Shilole athibitisha kupigwa na Uchebe, asema kuanzia leo yeye siyo mke wa Uchebe

uchebe ni muislamu na quran inaruhusu wanawake kupigwa.nikushangae unayepinga maandiko ya dini isiyokuhusu.wewe ni nani upinge maandiko ya waislamu?? waislamu wakusikilize wewe au waisikilize quran?
Unachojaribu kukifanya wala hakitokusaidia. Wala hakijawahi kuwasaidia watu mfano wako waliopita. Allah akuongoze.
 
Nyie mnafikiri kuzidi kipato kunawapa justification ya kujiamulia kumuheshimu mume au kutokumuheshimu? Hamna tofauti na yule anaekomaliaga eti mwanaume nae adeki na kuosha vyombo kama zamu kwa maana yeye mke anachangia pato katika familia.

Ukiwa huna adabu kwa mwanamume rijali lazma atakubunda tu!!! Jiheshimu umpe peace of mind mumeo, hatakaa akuwazie mabaya. Daima mtadumu katika amani.

Tatizo lenu wanawake wa kibongo mkishika hela na mali zaidi ya waume mnakuwa na roho ya unyanyasaji na dharau. Yani baba wa familia asihoji umelala wapi siku 2 mfululizo bila taarifa.
Huyo kama Zoë , mwenye hayo mawazo ya ki Beijing
 
Tokea awali nilipatwa na hisia hii inawezekana kuwa ni stunt ya kishamba ya kutafuta publicity na kwa asilimia kubwa alifanikiwa kwani "alibreak the internet" siku alipoweka wazi kwamba amekuwa anakuwa physically abused na mumewe,watanzania wasishangae wakimuona na mavazi ya kijani na njano akiwa anachukua fomu ya kugombea nafasi fulani ya kisiasa katika siku hizi za usoni.
 
Hii dhana ya kwamba mke akiwa na kipato kikubwa kuliko mume tafsiri yake kuwa mwanaume analelewa imashangaza kidogo

Maana kimsingi wanawake wengi wa Afrika ni wabinafsi

Mwanamke anaweza kuwa na kipato kikubwa lakini Mume hajawahi gusa hela ya mkewe ila mke anaenjoy hela ya mumewe

Lakini bado itahesabiwa mwanamke anamlea mwanaume.

Nafikri dhana ya kulelewa iwe kwa mwanaume ambaye hajishughulishi.

Mwanamke kutangulia kuwa na kipato kikubwa ni mfumo tu wa maisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom