Shinyanga Kahama: Askari ajiua kwasababu ya kukosa watoto

Hizi benki zingine hovyo kabisa matawi utadhani dula wakala wa mpesa. Ona sasa hadi askari wetu amejiua.

Sababu ya kukosa mtoto kwenye 30s haina mashiko. Hawa askari wana usongo mkubwa sana wa mawazo, wamejaa matatizo chungu nzima. Mishahara yao kiduchu mno. Wanaishi kwa tabu sana ndio maana wakiambiwa waje kutuzuia tu basi watatupiga utadhani kuku kala mahindi. Nyie askari mna shida kama sisi, jiongezeni
 
Inategemea na Jamii aliyo kuwa anaishi nayo walikuwa wanamatashi gani kwake.
nimehisi ivo pia na washkaji ndo chanzo kumpigia kelele vp wew huna mtoto mpk sas anajiona hana thman tena ktika jamii iliyomzunguka..pole kwa wafiwa
 
Kukosa mtoto kusikie tu kwa jirani
Kweli. Mmmhh hicho kitu cha kukosa mtoto hlf imeonekana mmojawapo ana tatizo kinauma sana...watu wasikie tu....ila tatizo kubwa litakua katika fikra za mwenye tatizo baada ya kulijua tatizo kweny mwili wake na asipopata ushaur wa kitaalam ndy kama hivy anajiua
 
Kweli. Mmmhh hicho kitu cha kukosa mtoto hlf imeonekana mmojawapo ana tatizo kinauma sana...watu wasikie tu....ila tatizo kubwa litakua katika fikra za mwenye tatizo baada ya kulijua tatizo kweny mwili wake na asipopata ushaur wa kitaalam ndy kama hivy anajiua
Itakuwa aligundua yeye ana tatizo, ingekuwa tatizo lipo kwa mke jamaa angetafuta mwingine wa kuzaa nae! Sad!
 
HABARI MPYA: Askari Polisi Gideon Clement (30) wa kituo kikuu Cha Polisi Mjini Kahama Mkoa wa Shinyanga amejiua kwa kujipiga risasi asubuhi ya leo wakati akiwa kwenye lindo Benki ya Access tawi la Kahama

Marehemu ameacha ujumbe wa maandishi kwa njia ya simu kwa mke wake akieleza sababu ya kujiua ni kutokana na kukosa mtoto hivyo hajaona sababu ya kuendelea kuishi

Taratibu za mazishi zinaendelea

Habari zaidi...

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao amesema sababu za askari huyo kujiua ni kutokana na kutofanikiwa kupata mtoto licha ya kuishi kwenye ndoa na mkewe kwa muda wa miaka mitano.

"Sababu za kujiua kwake ameeleza kwa ujumbe aliotuma kwa mke wake kwamba hana sababu za kuendelea kuishi kwa sababu hajajaliwa kupata mtoto na amekaa kwenye ndoa kwa muda wa miaka mitano na mke wake ambaye ni mwalimu na inasemekana jana alilalamikia sana jambo hilo na alianza kuonesha dalili kwa kumtumia mkewe ujumbe wa simu akieleza kuhusu mali zake vikiwemo viwanja viko wapi",ameeleza Kamanda Abwao.

Kamanda Abwao amesema taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Muleba kwa ajili ya mazishi zinaendelea.
R.I.P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hatari sana kwa watu wenye uwezo huu wa kufikiri kushinda na kukesha na silaha,Labda jogoo hasimami kabisa ILA kwa sababu yake ni nonsense.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom