kson m
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 6,648
- 3,003
Kuna jamaa yangu wa karibu alidumu ktk ndoa miaka 7 na akapata mtoto mwaka wa 8.sasa anao watoto wawili !! Maamuzi ya haraka hayajengi...jipe muda na omba ushauri .
Sent using Jamii Forums mobile app
HABARI MPYA: Askari Polisi Gideon Clement (30) wa kituo kikuu Cha Polisi Mjini Kahama Mkoa wa Shinyanga amejiua kwa kujipiga risasi asubuhi ya leo wakati akiwa kwenye lindo Benki ya Access tawi la Kahama
Marehemu ameacha ujumbe wa maandishi kwa njia ya simu kwa mke wake akieleza sababu ya kujiua ni kutokana na kukosa mtoto hivyo hajaona sababu ya kuendelea kuishi
Taratibu za mazishi zinaendelea
Habari zaidi...
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao amesema sababu za askari huyo kujiua ni kutokana na kutofanikiwa kupata mtoto licha ya kuishi kwenye ndoa na mkewe kwa muda wa miaka mitano.
"Sababu za kujiua kwake ameeleza kwa ujumbe aliotuma kwa mke wake kwamba hana sababu za kuendelea kuishi kwa sababu hajajaliwa kupata mtoto na amekaa kwenye ndoa kwa muda wa miaka mitano na mke wake ambaye ni mwalimu na inasemekana jana alilalamikia sana jambo hilo na alianza kuonesha dalili kwa kumtumia mkewe ujumbe wa simu akieleza kuhusu mali zake vikiwemo viwanja viko wapi",ameeleza Kamanda Abwao.
Kamanda Abwao amesema taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Muleba kwa ajili ya mazishi zinaendelea.
Sent using Jamii Forums mobile app