Shinyanga: Mume aua mke wake kwa Panga akimtuhumu kusaliti Ndoa yao

Mwanaume anayejulikana kwa jina la Heneriko John (53) mkazi wa Manispaa ya Shinyanga, amedaiwa kumuuwa mke wake Regina Jiyenze (45) kwa kumkata mapanga kichwani na mabegani, kisha kujisalimisha kwa Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 5, saa tatu asubuhi katika Mtaa wa Mbulu Kata ya Mhongolo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Kyando amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, ambapo mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa sio mwaminifu kwenye ndoa yao, kitendo ambacho kilimfanya mtuhumiwa kujichukulia sheria mkononi na kumkata mapanga na kusababisha mauaji.

“Katika eneo la tukio tumeokota panga lenye damu likiwa umbali wa mita 20 kutoka katika eneo la tukio lilipotendeka, mtuhumiwa tunamshikilia mara baada ya kujisalimisha mwenyewe, na tutamfikisha mahakamani baada ya upelelezi kukamilika,” amesema Kyando.

“Mtuhumiwa alitumia mbinu ya kumvizia mke wake na kumkata mapanga wakati akiwa nyumbani kwa balozi Manungu Bundala, alipofika kwa ajili ya kushitaki kutishiwa kuuawa na mume wake, ndipo alipokatwa mapanga sehemu za kichwani na mabegani na kufariki dunia,” amesema.

Aidha kamanda alitoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi kisa wivu wa mapenzi, kwani kitendo hicho hakifai na kinaonekana kimekuwa sugu.

Ametoa ushauri kwa wapenzi au wanandoa, kuwa wakiona mwenzake sio mwaminifu kwenye mahusiano ni bora waachane kuliko kuchukua hatua mbaya kama hiyo.

Chanzo: Mwananchi
Daah, anyway, maisha hayana formula.
 
Hai apply kama mtuhumiwa mwenyewe ame confess. Kama angekuwa anayakana mashtaka basi ndio inahitaji ushahidi ili kumpata na makosa. Kama ame confess mwenyewe ushahidi wa nini sasa?
Kukiri kosa ndo kutenda kosa? what if huyo jamaa alitumwa na mtu amuue huyo mke baada ya kuwa na Siri nzito juu ya Jambo fulani.?

Hata Kama mtu makiri kosa lazima uchunguzi ufanyike mkuu!!
 
Watu wa mikoani wapo serious sana

Kuna yule boya alimpiga faini mtu kisa uroda yaani ni matakataka

Sijui mavyakula wanayokula yanawapunguzia akili kisha yanawaongezea nyege
Aliyemchoma mpenziwe moto kwenye nyumba alikuwa wa mkoani?
 
Wanaumme wajifunze kuvumilia, mbona wake zao wanavumilia!! Mwanamme anaweza kwa na kimada, na watoto, na kila mtu anajua, mke anamvumilia na kuendelea na ndoa .
Ndo maana wanakufa haraka maana wanajaza mizigo mingi vichwani mwao,na stress kibao
 
Ila hizo kesi mikoa hiyo ni kama zimekithiri ni kwamba wenzetu wa pande hizo ndo wanawivu sana na roho ngumu hivo!
 
... uko sahihi. Mojawapo ya document muhimu kwenye kesi za jinai mahakamani ni Hati ya Mashtaka yaani Charge Sheet ambayo ina maelezo yote muhimu kuhusiana na kesi husika ikiwemo taarifa za vyombo mbalimbali vinavyohusika. Kwa mfano, ni lazima daktari wa magonjwa ya akili athibitishe kama mhusika yuko sawasawa kichwani, n.k.

Charge Sheet haiwezi kuwa na just maelezo eti MTUHUMIWA ALIKIRI! Pamoja na kukiri mwenyewe kwa mfano na daktari pia kuthibtisha ni mzima kichwani; je, hapakuwa na force nyingine behind? Kwa mfano, hapakuwa na wahusika wengine walioshirikiana na mhusika kupanga mauwaji hayo? Hawa nao ni lazima wapatikane na kufikishwa mahakamani. Utawapataje bila uchunguzi? Chaliifrancisco
Umemaliza kila kitu mkuu
 
Eti atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika. Mtuhumiwa kaua mbele ya balozi, akajipeleka mwenyewe Polisi kuwaambia nimeua, sasa upelelezi gani wanautaka?

Maiti ipo, panga lipo, balozi yupo, mtuhumiwa yupo!

Polisi bhana!
 
Waafrika na wahindi kwa ukatili/mauwaji hawatofautiani sana. Kidoooogo wahindi wanauafazali ingawa wengiwao wana roho mbaya na wabaguzi.
Europeans and Americans pia ni makatili, wao vyombo vyao vya habari na social medias huwa havihubiri sana uovu wao.
 
Watu wa mikoani wapo serious sana

Kuna yule boya alimpiga faini mtu kisa uroda yaani ni matakataka

Sijui mavyakula wanayokula yanawapunguzia akili kisha yanawaongezea nyege
😀😀😀😀equation haibalance ...........jamaaa wapo sensitive sana
 
Back
Top Bottom