Shinikizo la Mh Ali Juma Shamuhuna kutakiwa ajiuzulu na Memba BLW. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shinikizo la Mh Ali Juma Shamuhuna kutakiwa ajiuzulu na Memba BLW.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jan 25, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Waziri wa Maji, Makaazi, Nishati na Ardhi, Ali Juma Shamhuna yupo katika shindikizo kubwa la wajumbe wa baraza la wawakilishi wakimtaka aachie ngazi kutokana na kuchukua uamuzi wake binafsi juu ya suala la ombi la ongezo la bahari kuu kuwasilishwa huko Umoja wa Mataifa (UN) Jana katika baraza la wawakilishi la Visiwani Zanzibar kulikuweko majadiliano makali kuhusu hoja iliowasilishwa na mwakilishi wa eneo la Mji Mkonge wa Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu, Hii imetokana na ombi la serikali ya Muungano wa Tanzania kwa Umoja wa Mataifa kuomba nyongeza ya mpaka katika Bahari ya Hindi ni kuipokonya Zanzibar haki yake. Yeye alitaka kuwepo mazungumzo ya kuamua nani anamiliki eneo hilo kati ya Tanzania na Zanzibar. Othman Miraji alimpigia simu Salim Said Salim, mwandishi wa habari mkongwe Visiwani humo, kutaka kujuwa nini kilichozunguka katika hoja hiyo ya Mwakilishi Jussa hata Wazanzibari kuwa na hamu na mjadala huo.
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Natoka mikoa ya kaskazini ila sijaelewa maana ya maneno yafuatayo
  1. Shindikizo
  2.Memba
  3. Mji Mkonge
   
 3. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,723
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  zanzibar sio nchi. Haitambuliki kimataifa.UN hawaitambui zanzibar, so wanapoteza muda tu.
   
 4. n

  nakuja Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  huku bara imeshindikana kwa wakina ngeleja,kigoma malima,maige na wengineo wengi labda huko zenji mtaweza tungoje tuone.
   
 5. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Mkimfukuza tu huko (SMS) anakuja huku (JMT) tunampatia cheo cha Waziri wa mambo ya ndani
  anakuwa juu kuliko Shein ambaye huku JMT ni Waziri asiye na wizara maalamu. Au Shein naye
  mtafurusha maana alikuwepo kwenye kikao cha baraza la mawaziri wa JMT kilichoamua kuhusu pendekezo
  hilo. Just thinking aloud
   
 6. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Shamuhuna hakujiwakilisha, bali anawakilisha serikali ya mapinduzi ya Zanzibar. Kama wajumbe wa BLW wana ubavu waishinikize serikali yote ijiuzulu siyo kumkomalia mtu mmoja.
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na swala la kupeleka maombi UN ili Tanzania ioengezewe eneo la bahari limeridhiwa na baraza la mawaziri wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambalo Rais wa Zanzibar ni mjumbe. Hizi kelele anazoleta Jussa sijui ni za nini? Kama vipi Jussa apeleke maombi hayo kama Zanzibar UN na awaeleze nchi ya Zanzibar ni ipi?

  Pia napata wasiwasi, hivi hizi kelele za Jussa ni kwamba anaipenda na kuitetea Zanzibar au kuna jingine limejificha? Anamwakilisha nani? Week iliyopita Jussa amenukuliwa na vyombo vya habari akiwaambia wananchi huko Pemba kuwa wananchi wawe tayari kufa kupigania haki ya Zanzibar! Sijui ni busara gani kwa mtu kama yeye Jussa kuanza kuwaandaa wananchi kwa fujo huku akijua fika kuwa issue nzima inaendana na katiba ya Tanzania? Bunge lililopita Jussa kala posho kama mbunge kwenye bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania hivi alijiuliza kama hizo za posho zimetoka Zanzibar au zimetoka Tanganyika?
   
 8. m

  mpingiti Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 15
  Zanzibar si nchi lakini tukumbuke kuwa kiti cha hiyo TANZANIA huko UN, basi ni cha ZANZIBAR. Tanganyika wala Tanzania hawana kiti UN. Tusijifanye vipofu au mabubu, upepo ulianza mashariki, Urusi ikasambaratika. Scotland, imeshaanza na Zanzibar iko katika vugu vugu kubwa lenye kivuli cha kero za Muungano. Dau likizama itabidi Tanganyika mukaombe usajili huko UN kwani Zanzibar atachukuwa kiti chake. Wake up Tanganyika.
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huyu nina wasi wasi anatapatapa kwa niaba ya Seif mpenda madaraka si mawazo yake lakini mwache atajionea mwenyewe CCM A itakavyo deal naye .
   
 10. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Sio muumini wa magamba original ila najua/naamini kuwa magamba wana uwezo mzito sana wa kumnyamazisha/kumshughulikia huyu m.puuzu Jussa .Kama Maalimu Seif katulizwa yeye Jussa ni nani!

  Zanzibar kuna matatizo chungu nzima ya mambo ya kijamii hawayaoni wala kuyapigia kelele wao wanaleta chokochoko za muungano ili wapewe madaraka.
   
 11. Fatal5

  Fatal5 Senior Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  UNITED NATION WANAITAMBUA ZANZIBAR NI NCHI HATA KABLA YA JINA LA TANZANIA HALIJAUNDWA
  " WAKE UP TANGANYIKANS THIS IS THE ONLY TIME TO FIGHT TO GET BACK OUR TANGANYIKA"

  [​IMG]
  Zanzibar ikiwasilishwa katika umoja wa mataifa 1963

  KAMA WEWE NI MTANGANYIKA HALISI BASI IJUE HISTORIA YA NCHI YAKO KULIKO KUBERULIWA BERULIWA
  TUU NA MAJACUC:focus:


  [​IMG]THEY ALWAYS PROUD TO BE ZANZIBARIS EVERY WHERE THE GO AROUND THE WORLD[​IMG]
   
 12. K

  Kivia JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wachangiaji wengi hapa jf upeo ni mdogo wa kuchambua mambo. Ndo maana michango yao utaona inafanana wote kama wamekariri. Unashindwa kuelewa hata viwango vyao vya elimu sijui std 7. Hakika ni matatizo. Hawasomi vitabu mbalimbali vya historia za watu makini wakajua ukweli wanaishia vitabu vya historia vilivyoandikwa na CCM halafu mtu huyo anachangia mambo mazito. Hakika ni msiba mzito kwa vijana hawa.
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Hoja si kama Zanzibar haikuwahi kuwa na seat UN. Inajulikana kabisa kwamba walikuwa na seat lakini seat hiyo ilikoma baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar hivyo seat ya sasa ni Tanzania. Sijui kwa nini kuna watu wanang'ang'ania hoja kwamba watu wa Tanganyika hawajui historia ya Zanzibar. Je, sasa hivi Zanzibar ina seat UN? Zanzibar ina wizara ya mambo za nje? au Tanganyika ina wizara ya mambo za nje?

  Zanzibar wamekaa wakabaili katiba yao jambo ambalo ni jema, ningeshauri sasa wakae wajiondoe kwenye muungano. Haya matishio ya mara sisi ni nchi kamili, mara hatutaki mipaka yetu iingiliwe yamechosha. Either you in or out.
   
 14. m

  mANg'HOnDi Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  changia na wewe ili usomeke sio kulaumu ma wazo ya wenzako.
   
Loading...