Shinyanga: Kiongozi wa CHADEMA aumizwa vibaya, akimbizwa hospitali

taarifa zilizopatikana leo jioni vijana hawa walimshambulia kiongozi huyo wa CDM wameachiwa KWA DHAMANA ILIHALI hali ya mgonjwa bado haijaimarika, hali inayo sababisha wananchi kutokuwa na imani na jeshi la polisi kiasi cha kupelekea kuaminika Polisi naye ni mshindani wa pili baada ya CCM

Kama ni hivyo? KWANINI wasiwaachie SHEIKH PONDA na FARID - UAMSHO???
 
JUMAMOSI, OCTOBA 27, 2012 09:58 NA SAM BAHARI, SHINYANGA

HALI ya kisiasa nchini imeendelea kuwa mbaya baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Tawi la Mwawaza, Bundala Katunge, kuchomwa mkuki na watu wanaosadikiwa ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tukio hilo, lilitokea Oktoba 24, mwaka huu saa 7.30 usiku, ambapo kundi la watu wanaokadiriwa kufikia kumi, kumvamia kiongozi huyo kisha kumchoma mkuki sehemu za tumboni.

Akizungumza kwa taabu na MTANZANIA akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, wodi namba 5, Katunge alisema, watu waliomvamia ni wafuasi wa CCM, ambao amekuwa akipambana nao katika masuala ya kisiasa.

"Kumekuwa na uhasama mkubwa mno eneo hili, hawa watu nawatambua vizuri ni wana CCM, ambao wamenichoma mkuki namna hii,

…nakumbuka nikiwa nimelala usiku, nilisikia kishindo kizito nje nikaamua kutoka, nikaona watu wanashusha bendera ya chama changu, ghafla wakanivamia," alisema Katunge.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Mwawaza, Kulwa Tungu alisema, kampeni za udiwani katika kata hiyo, zinaendeshwa kwa ubabe tofauti na kampeni zozote zilizowahi kutokea miaka ya nyuma.

"Mimi sijawahi kuona uchaguzi kama huu, inapofika usiku utaona vijana wengi kutoka kata za jirani, wanazunguka ndani ya maeneo yetu usiku kucha wakiwa wamevaa makoti na kofia nyeusi, huku wakiwa na vipande vya nondo na mapanga… hali hii imesababisha kutoweka kwa amani," alisema Tungu.

Tukio la kwanza lilitokea Oktoba 19, mwaka huu saa moja usiku, baada ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Kata ya Mwawaza, Shija John kuvamiwa nyumbani kwake na kundi la watu kumi, kisha kushambuliwa na kumsababisha maumivu makali.

John ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Bugimbagu, kata ya Mwawaza, alidai vijana waliomvamia na kumpiga na kumuumiza ni wafuasi wanaodaiwa kuwa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi mkoani Shinyanga, watuhumiwa hao wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM, wametiwa mbaroni na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kuanzia Jumatatu ijayo.

Afisa mmoja wa Polisi, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema wahusika wote watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.

"RPC wa Shinyanga, ameapa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hawa! Amesema hawezi kukubali kundi la watu wachache, waendelee kuvunja amani bila sababu ya msingi," alisema ofisa wa polisi.


Hayatozuka ya kuambiwa naye alikuwa Al-Qaida????
 
Inawekana vipi wapewe dhamana!! Au ndo wanataka wasikose kupiga kura? Zis kantry bwana!?
 
Wakuu, sina cha kusema zaidi kumwomba Mwenyezi Mungu aepushie mbali kadhia hii ya machafuko tarajiwa katika nchi ya TZ, na kamanda aliyejeruhiwa apate nafuu mapema.
 
Back
Top Bottom