiwani wa chadema walipowahoji ccm wakaja juu hivyo kuibua ngumi emmanuel ntobi diwani wa chadema ndoo alifichua maovu hayo.
12220ccb83579dbc4405a0847e91902d.jpg

Kumetokea vurugu za aina yake katika baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga baada ya madiwani hao kutoelewana na kutaka kuchapana makonde kavu kavu kwenye kikao chao cha baraza cha kawaida baada ya madiwani wa Chadema kuanzisha vurugu kwa madai ya kuonewa kwenye kikao hicho.

Vurugu hizo zimeibuka leo baada ya madiwani wa Chadema wakati wakiomba muongozo wa kanuni kwenye kikao hicho huku mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni naibu meya wa manispaa hiyo Agnes Machiya akidaiwa kuwapuuza na kuruhusu kikao kuendelea ndipo hali ya hewa ilipochafuka.

Wakati vurugu hizo zilizoenda sambamba na kupiga meza na kelele za hapa na pale zikiendelea, naibu Meya Agnes Machiya alimruhusu diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole (CCM) kuendelea kusoma taarifa yake ya kata.

Wakati Mwendapole akiendelea kusoma taarifa yake diwani wa Chadema kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi aliinuka huku akimtolea lugha chafu diwani huyo kisha kukata waya wa kipaza sauti alichokuwa anatumia Mwendapole.

Baada ya waya huo kukatwa huku meza zikiendelea kupigwa kwa fujo ndipo diwani Mwendapole alijawa na hasira na kutaka kumchapa vibao diwani wa Chadema Emmanuel Ntobi katika kikao hicho.

Kufuatia hali hiyo diwani wa viti maalumu Mariam Nyangaka (CCM) aliinuka na kumtuliza Mwendapole kisha kumtoa eneo la tukio.

"Haiwezekani ufanye fujo halafu ukate na waya wewe ni mtoto mdogo nitakulamba makofi, usalama mnafanya nini humu toeni nje hawa sisi tuendelee na kikao wameshazoea kususa hata Dar es salaam ilikuwa hivyo CCM tukachukua umeya," alisikika akiongea Mwendapole.

Vurugu hizo ziliendelea mpaka pale ofisa wa jeshi la polisi aliyekuwepo kwenye kikao hicho kuingilia kati na kutuliza ghasia hizo.

Madiwani wa Chadema mara kwa mara wamekuwa wakimtuhumu naibu meya Agnes Machiya kuendesha vikao kibabe kwa kutofuata miongozo na kanuni za vikao na kudaiwa kuwanyanyasa madiwani wa Chadema na kuwabeba madiwani wa CCM.

Baraza hilo la madiwani limejadili ajenda mbalimbali ambapo kitakaa ndani ya siku mbili kwa kusoma taarifa mbalimbali kwa mstakabali wa maendeleo ya wakazi wa mjini Shinyanga.

Chanzo:
Malunde blog
 
Mbona hizo "ngumi" sizioni. Kwenye picha madiwani wanaonekana wakibadilishana mawazo tu basi. Lete picha zinazoonyesha hayo masumbwi. Manaake upotoshaji sasa umeshamiri.
 
Emmanuel Ntobi njoo huku utupe habari imekaaje hii ya kuchapana makonde kwenye kikao? Hapo Mwendapole lazima atakuwa amepigana!
 
Ofisa wa Jeshi la Polisi akiendelea kutuliza jazba za madiwani wa Chadema

*****
Kumetokea vurugu za aina yake katika baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga baada ya madiwani hao kutoelewana na kutaka kuchapana makonde kavu kavu kwenye kikao chao cha baraza cha kawaida baada ya madiwani wa Chadema kuanzisha vurugu kwa madai ya kuonewa kwenye kikao hicho.

Vurugu hizo zimeibuka leo baada ya madiwani wa Chadema wakati wakiomba muongozo wa kanuni kwenye kikao hicho huku mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni naibu meya wa manispaa hiyo Agnes Machiya akidaiwa kuwapuuza na kuruhusu kikao kuendelea ndipo hali ya hewa ilipochafuka.

Wakati vurugu hizo zilizoenda sambamba na kupiga meza na kelele za hapa na pale zikiendelea, naibu Meya Agnes Machiya alimruhusu diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole (CCM) kuendelea kusoma taarifa yake ya kata.

Wakati Mwendapole akiendelea kusoma taarifa yake diwani wa Chadema kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi aliinuka huku akimtolea lugha chafu diwani huyo kisha kukata waya wa kipaza sauti alichokuwa anatumia Mwendapole.

Baada ya waya huo kukatwa huku meza zikiendelea kupigwa kwa fujo ndipo diwani Mwendapole alijawa na hasira na kutaka kumchapa vibao diwani wa Chadema Emmanuel Ntobi katika kikao hicho.

Kufuatia hali hiyo diwani wa viti maalumu Mariam Nyangaka (CCM) aliinuka na kumtuliza Mwendapole kisha kumtoa eneo la tukio.

"Haiwezekani ufanye fujo halafu ukate na waya wewe ni mtoto mdogo nitakulamba makofi, usalama mnafanya nini humu toeni nje hawa sisi tuendelee na kikao wameshazoea kususa hata Dar es salaam ilikuwa hivyo CCM tukachukua umeya," alisikika akiongea Mwendapole.

Vurugu hizo ziliendelea mpaka pale ofisa wa jeshi la polisi aliyekuwepo kwenye kikao hicho kuingilia kati na kutuliza ghasia hizo.

Madiwani wa Chadema mara kwa mara wamekuwa wakimtuhumu naibu meya Agnes Machiya kuendesha vikao kibabe kwa kutofuata miongozo na kanuni za vikao na kudaiwa kuwanyanyasa madiwani wa Chadema na kuwabeba madiwani wa CCM.

Baraza hilo la madiwani limejadili ajenda mbalimbali ambapo kitakaa ndani ya siku mbili kwa kusoma taarifa mbalimbali kwa mstakabali wa maendeleo ya wakazi wa mjini Shinyanga.

Chanzo:
Malunde blog
 
Siasa za namna hii ni hatari sana
Hili ni tatizo lililotengenezwa na viongozi wote wa vyama vya siasa walio tangulia baada ya kutengeneza image ya chuki na kudharaulina baina yao hivyo kuweka sura kuwa kila wanapo kutana chama tawala na vyama vya upinzani basi kuna uadui na kutunishiana misuli hali ambayo inadhuru hadi mambo yenye tija kwa taifa, na watu wa kuondoa dhana hii ni hao hao viongozi wakuu wa vyama hivyo vya siasa na si mtu mwingine
 
Zngechapwa hapo siku nyingine wangeheshimiana maana inaonekana ni kawaida yao kila kikao vulugu tu
 
Yani chadema mara nyingi wana act kama wana mama kila mara wanalia kuonewa...
 
Uwiano kati ya madiwani wa CCM na CDM upoje?

Wangewaacha waheshimiane,najua kidume na kibonde wakijulikana huu ujinga unaisha.
 
Back
Top Bottom