Shinyanga: DC alowaweka Korokoroni masaa 48 Watetezi wa Haki za binadamu, akaliwa kooni | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shinyanga: DC alowaweka Korokoroni masaa 48 Watetezi wa Haki za binadamu, akaliwa kooni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by figganigga, Jul 16, 2017.

 1. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2017
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 15,320
  Likes Received: 7,409
  Trophy Points: 280
  WATETEZI WAWILI WA HAKI ZA BINADAMU WALIKAMATWA NA POLISI KATIKA WILAYA YA KISHAPU- MKOANI SHINYANGA.

  Watetezi wawili wa haki za binadamu wanaojihusisha na uwajibikaji wa jamii na secta ya madini walikamatwa na Maafisa wa Polisi katika Wilaya ya Kishapu- Mkoa wa Shinyanga. Bibi Anna Mushi na Nicolaus Ngelela waliokua wakifanya kazi kwa niaba ya shirika la Action for Democracy and Local Government (ADLG) lenye ofisi zake mjini Shinyanga walikamatwa tarehe 12 Julai 2017 wakati wakifanya semina ya kujenga uwezo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizo karibu na maeneo yenye uwekezaji wa madini.

  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Ndugu Jimmy Luhende aliiambia THRDC kuwa Shirika lake limekuwa likifanya semina katika vijiji kadhaa kuanzia tarehe 11 Julai 2017 na walikuwa karibu kukamilisha mpango huo kwa kutembelea vijiji vitano katika wilaya hiyo. Siku ya tukuo, baadhi ya wafanyakazi wa ADLG walifika mahali ambapo semina ilitakiwa kufanywa na kumuona Mkuu wa Wilaya akiwa amewasili eneo hilo akiwa na Maofisa wa Polisi.

  Mara baada ya semina hiyo kuanza Maofisa wa Polisi waliwakamata watetezi hao wa haki za binadamu kutoka ADLG kufuatia amri ya Mkuu wa Wilaya ya masaa 48. Ndugu Luhende alisema. Maofisa wa Polisi hawajathibitisha mashtaka dhidi ya Bibi Anna na Ngelela.

  Hata hivyo, inadaiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ndiye aliyeamuru kukamatwa kwao kwa madai kuwa ofisi yake haikupewa taarifa kuhusu mkutano huo.

  THRDC leo imetoa kauli ya kukemea vitendo hivyo.


  My Take:

  Tuoneeni huruma tumetubu.
   
 2. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #41
  Jul 17, 2017
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,231
  Likes Received: 562
  Trophy Points: 280
  Hii tabia ya baadhi ya viongozi awamu ya 5 ni "Terrorism per se" Askari kamata polisi

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 3. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #42
  Jul 17, 2017
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,231
  Likes Received: 562
  Trophy Points: 280
  Evolution inaendelea kwenye ubongo wako.
  Hayo uliyojiuliza ni obvious kwa binadam wa kawaida


  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 4. a

  amaninginana Member

  #43
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 7, 2015
  Messages: 12
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Bado kidogo maji tutayaita mma, is a matter of time tu


  ahaaaaaaaaaaaaaaaa aisee htr
   
 5. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #44
  Jul 18, 2017
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 24,702
  Likes Received: 24,822
  Trophy Points: 280
  Huyo alipewa u DED
   
Loading...