SHINIKIZO LA DAMU/BP Husababishwa na Upungufu wa maji mwilini (dehydration)

Fadhili Paulo

JF-Expert Member
Sep 1, 2011
3,211
988
MAJI HUKINGA NA KUPONYA SHINIKIZO LA DAMU (BP):

Shinikizo la damu (hasa la juu) ni kiashiria cha mwili kupungukiwa maji kwa kiwango kikubwa, ni wakati ambapo mwili unajaribu kujizoesha na upungufu wa jumla wa maji wakati kunapokuwa hakuna maji ya kutosha kuijaza mishipa ya damu yenye kazi ya kusambaza maji kwenye seli mhimu.

Mishipa ya damu imebuniwa maalumu kuendana na mtiririko uliosawa wa ujazo wake wa damu na mahitaji mbalimbali ya tishu kwa kufunga na kufungua mishipa mbalimbali ya damu.

Figo hushtuka upesi kulingana na mtiririko wa damu. Hili linaposhindikana, Figo huitoa homoni iitwayo 'renini' ambayo yenyewe huzarisha kitu kiitwacho 'angiotensini' ambayo huwa na matokeo mawili; kwanza huzibana ateri na kupandisha shinikizo la damu, pili huisababisha tezi ya 'adreno' kutoa homoni iitwayo 'aldosteroni' ambayo huzifanya figo kuishikilia chumvi na hivyo kusababisha kupanda kwa shinikizo la damu.

Asilimia 94 ya damu ni maji. Kwa ujumla kila seli ndani ya miili yetu ina bahari ya maji baridi ndani yake na bahari ya maji chumvi nje yake. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa maji ya bahari hizo mbili.

Chumvi inayashikilia na kuyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli (osmotic retention) na potasiamu inayashikilia maji ndani ya seli.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji (haunywi yakutosha) mwili utaongeza ujazo wa maji chumvi kwenye bahari ya nje ya seli.

Kupitia mfumo maalumu, homoni iitwayo 'vasopressini' hutolewa ambayo inaweza kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli na kuyachoma maji hayo baridi ndani katikati ya bahari ya ndani ya seli kama yanavyohitajika ili kuutunza uwiano sawa wa maji ndani na nje ya seli.

Lakini ili mbinu hii ifanikiwe, vasopressini husababisha kapilari na mishipa ya damu kujikaza au kupunguza vipenyo vyake na kukupatia wewe shinikizo la damu (BP) ambalo ni mhimu ili kuyachuja na kuyachoma maji baridi ndani ya seli toka katika bahari ya maji chumvi iliyopo nje ya seli.

Kama mishipa ya damu haitapunguza vipenyo vyake, baadhi ya gesi itaachana na damu ili kuziba nafasi zilizowazi kutokana na kupungua kwa umajimaji (fluids) mwilini na hatimaye kukusababishia msongamano wa Gesi (Gas locks).

Sifa hii ya vipenyo vya mishipa ya damu kujirekebisha kwa ajili ya mzunguko wa damu, ndiyo mtindo unaotumika zaidi katika kanuni za kihaidroliki wakati ambapo mzunguko wa damu mwilini umejirekebisha kuendana na kiasi cha umajimaji kinachopatikana.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji kwa mfano kutokana na kutokunywa maji ya kutosha; asilimia 66 ya kuishiwa maji inajionesha kwa kupungua kwa ujazo wa seli, asilimia 26 inapotea toka ujazo wa umajimaji uliopo sehemu ya nje ya seli na asilimia 8 tu inapotea toka katika ujazo wa damu.

Shinikizo la juu la damu ni kiashirio cha mwili kupungukiwa maji kwa asilimia 8 tu, lakini madhara yanajitokeza sababu ya asilimia 66 ya kupunguwa kwa ujazo wa seli.

Maji na chumvi vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida.

Hii ndiyo sababu shinikizo la damu linapaswa kutibiwa kwa kuongeza unywaji wa maji pekee. Dr.Batmanghelidj anasema; Maji peke yake, ni dawa bora ya kukojosha, pekee ya asili tuwezayo kuiendea.

Kama watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu wangeongeza kiasi cha uchukuaji maji, hawatazihitaji dawa za kukojosha, watazarisha mkojo wa kutosha na hivyo kuiondoa chumvi iliyokuwa imezidi!. Watatakiwa pia kuacha kula vyakula visivyo na chumvi na hivyo kuepukana na mikakamao ya mishipa (cramps) kwenye miguu yao.

Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, kutokulielewa shinikizo la damu kama moja ya ishara za mwili kupungukiwa maji na kulitibu kwa dawa za kukojosha ambazo zinaukausha mwili zaidi, baada ya muda zitasababisha kuzibika kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye ubongo, zitasababisha shambulio la moyo (heart attack), mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia, ugonjwa wa kibofu cha mkojo, na mwishowe kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Daktari mwingine, dr.David Brownstein katika kitabu chake; "Salt your way to live", anasema kwamba alifundishwa katika vyuo vya kiganga kuwa chumvi husababisha shinikizo la damu na kuwa kila mmoja lazima ale vyakula vyenye chumvi kidogo.

Wakati akiwatibu wagonjwa wake, anasema; alianza kuona kuwa wale wanaotumia vyakula vyenye chumvi kidogo wanapata matokeo ya chini kutoka katika vyakula hivyo na wengi wao walikuwa wana uhaba wa madini pia.

Katika utafiti wake ili kuwasaidia wagonjwa wake, ndipo akaja na jibu la chumvi ya bahari ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ambayo huwa na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake, alianza kuona kitu kigeni kinaanza kutokea. Wagonjwa wake hao wakaanza kuona mashinikizo yao ya damu yanaanza kushuka katika kiwango ambacho wanaweza kuachana kabisa na matumizi ya dawa.

Dr.Batmanghelidj anasema, ikiwa watu watatembea (mazoezi), watakunywa maji halisi zaidi na kuongeza chumvi (siyo sodiamu) kidogo ya ziada kwenye milo yao, mashinikizo yao ya damu yatarudi katika hali yake ya kawaida.

Swali la kujiuliza; Ni zaidi ya miongo mitatu sasa tangu tulipoambiwa kula vyakula vyenye chumvi kidogo ili kuepukana na shinikizo la damu, kwanini sasa Idadi ya watu wanaopatwa na ugonjwa huu inazidi kuongezeka?.

Narudia tena, mwili unapoanza kuishikilia chumvi, hufanya hivyo ili kuhifadhi maji, toka katika bahari chumvi hiyo ya nje ya seli, maji huchujwa na kutumika wakati wa mahitaji ya dharura.

Maji na chumvi kwa pamoja vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida. Kuikimbia chumvi kunasababisha shinikizo la damu (BP) kuwa sehemu ya maisha yetu, tutapata nafuu, lakini baada ya muda hali hurudi ileile na pengine kuwa watumwa wa kuchagua kula hiki au kile.

Kwa hali ilivyo sasa, shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti. Siku hizi wanene kwa wembamba, watoto kwa wakubwa wanaugua BP. Usisahahu kusoma ukurasa wa ‘maajabu ya chumvi'.

Makala zingine: CHumvi:
http://maajabuyamaji.net/2012/12/maajabu-ya-chumvi/
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom