Shinyanga: Vijana 2 chini ya miaka 18 mbaroni kwa kumbaka mtoto wa miaka 6 kwa zamu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, linawashikilia vijana wawili, wakazi wa mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka sita kwa zamu.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Debora Magiligimba, akitoa taarifa hiyo jana kwa vyombo vya habari, alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 12, mwaka huu majira ya saa tatu kasorobo usiku.

Alisema watuhumiwa hao (majina yao yanahifadhiwa kutokana na kuwa na umri chini ya miaka 18), walimlaghai mtoto huyo kuwa watamnunulia pipi pamoja na kumpatia hela, na kisha kumpeleka vichakani nyuma ya nyumba yao na kuanza kumbaka kwa zamu.

"Tukio la kubakwa kwa mtoto huyu liligunduliwa na mama yake mzazi (jina limehifadhiwa), ambaye alikuwa akimtafuta mwanawe na kumuona akiwa ameumia sehemu za siri, ndipo akatoa taarifa polisi," alisema Magiligimba.

Alisema chanzo cha mtoto huyo kubakwa ni tamaa za kingono na kwamba upelelezi ukikamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani, ili kuchukuliwa hatua kali zaidi za kisheria.

Pia, kamanda alitoa wito kwa wazazi na walezi mkoani humo, kuendelea kutoa taarifa za ukatili, ili wahusika wachukuliwe hatua na kukomesha vitendo hivyo.
 
Chanzo cha mtoto kubakwa ni tamaa za ngono? Seriously?
Mtoto wa miaka sita anajua ngono?Anapata hisia?
Wamemuonea na kumdhalilisha kusema amebakwa kwa tamaa ya ngono it's not right and it's not fair.

A six year old is naive and innocent. Wakisema tamaa ya kupewa hela na kununuliwa vitu sawa lakini sio ya ngono.
 
Chanzo cha mtoto kubakwa ni tamaa za ngono???Seriously??
Mtoto wa miaka sita anajua ngono?Anapata hisia?
Wamemuonea na kumdhalilisha kusema amebakwa kwa tamaa ya ngono it's not right and it's not fair.
A six year old is naive and innocent. Wakisema tamaa ya kupewa hela na kununuliwa vitu sawa lakini sio ya ngono.
Tamaa za wabakaji sio huyo mtoto.
 
Elimu! Elimu! Elimu kwa watoto aisee.

Malezi pia muhimu wazazi tukumbuke hilo tutapoteza watoto.

Hawa watoto wanaweza kuwa walianza kuangalia picha ngono toka zamani.
 
Kwanini hawajataja umri wa hao vijana ambao technically ni watoto? Kwanini mtoto wa miaka sita aendelee kuwa nje mpaka mida ya saa tatu kasoro?

Hao wote ni watoto walikuwa wanapractice waliyowahi kuyaona.
 
watoto wa miaka 14 ndio wametumia mbele na nyuma ???

hapo ni ile michezo ya k'toto ambayo hata sisi tulishaicheza ila sio kweli kwamba mtoto wa miaka 14 ana uwezo wa kupiga mashine ile k'sawa sawa ndio maana mi naona ni kesi ya k'puuzi hii
 
Chanzo cha mtoto kubakwa ni tamaa za ngono? Seriously?
Mtoto wa miaka sita anajua ngono?Anapata hisia?
Wamemuonea na kumdhalilisha kusema amebakwa kwa tamaa ya ngono it's not right and it's not fair.

A six year old is naive and innocent. Wakisema tamaa ya kupewa hela na kununuliwa vitu sawa lakini sio ya ngono.
Kuna shida hapa.. How come motto wa miaka 6 akawa na tamaa za ngono...
 
Kuna shida hapa.. How come motto wa miaka 6 akawa na tamaa za ngono...
Acha miyeyusho.

Wabakaji ni under 18. Means wanaweza kua na miaka 17, 16, 15, 14, 13, 12 n.k.

Na walitumia ahadi ya pipi na hela kumlaghai.

Akili yako hapo inakwambia huyu mtoto wa miaka 6 alikua na tamaa za ngono ndiyo akataka pipi na hela? Mbona watu wengine mnaandika vitu hamfikirii?

Watendaji tukio wameweza kumuachia maumivu huyo mtoto means wamepevuka na wanajua nini wanachofanya so wao kua na libido ni given.

Watu wengine mnajaza ghasia
 
Chanzo cha mtoto kubakwa ni tamaa za ngono? Seriously?
Mtoto wa miaka sita anajua ngono?Anapata hisia?
Wamemuonea na kumdhalilisha kusema amebakwa kwa tamaa ya ngono it's not right and it's not fair.

A six year old is naive and innocent. Wakisema tamaa ya kupewa hela na kununuliwa vitu sawa lakini sio ya ngono.
Nadhani wabakaji ndo walikuwa na tamaa za ngono
 
Hao watoto waliobaka hawajitambui wala hawajielewi.
Shule ilibidi ifundishe jinsi ya kujitambua na kujielewa pia na sio kukariri notes pekee ili ufaulu mitihani.
 
Nadhani wabakaji ndo walikuwa na tamaa za ngono
Gotcha, japo style ya uandishi inapelekea kuonyesha mtoto ndo alikua na tamaa .
Wameandika chanzo cha "kubakwa" ni tamaa ya ngono
Wangeandika chanzo cha "kubaka" ni tamaa ya ngono
 
Chanzo cha mtoto kubakwa ni tamaa za ngono? Seriously?
Mtoto wa miaka sita anajua ngono?Anapata hisia?
Wamemuonea na kumdhalilisha kusema amebakwa kwa tamaa ya ngono it's not right and it's not fair.

A six year old is naive and innocent. Wakisema tamaa ya kupewa hela na kununuliwa vitu sawa lakini sio ya ngono.
Tamaa ya ngono ni wale wabakaji.
 
Back
Top Bottom