Shinikizo la Damu Mwilini – Ukweli wa Mambo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shinikizo la Damu Mwilini – Ukweli wa Mambo

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Shinikizo la juu la damu mwilini ni nini?  Namna ambavyo damu yako hupiga kwenye ukuta wa mishipa ya mwili wako huitwa shinikizo. Kwa kawaida shinikizo la damu la mtu hupanda na kushuka siku nzima. Kwa wengine hubakia juu kila wakati. Hawa ndio watu walio na shinikizo la juu la damu mwilini au Hypertension.

  Hali hii huweza kuathiri na kuharibu moyo wako, macho na figo. Huzidisha nafasi yako ya kushikwa na ugonjwa wa pigo (Stroke) au hata kushikwa na ugonjwa wa moyo.

  Hivyo basi dalili zake ni nini?
  Ugonjwa huu hujulikana kama “muuaji mnyamavu” kwa maana, mtu hukaa nao kwa miaka bila kujua. Njia ya pekee ya kujua iwapo una ugonjwa huu, ni kwenda kupimwa shinikizo lako la damu.

  Nitazuiaje ugonjwa huu au hata kuutibu?

  Jambo la kushangaza ni kuwa, hatua za kuchukua katika kuzuia shinikizo la juu la damu mwilini ni sawa na za kuutibu ugonjwa huu. Jambo muhimu sana ni kuhakikisha kuwa, unapimwa shinikizo lako angalau mara moja kwa mwaka na mhudumu wa kiafya aliyehitimu. Ni muhimu kwa sababu, kipigo cha damu cha mtu kwa kawaida huendelea kupanda maishani mwake. Njia nyingine ni pamoja na;

  • Kufanya mazoezi ya mwili ya mara kwa mara
  • Uepukane kabisa na kuvuta sigara na kulewa
  • Ule lishe bora lisilo na chumvi
  • Punguza uzani iwapo wewe ni mkubwa
   
 2. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wengine wameshaathirika na bp,wape ushauri
   
Loading...