beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Majengo mawili ya nyumba za walimu ambayo ujenzi wake haujakamilika katika Shule ya Sekondari Mwasele, Kata ya Kambarage, Manispaa ya Shinyanga, yamedaiwa kugeuzwa danguro na kusababisha baadhi ya wanafunzi kupewa ujauzito na kuacha masomo.
Diwani wa Kambarage, Hassani Mwendapole, alipaza kilio hicho wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la manispaa hiyo kilichojadili utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20 ya Sh. bilioni 41.5 kwa kipindi cha nusu mwaka.
Alidai miradi mingi ya maendeleo imeendelea kuwa kiporo, zikiwamo nyumba mbili za walimu zilizoko katika shule hiyo, ambazo kwa sasa zimegeuka kuwa 'guest house' na kusababisha ujauzito kwa wanafunzi shuleni hapo.
“Nyumba hizi za walimu katika Shule ya Sekondari Mwasele zilijengwa tangu mwaka 2011 na sasa kuna mapagale tu, na yameshageuka kuwa kama guest house, zinatumika kwa ngono na kusababisha kuwapo mimba za wanafunzi," alilalamika.
Diwani wa Viti Maalum, Shela Mshandete, alitoa ushuhuda kuwa kwenye majengo hayo ya nyumba za walimu ambayo hayajakamilika kujengwa, kuna wanafunzi walishakamatwa wakifanya ngono.
Pia Diwani wa Mwamalili, Paulo Machela, alisema kuna haja ya kukamilisha miradi ya maendeleo ambayo ni viporo, akieleza kuwa mingi ilijengwa kwa nguvu za wananchi.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, John Kisandu, aliuagiza uongozi wa manispaa hiyo kuhakikisha hadi kufikia Juni mwaka huu, unakamilisha miradi ambayo ni viporo, na ile ambayo haitakamilika, iingizwe kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi, alisema tayari alishamwagiza mchumi wa manispaa hiyo, Gwakisa Mwashebya, afuatilie miradi yote ambayo ni viporo ili kupata idadi kamili.
Chanzo: IPP Media