Shime Watanzania tuupiganie Uhuru wetu unaoporwa. Tutajuta!

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,569
50,393
Mwalimu Nyerere na wenzake walipambana na mkoloni siyo kwasababu walitaka nchi yetu ipate ama ijenge vitu la hasha.

Mwalimu Nyerere na wenzake walipambana na mkoloni siyo kwasabb walitaka kuunda serikali itakayo watisha watu na kuwafanya wawe na "heshima" kwa watawala.

Mwalimu Nyerere na wenzake walipambana na mkoloni siyo kwasabb walitaka kuendeleza/kujenga maeneo walikotoka na kuyafanya ya kimkakati.

Akina Mwalimu Nyerere na wenzake hawakupambana na mkoloni ili wageuke chui wa kuwakamata kila atakayejaribu kutoa mawazo kinzani.

Nini waliktaka akina Mwalimu Nyerere na wenzake?

Walipambana na mkoloni ili wananchi wa nchi hii wapate UHURU wa kufanya , kusema na kutenda bila ya woga ili mradi wasitoke nje ya mipaka ya kikatiba.

Lakini sasa Uhuru hakuna tena. Katiba haiheshimiwi, watu wanatishwa, tunalingishiwa ujenzi wa miundombinu eti ndiyo kitu mihimu kuliko uhuru wetu. Ebo!

Rais bila soni anatumia mabilioni ya shilingi kujenga miundombinu mikubwa kijijini kwao. Tumenyamaza! Hakuna anayethubutu kukemea.

Amevuruga uchaguzi serikali za mitaa watanzania kimyaa! Amevuruga uchaguzi mkuu tunamwagalia tu'. Na sasa kuna kila dalili na mikakati ya wazi imewekwa ili kumuongezea muda afie madarakani. Hatusemi.

Hakika tutavuna mabua, maana tunacheka na nyani.

Namkumbuka Tundu Lisu alliyepata kuona mbali ingali bado na mapema (2016) alisema "Tuna rais wa ajabu haijapata kutokea"
 
Ungeishi enzi za Nyerere usingeandika utopolo huu yote ni copy na paste. Yaliyopo yalikuwepo.

Ye ndo mwasisi wa yote haya
 
Back
Top Bottom