Shinyanga: Bodaboda wafanya vurugu, Polisi watumia mabomu kuwatawanya

marveljt

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
1,503
1,479
Polisi wa kuzuia ghasia wanarusha mabomu ya machozi kukabiliana na wafanyabiashara almaarufu kama boda boda. Sekeseke hilo limetokea baada wa wafanyabiashara hao kuandamana kufuatia kifo cha mwenzao.

Kifo hicho kilichosababishwa na polisi almaarufu kama makirikiri hapo jana baada ya polisi hao kumkimbiza na hivyo kukosa mwelekeo hali iliyosababisha kuangukia mtaroni.

---------

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga leo limewatawanya madereva bodaboda zaidi ya 100 waliokuwa wanaandamana kuelekea eneo la Ibinzamata kwenye msibani kwa dereva mwenzao Joel Mamla (26) ambaye alifariki dunia jana akiwa amempakia askari wa usalama barabarani aliyekuwa amemkamata kwa kosa la kutokuvaa kofia ngumu (Helment).

Joel ambaye alikamatwa na askari waliokuwa kwenye majukumu yao ya kila siku, aliamuliwa kuelekea kituo cha polisi huku akiwa na askari amembeba kwenye pikipiki yake lakini baadaye anadaiwa kuwa alibadilisha uelekeo na kwenda Barabara ya Tinde huku akimwambia askari watakufa pamoja na kisha kuigongesha pikipiki kwenye nguzo ya alama za barabarani na baadaye kufariki dunia huku askari huyo akijeruhiwa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Jumanne Murilo, amekiri kutokea kwa tukio hilo.

“Deereva bodaboda huyo baada ya kukamatwa aliamliwa apelekwe kituoni, ndipo akambemba askari PC Edmond, lakini kabla hawajafika kitunoni, ghafla alielekeza pikipiki mahala pengine huku akimwambia askari lazima wafe wote.

“Wakati pikipiki hiyo ikiwa mwendokasi, askari huyo alianza kujihami kumzuia lakini bahati mbaya hakufanikiwa na hatimaye kusababisha ajali hiyo iliyopelekea kifo,” alisema Kamanda Murilo.

Aidha alisema baada ya tukio hilo wananchi kwa kushirikiana na bodaboda walianzisha vurugu kwa kuwarushia mawe askari polisi, ndipo jeshi hilo lilipotumia nguvu ya ziada kupiga mabomu, ili kuimarisha usalama na hali ya amani ambpo hatimye kufanikiwa kuituliza.

Na:Gabriel Ng’osha/GPL
 
Kule Morogoro kuna vodafasta mmoja anaitwa Lama alishawasababishia vlema waendesha pkpk wengi kwa kuwakimbiza ovyo ila walimchkao siku alisabasha bodaboda mmoja kujiingiza kwnye gali kubwa na laia kuanza kumtembezea chichapo uyo vodafasta mwenzake baada ya kuona laiya wanazidi kumiminika akadandia daladala akakimbia na kumuacha mwenzake akiazibiwa adi leo uyo voda fasta agusi pkpk na hakuna habari ya vodafasta kukimbiza bodaboda..
 
Wafanyabiashara almaarufu kama BODABODA afu eti polisi almaarufu kama MAKHIRIKHIRI.Daah ngoja kwanza ninywe chai...
Kipi kilichokuchanganya? Kuna majina ambayo yapo maarufu zaidi ya majina halisi mfano bodaboda,daladala,mabaka,vodafasta,machozi ya simba,mate ya mende n.k
 
kule morogoro kuna vodafasta mmoja anaitwa *lama* (Rama) alishawasababishia **vlema** (Vilema) waendesha **pkpk** (Pikipiki) wengi kwa kuwakimbiza ovyo ila **walimchkao** siku **alisabasha** (Alisababisha bodaboda mmoja kujiingiza **kwnye gali** (Kwenye gari) kubwa na **laia** (Raia) kuanza kumtembezea **chichapo uyo** (Kichapo huyo) vodafasta mwenzake baada ya kuona **laiya** (Raia) wanazidi kumiminika akadandia daladala akakimbia na kumuacha mwenzake **akiazibiwa** (Akiadhibiwa) adi leo uyo voda fasta agusi **pkpk** (Pikipiki) na hakuna habari ya vodafasta kukimbiza bodaboda..
We jamaa ulikuwa una point...
 
Kweli TZ kuna nyumbu wengi. Hivi ameelewa alichokiandika. Bila shaka huyu ni darasa la nne failed.... Hujui alama za mkato, nukta, koma. Magufuli ana kazi kubwa sana ......:oops:
yani sioni ata cha kukujibu ila wakikupima kama c tikiti au kibaskeli mi najijinyonga...
 
yani sioni ata cha kukujibu ila wakikupima kama c tikiti au kibaskeli mi najijinyonga...
hivi wewe unajiona mzima kweli ? kama sio la nne au la saba aliyefeli mi naacha kazi... Niwekee cheti chako cha ata Diploma tu.. Na kama unacho basi TCU watakua walifanya makosa kusajili hicho chuo ulichosoma...... Nyie ndo Magufuli anakosa usingizi kwa ajili ya kuwaza nyumbu kama hii inayojiona mzima
 
Wacha upuuzi wewe fisiem. Namaanisha Rais ana kazi ya kuhakikisha mitaala inaboreshwa na walimu wanapata mafunzo stahiki ili kuweza kupunguza idadi ya nyumbu kama hawa. Atumie wizara na wataalam husika. Huna akili ya kujiongeza mpaka utafuniwe.. Ngiri pori wapo wengi kweli
Kwani wizara ya elimu haipo?
 
kule morogoro kuna vodafasta mmoja anaitwa lama alishawasababishia vlema waendesha pkpk wengi kwa kuwakimbiza ovyo ila walimchkao siku alisabasha bodaboda mmoja kujiingiza kwnye gali kubwa na laia kuanza kumtembezea chichapo uyo vodafasta mwenzake baada ya kuona laiya wanazidi kumiminika akadandia daladala akakimbia na kumuacha mwenzake akiazibiwa adi leo uyo voda fasta agusi pkpk na hakuna habari ya vodafasta kukimbiza bodaboda..

Na wewe uwe makini, BAKITA watakushughulikia
 
Back
Top Bottom