Shinyanga: Mabinti waogeshwa dawa inayodaiwa kuvutia Wanaume. Serikali yaombwa kupiga marufuku

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali imeombwa kupiga marufuku vitendo vya baadhi ya wazazi kuwapeleka mabinti wao wenye umri kati ya miaka 10 hadi 15 kuogeshwa dawa la kuvutia wanaume maarufu ‘samba’ kwa kuwa vinachochea maambukizi ya virusi vya Ukimwi na mimba za utotoni.

Ombi hilo, limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kivulini linalojihusisha kupinga ukatili kwa watoto na wanawake, Yassin Ally.

Alisema vitendo hivyo vinakwenda kinyume na mikakati ya Serikali ya kutokomeza Ukimwi na mimba za utotoni.

1.jpg

Alisema vitendo hivyo, vinafanyika kwa wingi Mkoa wa Shinyanga na kufafanua hivi karibuni alikwenda kutoa semina kwa baadhi ya shule ndani na kuelezwa wanafunzi wa kike wamekuwa wakikosa masomo kutokana na kwenda kuogeshwa.

“Wiki iliyopita nilikwenda Mkoa wa Shinyanga, nilifika baadhi ya shule na kukuta wasichana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 15 ni watoro, nilipodadisi sababu ya kushindwa kufika niliambiwa wanakwenda kuogeshwa dawa za mvuto maarufu Samba," amesema.

“Cha ajabu walimu wanajua kabisa, watendaji wa vijiji, vitongoji na hata waratibu elimu wanafahamu lakini wanashindwa kuchukua hatua ili kukomesha mila na desturi za ajabu ambazo zinasababisha watoto kuingia kwenye maradhi na mimba za utotoni.

“Wito wnagu Serikali kupitia kwa wakuu wa mikoa, makamanda wa polisi, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wapige marufuku vitendo hivyo na wafuatilie kwa ukaribu na kuwachukulia hatua wazazi ambao watabainika kujihusisha na imani potofu, haiwezekani ukamvutia mwanaume kwa dawa ili apende binti, acheni binti akifikisha umri atachagua mwanaume anayempenda,”alisema.

Alisema vitendo hivyo, vinaibuka mikoa ya kanda ya ziwa kutokana na kushamiri kwa waganga wa jadi ambao wamejiegesha katika taaluma hiyo, lengo kubwa ni kutafuta kipato.
 
Back
Top Bottom