Shinyanga: Suma JKT waagizwa kuwachukulia hatua Walinzi wake waliompiga raia Hospitalini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Mkuu wa wilaya Shinyanga, Jasinta Mboneko, ameuagiza uongozi wa kampuni ya ulinzi ya Suma JKT, kuwachukulia hatua kali za nidhamu walinzi waliohusika kwenye tukio la kumpiga mwananchi Daudi Lefi, aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo kumuhudumia mgonjwa.

Agizo hilo amelitoa hii leo Januari 23, 2021, alipofika hospitalini hapo akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama na kufanya kikao cha ndani na uongozi wa hospitali hiyo na kueleza kuwa hospitali siyo sehemu ya kufanya fujo kwani Wananchi wanahitaji huduma.

Jana Januari 22, 2021, katika mitandao ya kijamii ilisambaa video ikionesha walinzi wakimshambulia, mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Daudi Lefi, aliyekuwa akitoka kwa ajili ya kutafuta dawa za mgonjwa ambaye ni mama yake, na ndipo walinzi hao walianza kumpiga kwa madai ya kwamba muda wa kuona wagonjwa umekwisha.

Imeelezwa kuwa wakati kijana huyo akishushiwa kipigo na walinzi hao, mdogo wake, Lydia Lefi, alisikika akiwataka waache kumpiga ndugu yake kwa kuwa walikuwa wanakwenda kuchukua dawa.

... uliwahi kuletwa uzi humu kwamba hao wanaoitwa walinzi wa SUMA JKT most of them wana matatizo ya kisaikolojia. Ether, mafunzo waliyopitia walipata harassment mbaya sana, au mazingira ya kazi (kipato) ni tatizo, etc. Wataalamu wa ustawi wa jamii wanaweza kufanya research zao wakaja na majibu kwanini hawa vijana wana majibu na matendo ya ajabu ajabu.
 
Hao walinzi labda huko mafunzoni wanadukuliwa mtandao pendwa Joti
 
Hizo ni politics hakuna hatua yeyote itakayochukuliwa na suma jkt,nilitegemea mkuu wa wilaya angeambatana na victims kwenda police station na kufungua mashitaka dhidi ya waziri wa ulinzi na jkt,waziri wa afya,mkuu wa hospital husika na walinzi wahusika na kuiachia mahakama iamue kwanza criminal case then kesi ya madai.5 mingine na haki kama hii ndoto ndani ya nchi yetu.
 
Askari akifanya criminal act , hiyo inamhusu yeye mwenyewe tu.
Hapo ni kufungua malamiko polisi ili hatua nyingine ziendelee.
 
Hawa Hawa Suma Jkt

Waliua mtoto wa miaka kumi na moja ,Tena kwa risasi zaidi ya tano...
Kisa kuingiza mifugo ndani ya msitu, unaofahamika kwa jina ' Forest' huko Arusha...

Kisha wakampiga risasi ya mguu mzee , mmoja
Kwa kosa Hilo hilo la kuingiza mifugo , ila mzee huyu aliingiza mifugo kwenye mashamba ya serikali , huko Arusha mashamba hayo yanafahamika Kama mashamba ya kilimo...

Idara husika iwaangali hawa Suma Jkt kwa jicho la tatu...
 
... uliwahi kuletwa uzi humu kwamba hao wanaoitwa walinzi wa SUMA JKT most of them wana matatizo ya kisaikolojia. Ether, mafunzo waliyopitia walipata harassment mbaya sana, au mazingira ya kazi (kipato) ni tatizo, etc. Wataalamu wa ustawi wa jamii wanaweza kufanya research zao wakaja na majibu kwanini hawa vijana wana majibu na matendo ya ajabu ajabu.
Kama umeshawahi pitia haya mafunzo. Jeshini harrasment ni kitu cha kawaida.. yaani ni daily.

I dont know kwann waliweka vile.. maybe kumjenga mtu kisaikolojia.

Lakin in reality si wote wana cope na hiyo harrasment. Ndio maana wengine wakitoka wanakuwa visirani.

Sijajua mafunzo ya suma jkt yakoje. Ila wanatakiwa wawe wanapelekwa training za ulinzi mbali na JKT training yenyewe. Before hawajawa deployed
 
Askari akiganya criminal act , hiyo inamhusu yeye mwenyewe tu.
Hapo ni kufungua malamikonpolisi ili hatua nyingine ziendelee.
Ndio maana if u read underlines nimeelezea hili hapo kuna criminal case na civil one,kuwahusisha niliowataja hapo ni about accountability ya nafasi zao!mkuu tunahitaji tupate a glass of wine together!!
 
Kama umeshawahi pitia haya mafunzo. Jeshini harrasment ni kitu cha kawaida.. yaani ni daily...
... harassment, as you have said, is normal in military trainings, but won't affect you much as you know there is "hope" at the end of the "tunnel". Tatizo linakuwa kubwa pale unapokuwa harassed, yet when you come to the ground the situation is even worse! Hapa lazima uwe "mnyama".
 
Mkuu wa wilaya Shinyanga, Jasinta Mboneko, ameuagiza uongozi wa kampuni ya ulinzi ya Suma JKT, kuwachukulia hatua kali za nidhamu walinzi waliohusika kwenye tukio la kumpiga mwananchi Daudi Lefi, aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo kumuhudumia mgonjwa...

MK254
 
Mwaka Jana walinzi wa Suma jkt inasemekana walimuua kiongozi wa timu ya Coastal Union pale Jangwani sidhani kama kuna hatua imechukuliwa dhidi ya vibaka hawa

Miaka ya 2013 kuna askari kiongozi wa suma jkt nzega alikuwa na mashitaka ya kuua mchimbaji mdogo mgodini sijui naye aliishia vipi?
 
Kama umeshawahi pitia haya mafunzo. Jeshini harrasment ni kitu cha kawaida.. yaani ni daily.
I dont know kwann waliweka vile.. maybe kumjenga mtu kisaikolojia.
Lakin in reality si wote wana cope na hiyo harrasment. Ndio maana wengine wakitoka wanakuwa visirani.

Sijajua mafunzo ya suma jkt yakoje. Ila wanatakiwa wawe wanapelekwa training za ulinzi mbali na JKT training yenyewe. Before hawajawa deployed

Tafuta maana ya PTSD... mafunzo ya kwetu Afrika huwa ni kukomoana, unakuta kurutu anacharazwa viboko balaa eti mafunzo.
 
Hizo ni politics hakuna hatua yeyote itakayochukuliwa na suma jkt,nilitegemea mkuu wa wilaya angeambatana na victims kwenda police station na kufungua mashitaka dhidi ya waziri wa ulinzi na jkt,waziri wa afya,mkuu wa hospital husika na walinzi wahusika na kuiachia mahakama iamue kwanza criminal case then kesi ya madai.5 mingine na haki kama hii ndoto ndani ya nchi yetu.
Aliepigwa alishasamehe mbele ya wanadamu na mbele za Mungu
 
Back
Top Bottom