Watu wa sheria kama wapo hivi hatuwezi kufungua kesi kwa huu ukiukwaji wa sheria???
Serikali dhaifu huzaa vitendo vya ajabu ajabu, tume ya uchaguzi ilikuwa wapi????Kama demokrasia ndiyo hii basi nachelea kusema imevuka mipaka na kukoma zaidi hata ya nchi za magharibi.Hali hii imejitokeza siku ya Jumapili ya tarehe 24/06/2012 mkoani Shinyanga kata ya Masekelo maarufu kama kambi ya upinzani mkoani humo mtaa wa bondeni.Kitendo kilicho washangaza wapiga kura ni kwa jeshi la Polisi kuchukua dhima ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kinacho shangaza ni sheria gani iliyotumika kwa jeshi la polisi kugeuka tume ya uchaguzi na kutangaza matokeo ya uchaguzi huu ambao matokeo yake yalitangazwa mnamo mida ya saa tano usiku, kitendo kilicho sababisha mabomu ya machozi kurindima na kuwatawanya wakazi wa maeneo hayo ya Bondeni.Kama hali ndiyo hii basi demokrasia nchini mwetu imevuka mipaka na kushinda hata nchi za magharibi.
Wakuu wana JF tujaribuni kuliweka sawa hili kama kweli sheria za uchaguzi zina ruhusu chombo cha dola kuchukua majukumu hayo.
Source sammosses from Shinyanga
Huu ni ukibaka wa demokrasia. Hivi hawa polisi wa miaka hii wanafundishwaje?
kwa hiyo unamaanisha yatakuwa yanatolewa kwenye kambi za jeshi