BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Mkazi mmoja wa Kitongoji cha Mwamala, Kijiji cha Igumanghobo, Kata ya Idukilo Mkoani Shinyanga aliyekuwa akichimba madini katika Kijiji cha Mwang’holo, Kata ya Mwadui Lohumbo anadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi wanaolinda eneo la Mwekezaji Kampuni ya El-Hillal Minerals Ltd.
Marehemu ametajwa kwa jina la Cosmas Hamis Kusililwa umri wa miaka 25 ambaye ni mchimbaji mdogo inadaiwa amepigwa risasi tarehe 10/3/2022 akiwa nje ya eneo la mwekezaji huyo ambako wachimbaji wengi wadogo hujitafutia riziki kwa kuchimba Madini ya Almasi.
Tukio hilo limelaaniwa vikali na viongozi mbalimbali kikiwemo Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan asitishe uwekezaji wa mwekezaji huyo ambaye ameshindwa kuliendelea eneo alilopewa kwa zaidi ya miaka 15 hivi sasa.
Kwa upande wao, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, William Jijimya na Katibu wa CCM Wilayani humo, Peter Mashenji wamesema kitendo kilichofanyika ni cha kinyama na kwamba wakazi wa Kishapu hawahitaji mwekezaji anayewafanyia vitendo vya ukatili wananchi ambapo pia wamemuomba Mhe Waziri wa Madini kuchukua hatua haraka.
JESHI LA POLISI LAFANYA UCHUNGUZI
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP George Kyando alisema: “Hilo ni tukio ni la muda nikilizungumza leo itaonekana kama ni jipya.
Alipoulizwa likuwaje akasema: "Uchunguzi unaendelea, ukikamilika hatua zitachukuliwa.”
Kuhusu hatua zilizochukuliwa kwa mtuhumiwa na kama bado anaendelea na majukumu yake kama kawaida alisema: “Hatujamkamata, anaendelea na majukumu yake kama kawaida kwa kuwa uchunguzi haujakamilika, wala siwezi kumtaja jina kwa kuwa tutaharibu uchunguzi.
“Nimeshazungumza na ninarudia wananchi wawe watulivu na kama kunakuwa na tatizo lolote wasichukue hatua mkononi, maana askari anaweza kufanya hivyo katika njia ya kujihami.
“Wasivamie askari kwa kuwa kama kuna malalamiko yao kwa wawekezaji au ardhi basi wafuate taratibu za kisheria, kuna mahakama na vyombo vingine vya kufikisha kile wanachokilalamikia na siyo kuchukua hatua mkononi.”

=====================================================