Shinyanga: Polisi kutangaza matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa inakubalika kisheria?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Kama demokrasia ndiyo hii basi nachelea kusema imevuka mipaka na kukoma zaidi hata ya nchi za magharibi.Hali hii imejitokeza siku ya Jumapili ya tarehe 24/06/2012 mkoani Shinyanga kata ya Masekelo maarufu kama kambi ya upinzani mkoani humo mtaa wa bondeni.Kitendo kilicho washangaza wapiga kura ni kwa jeshi la Polisi kuchukua dhima ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kinacho shangaza ni sheria gani iliyotumika kwa jeshi la polisi kugeuka tume ya uchaguzi na kutangaza matokeo ya uchaguzi huu ambao matokeo yake yalitangazwa mnamo mida ya saa tano usiku, kitendo kilicho sababisha mabomu ya machozi kurindima na kuwatawanya wakazi wa maeneo hayo ya Bondeni.Kama hali ndiyo hii basi demokrasia nchini mwetu imevuka mipaka na kushinda hata nchi za magharibi.

Wakuu wana JF tujaribuni kuliweka sawa hili kama kweli sheria za uchaguzi zina ruhusu chombo cha dola kuchukua majukumu hayo.

Source sammosses from Shinyanga
 
Ndo hayo hayo! Serikali inasimamiwa na bunge, bunge nani analisimamia? Mahakama nani anazisimamia tofauti na wao kwa wao? Tume ya uchaguzi nani anawasimamia kuendesha chaguzi, hata kama iko chini ya serikali! tunahitaji wembe mkali wa kukata hizi fitina za kijinga tena za kujitakia.
 
Yani huo ni ubakaji mkubwa wa demokrasia na ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi nadhani hawa polisi wanasahau kuwa wao wanahamasisha kutii sheria bila shuruti lakini kwa wao kuwa wa kwanza kuvunja sheria sijui wanatufundisha nini nadhani huo uchaguzi ni kama haujafanyika sababu mshindi ametangazwa na wahuni wa jeshi la polisi.
 
Ndo hayo hayo! Serikali inasimamiwa na bunge, bunge nani analisimamia? Mahakama nani anazisimamia tofauti na wao kwa wao? Tume ya uchaguzi nani anawasimamia kuendesha chaguzi, hata kama iko chini ya serikali! tunahitaji wembe mkali wa kukata hizi fitina za kijinga tena za kujitakia.
upo sahii mkuu
 
Heh! wameibaka democrasia... udhaifu mpaka kwenye vyombo vya dola.
 
Viongozi wa CDM mkoa wanalifuatilia jambo hili kwa mkurugenzi wa manispaa kwa kuwa ndiye msimamizi mkuu wa uchaguzi ndani ya majimbo,ili aweze kujibu hoja.
 
Huyo Polisi aliyekubali kutumika kiasi hicho ana elimu gani? Tusijekuwa tunamwonea. Duh usipokuwa mwerevu unaweza kutumika kwa lolote
 
hakushinda mgombea wa CCM wanayarudia waliyofanya kwenye uchaguzi wa Raisi 2010,lakini huyo mwenyekiti atafanya kazi na nani wananchi si wamemkataa
 
Huyo Polisi aliyekubali kutumika kiasi hicho ana elimu gani? Tusijekuwa tunamwonea. Duh usipokuwa mwerevu unaweza kutumika kwa lolote

Ni wajinga tu ndiyo watakao haingaika kuitafuta busara,mara ngapi wanatumiwa wakisha tekeleza Uyuda wao wanarudi mitaani kuomba suluhu.
 
Kama demokrasia ndiyo hii basi nachelea kusema imevuka mipaka na kukoma zaidi hata ya nchi za magharibi.Hali hii imejitokeza siku ya Jumapili ya tarehe 24/06/2012 mkoani Shinyanga kata ya Masekelo maarufu kama kambi ya upinzani mkoani humo mtaa wa bondeni.Kitendo kilicho washangaza wapiga kura ni kwa jeshi la Polisi kuchukua dhima ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kinacho shangaza ni sheria gani iliyotumika kwa jeshi la polisi kugeuka tume ya uchaguzi na kutangaza matokeo ya uchaguzi huu ambao matokeo yake yalitangazwa mnamo mida ya saa tano usiku, kitendo kilicho sababisha mabomu ya machozi kurindima na kuwatawanya wakazi wa maeneo hayo ya Bondeni.Kama hali ndiyo hii basi demokrasia nchini mwetu imevuka mipaka na kushinda hata nchi za magharibi.

Wakuu wana JF tujaribuni kuliweka sawa hili kama kweli sheria za uchaguzi zina ruhusu chombo cha dola kuchukua majukumu hayo.

Source sammosses from Shinyanga
Mkuu ndiyo Tanzania yetu hiyo...rejea uchaguzi wa meya wa Arusha polisi waliingia kwenye ukumbi wa madiwani na kuwatoa chadema....je uliwahi kuona pilosi kaingia bungeni na kuwatoa watu fulani...tutauondoa huu uhuni kwenye katiba mpaya na mwisho wao ni 2015....
 
Siku zote mtu hukifuata kifo chake yeye mwenyewe ama kwa mikono yake au juhudi zake kuelekea kifo hicho.Kitendo cha serikali kutoona mapungufu yake na kutokusikia kilio cha wengi ni hatua kubwa kuelekea kifo chake.Tutaona upungufu mkubwa na kuteleza kwingi ambako ndiko kifo kilipo pangiwa.
 
Sasa hiyo ni 2012 tu.................. 2015 JWTZ ndiyo watatangaza matokeo............. Si mnakumbuka ule mkwala wa Shimbo 2010???
 
kwa hiyo unamaanisha yatakuwa yanatolewa kwenye kambi za jeshi

Yawezekana,walikwisha sema hawezi kuikabidhi nchi kwa makaratasi,tunachosubiri ni suala la wakati ufike tuone na tupo tayari kwa lolote.Wazalendo wa kweli ndiyo pekee wataojenga nchi kwa kuipigania mpaka tone la mwisho
 
Hawana nguvu ya ushawishi kwahiyo wanaona afadhali watumie mabavu!! Serikali ya magamba imechemsha na walivyofilisika kiakili watasema madaktari wanatumiwa na wapinzani as if hao madaktari hawana akili zao!!
 
kwa hiyo unamaanisha yatakuwa yanatolewa kwenye kambi za jeshi

jamani msiogope, kabisa jeshi liko nyuma yenu, shimbo si mwanasiasa tu, shimbo sio mtendaji wa jeshi, kwanza nawahabarisha ni swaiba yake mkubwa Dhaifu ndo maana kauli kama ile ilitolewa. Askari na maafisa wa ngazi ya chini hatupo nae na ndo watendaji. msihofu si mliona hata misri...jeshi linaheshimu peoples power ndo maana likaitwa la wananchi sio polisi wa takukuru wala usalama wa ccm.
 
Back
Top Bottom