Shinikizo la Marekani dhidi ya Maafisa wa ICC: Sura yake katika siasa za Dunia na mwenendo wa Sheria za Kimataifa

Dec 23, 2016
31
69
Leo nimevutiwa kufanya uchambuzi wa kitendo cha Marekani kuiita mahakama ya jinai ya kimataifa (ICC) kua ni ya bandia na kutishia kuzuia Mali za maafisa wa mahakama hiyo. Marekani pia imetishia kuwazuia maafisa wa ICC kuingia nchini humo na ikiahidi kuongeza vikwazo.

Hii ni kufuatia azimio la ICC kufanya uchunguzi juu ya vitendo vya wanajeshi wa marekani katika mashariki ya kati nchini Afghanistan wakati wa vita nchini humo. Marekani inatuhumiwa kujihusisha na uhalifu wa kivita nchini Afghanistan.

Kupitia utawala wa Rais Donald Trump, taifa hilo juzi limeidhinisha vikwazo vyakiusafiri na kiuchumi dhidi ya viongozi na wafanyakazi wa ICC endapo mahakama hiyo itaendelea na azimio lake lakufanya upelelezi dhidi ya wanajeshi wa nchi hiyo.

Taifa hili limeongeza pia vitisho endapo ICC itafungulia mashtaka mshirika wake Israeli kuhusiana na uhalifu wa kivita katika mamlaka ya Palestina.

Swali lakujiuliza ni zipi athari za matendo haya katika muktadha wa Sheria za kimataifa pamoja na siasa za dunia kwa ujumla?
Hadi sasa hakuna tamko lolote lililotolewa na kiongozi, shirika au jumuiya yoyote ya kimataifa. Jumuiya ya umoja wa ulaya na umoja wa Afrika na nyinginezo, zote zimekaa kimya kukemea vitendo vya marekani.

Kumekua na kusita kwa viongozi, mashirika na jumuiya za kimataifa kukemea vitendo vya marekani ambayo vinaashiria ukiukwaji wa Sheria za kimataifa. Hii inaweza kua ni kutokana na ushawishi wa taifa hilo kisiasa kiuchumi nadunishi duniani.

Muktadha wa Sheria.

Mahakama ya ICC imeanzishwa mwaka 2002 kushughulikia kesi dhidi ya uhalifu wa kibinadamu. Mbali na kwamba kuanzishwa kwake kulikubalika na mataifa mengi duniani , mataifa makubwa yamekua yakisita kua wanachama na yamekua yakipuuza jitihada za mahakama hii.

Hadi sasa nchi kama Marekani, China, Urusi, Israel na Syria sio wanachama wa ICC.
Swala nyeti ni kua, taifa la marekani limekua likipuuza uwepo wa ICC pamoja na kudidimiza jitihada za mahakama hiyo. Mfano mzuri ni kupitisha Sheria ya uvamizi wa kuwakomboa maafisa watakaokua wanashikiliwa na mahakama ya ICC.

Hii ina maana kua endapo ICC itawashikilia maafisa wa marekani kwa tuhuma zozote za uhalifu wa kivita, raisi wa taifa hilo anaweza kuidhinisha operesheni ya kijeshi kuvamia mahakama na kuwakomboa maafisa wake.

Endapo ICC itatetereka kimsimamo, kwa kuyumbishwa na vitendo vya marekani, na endapo mataifa mengine na jumuiya zakimataifa hazitakemea vitendo vya marekani madhara yake yatakua makubwa kwa Sheria za kimataifa.

Miongoni mwa madhara yanayoweza kujitokeza ni kama kupungua kwa nguvu ya uhalali wa Sheria za kimataifa, kitendo ambacho kitapelekea mataifa mengine kuongeza mapuuzo dhidi ya Sheria na maazimio ya kimataifa.

Muktadha wa mwenendo na siasa za dunia.

Ushawishi wa marekani kiuchumi na kijeshi unatumika kikamilifu kudhoofisha utendaji wa mashirika na jumuiya za kimataifa.
Taifa hili limekua likishinikiza taasisi taasisi za kimataifa zinazotekeleza majukumu yake, ambayo kwa namna moja au nyingine yanagusa maslahi ya Marekani.

Wiki kadhaa zilizopita tulishuhudia marekani kusitisha mchango wake na kutoka kujiondoa katika uanachama wa shirika la afya duniani (WHO). Hii ni kufuatia tuhuma zilizokosa kichwa wala miguu, kua shirika hilo lilikua linaitetea China kuhusiana na janga la Corona.
Halkadhalika, miaka ya hivi karibuni taifa la Marekani limekua likitumia mabavu katika maswala mbalimbali. Hii inaweza kua ni kutokana na washindani wake kama China kuonyesha kuja juu kwa kasi hali inayotishia Utawala wa Marekani katika dunia kama taifa lenye nguvu.

Ni muhimu kutambua kua Sheria hazitungwi kuwaongoza wasio na nguvu pekee. Vitendo vya marekani vinashusha ushawishi wake katika mataifa mengine kama nchi ya mfano kwenye ufataji wa demokrasia, Utawala bora na misingi ya Sheria.

Huenda dunia ikaelekea katika mgogoro mkubwa siku za usoni kutoka nana vitendo vya marekani.

MAONO YA MWANDISHI
Huku kutapatapa kwa marekani kuna ashiria anguko la taifa hilo kwenye Utawala wake wa dunia katika miongo michache ijayo. Mshindani wake mkubwa, China, anazidi kuchukua nafasi na ushawishi wa dunia kiuchumi na kijeshi.

mfaumehassan@gmail.com
The Eye that Never Sleeps
 
Marekani ni kama panya anaesubiriwa aingie kwenye mtego wamrarue!! Sasa hapo kwenye kurarua kutakuja kuleta mtafaruku mkubwa kama hakuna kiumbe chenye nguvu hapa katikati!..

Namaanisha kuwa dunia inaenda kuadupt kitu cha tofauti huko mbeleni na matokeo yake yanaweza kuja kuwa dunia moja!!
Hicho ndicho ninachokiona.
 
Hapo bado hatujachunguza Yemen,Libya,Iraq,Pakstan unaweza utakayo yakuta ni makubwa kuliko ya Afighanstan.

Wenyewe mauaji ya kivita wana ya remba na kuyapaka rangi baadae wanayaita "colateral demage",ila wakifanya nchi nyingine na vikwazo wana wawekea ,sometimes inatakiwa dunia iwe fair haijalishi mkubwa au mdogo wote wanatakiwa wawe sawa mbele ya sheria.Ila ndio hivyo mkubwa hakosei hapo bado UK na France nk.
 
...matokeo yake yanaweza kuja kuwa dunia moja!!
Nadhani unataka kusema New World Order huu mpango upo na kinachofanyika ni kuandaa mazingira kwa utaratibu na ufanisi mkubwa sana ambao dunia (watu) yenyewe wataupokea kwa mikono miwili.
 
Nadhani unataka kusema New World Order huu mpango upo na kinachofanyika ni kuandaa mazingira kwa utaratibu na ufanisi mkubwa sana ambao dunia (watu) yenyewe wataupokea kwa mikono miwili.
Hilo lako mkuu..😜
 
Yaani kuna mijitu huwa Imekaa Mahali inashabikia USA nakutolea mfano Kanakwamba ni nchi ya mfano ikiwa hao mabepari ndio waonezi zaidi duniani.
Hawana rafikri wala adui hao wanamaslahi tu, ukiona mtu anakubalika sana na hao jamaa maana yake ni moja tu analiwa sana na hao Jamaa au wanamtumia sana kwenye mambo yao.
 
Ikija kwa wengine utasikia USA wanasisitiza wakamatwe na ICC kwa uhalifu na manenombofu mbofu lakini imefika zamu yao wanaaruka hawataki kusikia wanaitishia
 
Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.
Ni dalili za mwanzoni kabisa USA kuanguka.
Ni fursa adimu Kwa nchi za afrika na bara letu kunyanyuka na kutoka hapa tulipo, hatuwezi kunyanyuka kama USA bado ni super power.
Itakuwa ni fursa adimu pia Kwa nchi za mashariki ya kati kunyanyuka na kuwakimbiza wavamizi katika eneo hilo.
 
hakika.....
 
Ikija kwa wengine utasikia USA wanasisitiza wakamatwe na ICC kwa uhalifu na manenombofu mbofu lakini imefika zamu yao wanaaruka hawataki kusikia wanaitishia
Kwanza kitendo cha ICC kutaka kuichunguza USA inaonyesha kuwa marekani imeshuka sana kiushawishi katika siasa za kimataifa pia imekuwa sio tishio tena kwa baadhi ya nchi kubwa zenye ushawishi duniani.. Ijapokuwa nchi hizo hazijatoa comment zozote katika hilo sakata ..lakini nachelea kuamini kuwa hizi zitakuwa ni choko choko zao.. Za kumtaka mkubwa atambue kuwa mwisho wake wa kuanguka upo karibuni
 
Ndio maana natamani DT ashinde kwakishindo maana najua kama ataendelea kuzidi kuivuruga states

Alimpigia sana mkwara WHO ila jamaa wakakaza hatimae yeye akajitoa WHO yule MKUU alotaka ajiuzulu kakomaa hii inaonesha kwakiasi gani jamaa ushawishi unazidi kudidimia kwakasi yaajabu mnooooo.....
 
Hahaha jamaa ashinde tu ..hata Mimi na wish iwe hivyo
 
Back
Top Bottom