Shinyanga: DC alowaweka Korokoroni masaa 48 Watetezi wa Haki za binadamu, akaliwa kooni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shinyanga: DC alowaweka Korokoroni masaa 48 Watetezi wa Haki za binadamu, akaliwa kooni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by figganigga, Jul 16, 2017.

 1. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2017
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,612
  Trophy Points: 280
  WATETEZI WAWILI WA HAKI ZA BINADAMU WALIKAMATWA NA POLISI KATIKA WILAYA YA KISHAPU- MKOANI SHINYANGA.

  Watetezi wawili wa haki za binadamu wanaojihusisha na uwajibikaji wa jamii na secta ya madini walikamatwa na Maafisa wa Polisi katika Wilaya ya Kishapu- Mkoa wa Shinyanga. Bibi Anna Mushi na Nicolaus Ngelela waliokua wakifanya kazi kwa niaba ya shirika la Action for Democracy and Local Government (ADLG) lenye ofisi zake mjini Shinyanga walikamatwa tarehe 12 Julai 2017 wakati wakifanya semina ya kujenga uwezo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizo karibu na maeneo yenye uwekezaji wa madini.

  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Ndugu Jimmy Luhende aliiambia THRDC kuwa Shirika lake limekuwa likifanya semina katika vijiji kadhaa kuanzia tarehe 11 Julai 2017 na walikuwa karibu kukamilisha mpango huo kwa kutembelea vijiji vitano katika wilaya hiyo. Siku ya tukuo, baadhi ya wafanyakazi wa ADLG walifika mahali ambapo semina ilitakiwa kufanywa na kumuona Mkuu wa Wilaya akiwa amewasili eneo hilo akiwa na Maofisa wa Polisi.

  Mara baada ya semina hiyo kuanza Maofisa wa Polisi waliwakamata watetezi hao wa haki za binadamu kutoka ADLG kufuatia amri ya Mkuu wa Wilaya ya masaa 48. Ndugu Luhende alisema. Maofisa wa Polisi hawajathibitisha mashtaka dhidi ya Bibi Anna na Ngelela.

  Hata hivyo, inadaiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ndiye aliyeamuru kukamatwa kwao kwa madai kuwa ofisi yake haikupewa taarifa kuhusu mkutano huo.

  THRDC leo imetoa kauli ya kukemea vitendo hivyo.


  My Take:

  Tuoneeni huruma tumetubu.
   
 2. Hussein Melkiory

  Hussein Melkiory JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2017
  Joined: Jan 25, 2016
  Messages: 4,682
  Likes Received: 5,691
  Trophy Points: 280
  Duuu,,,,,sawa
   
 3. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2017
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,666
  Likes Received: 21,892
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa ma DC wa sasa wanatumia sheria gani ambazo hazikuwepo awamu zilizopita? Huu ushamba ulioanzia juu unakuja kwa kasi sana chini. Hili jambo likomeshwe kwa nguvu zote.
  Sii waende Kibiti wakatumie hiyo sheria nasi tutawaona wanajua kazi kweli?
   
 4. kirikou1

  kirikou1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2017
  Joined: Nov 8, 2016
  Messages: 2,902
  Likes Received: 3,535
  Trophy Points: 280
  Bado kidogo maji tutayaita mma, is a matter of time tu
   
 5. SDG

  SDG JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2017
  Joined: Feb 28, 2017
  Messages: 6,580
  Likes Received: 6,778
  Trophy Points: 280
  "Nyie mna mamlaka ya kumuweka mtu ndani hadi saa 48"Hii nilikua naiskia sana RFA kabla haijafungiwa na TRA.
  Naona hiki ndo walikisikia wakat wanaapishwa hawakuambiwa majukumu mengine?

  May Allah bless Me and You
   
 6. Dragoon

  Dragoon JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2017
  Joined: Nov 24, 2013
  Messages: 6,415
  Likes Received: 6,414
  Trophy Points: 280
  Kikanuni hakuna uhalali wa kumweka mtu korokoroni masaa 48. Watanzania wanaonewa. makosa yanoyoweza kumuweka mtu korokoroni kwa mda kama huo pasi mtu kuhoji ni unyang'anyi wa kutumia silaha, uhaini ma mauaji. Kuna makosa ya uhujumu uchumi pia yako wazi. Lakini si haki wala si utaratibu kumweka mtu kifungoni kwa zaidi ya saa 24 kwa kesi nje ya zilizoainishwa hapo juu. kwa kifupi wanafanyiwa FALSE IMPRISONMENT, sijui hawajitambui au waoga...
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2017
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,666
  Likes Received: 21,892
  Trophy Points: 280
  Hawa wangeambiwa "mtu akiwabishia jambo mfanyeni hata kinyume na maumbile" wangekuwa wamesha wachakaa wengi kwa vile tuu mteuzi kasema. Bure kabisa hawa. Hawa ni wa ku note majina yao ili wakati ukifika kufufua kesi za jinai za maonezi ili nao kuwaweza sio rumande bali mahabusu kabisa tena zile za magwiji wa uhalifu ili wajue kuwa walifanya ya hovyo.
   
 8. MKWEPA KODI

  MKWEPA KODI JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2017
  Joined: Nov 28, 2015
  Messages: 18,189
  Likes Received: 36,994
  Trophy Points: 280
  Aisee hivi vidikteta vitoto lazima tutafute mbinu ya kuvidhibiti, vinginevyo tukiviacha nchi itaingia kwenye matatizo
   
 9. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2017
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,592
  Likes Received: 25,529
  Trophy Points: 280
  Mnachotakiwa kufanya ni kurekodi majina ya Wakuu wote wa wilaya wanaotumia madaraka yao vibaya , iko siku yatahitajika .
   
 10. tamuuuuu

  tamuuuuu JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2017
  Joined: Mar 10, 2014
  Messages: 8,089
  Likes Received: 4,815
  Trophy Points: 280
  Wapuuzi sn hawa majuha.
  Amnesty international please notify Tanzania

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 11. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2017
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,592
  Likes Received: 25,529
  Trophy Points: 280
  Mnachotakiwa kufanya ni kurekodi majina ya Wakuu wote wa wilaya wanaotumia madaraka yao vibaya , iko siku yatahitajika .
   
 12. McNair

  McNair Senior Member

  #12
  Jul 16, 2017
  Joined: Mar 18, 2017
  Messages: 184
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 60
  Sheria ipi mkuu unarejea?

  Au hujui maana na lengo la saa 48 in cell?

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 13. SDG

  SDG JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2017
  Joined: Feb 28, 2017
  Messages: 6,580
  Likes Received: 6,778
  Trophy Points: 280
  Wakat ndo huu,

  May Allah bless Me and You
   
 14. McNair

  McNair Senior Member

  #14
  Jul 16, 2017
  Joined: Mar 18, 2017
  Messages: 184
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 60
  Kasome upya tena kwa semester moja on false imprisonment

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 15. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2017
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,004
  Likes Received: 37,713
  Trophy Points: 280
  Somebody,somewhere is a prolem
   
 16. MAGHAYOO

  MAGHAYOO Senior Member

  #16
  Jul 16, 2017
  Joined: May 1, 2017
  Messages: 149
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  Hivi suicide vest unaweza kuagiza eBay ama amazon?

  Msaada please
   
 17. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #17
  Jul 16, 2017
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,502
  Likes Received: 2,043
  Trophy Points: 280
  Unatafta Kiki Kwa Pikipiki..

  Msafwa
  Mpoloto, Mbeya
   
 18. U

  UCD JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2017
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 2,336
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Yaani wewe ni mbumbumbu kweli wa sheria nenda kasome sheria ya serikali za mitaa pia hakuna false imprisonment!!
   
 19. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2017
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Kinachofanya kazi ktk taaisi yoyote ili ni roho ya kiongozi........

  Kiongozi mkuu akiwa "boya" taasisi nzima inakuwa boya..

  Angalia:
  Wakati wa Jakaya, Jakaya alikuwa mtu "fair play"... Hivyo maeneno mengi ikawa hivyo .... Hapa nchi iliyoongozwa na roho ya kiongozi ambayo ni "fair".

  Tuangali awamu ya JPM
  JPM ni kiongozi mpenda sifa, mkurupukaji n.k.... Hivyo taasisi zote za chini yake zinaongozwa hivyo hivyo.
  Viongozi wa sasa wanatenda ndipo wafikiri... Hawana muda wa kufikiri ndipo watende .. Hii ni changamoto kubwa sana

  Sent using Nokia toch......
   
 20. mbalizi1

  mbalizi1 JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2017
  Joined: Dec 16, 2015
  Messages: 4,830
  Likes Received: 3,519
  Trophy Points: 280
  Kichomi
   
Loading...