shillingi yazidi kuporomoka

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,359
Hatari kubwa sana ya kiuchumi inatusogelea, jioni ya leo baadhi ya maduka ya kubadili fedha za kigeni yalikuwa yananunua dolari kwa Tshs 1,700.

Sijui benki kuu ya Tanzania inachukua hatua gani madhubuti kujaribu kuzuia halii hii?
 
Mnashangaa nini ndiyo makubwa ya JK hayo. Well hivi ile argument kwamba shilingi ikiporomoka inachangia kuongeza exports, kwa nini wasiiporomoe iwe $1 kwa laki moja?
 
Nchi iko gizani karibu mwaka sasa, hakuna tunachouza zaidi ya kugawa kile tulichonacho! Natamani Michael Sata aje Tanzania atusaidie. Pamoja la hayo, sisi tunaowaangalia viongozi wetu wakitusababishia matatizo ni sawa nao tu. Kwani tumebaki kupiga kelele za kichura bila kufanya kile kinachotakiwa.
 
Watatue matatizo ya umeme na kushinikiza makampuni ya madini yawepo nchini pamoja na kupunguza dollarisation nchini ndio Shillingi itapungua kuporomoka sasa hivi wanacheza makida makida tu!!!.
 
Nchi iko gizani karibu mwaka sasa, hakuna tunachouza zaidi ya kugawa kile tulichonacho! Natamani Michael Sata aje Tanzania atusaidie. Pamoja la hayo, sisi tunaowaangalia viongozi wetu wakitusababishia matatizo ni sawa nao tu. Kwani tumebaki kupiga kelele za kichura bila kufanya kile kinachotakiwa.

Dr wa ukweli Slaa ameshindwa mpaka mtafute mamluki toka nje?
Waleteni tu, tutapima sera zao.
 
Hifadhi katika dola! Mie ndo nimefanya hivyo maana kila siku hasara!!

Wakati hata mahindi yetu tunakatazwa kuuza nje na serikali ilyokataza haitaki tununue na matokeo yake yananyeshewa na mvua na kuoza. Sio wote tunaoweza kuhifadhi kwenye dola. Wengi wetu uchumi ni hand to near mouth income, imezidi hata ile ya hand to mouth.
 
Mkuu sisi tulio ughaibuni tunasali iwe hata 3000 kwa dola, ili vimshiko vyetu ukivipeleka Tz unatafuta gunia la kubebea.

Halafu zikifika Tanzania zinapukutika kama gesi kwani thamani shillingi inakuwa haina maana. Leo hii milioni 1 ni sawa na laki moja tu kwani wiki moja imeshaisha. Usiwe shallow thinker mkuu Shilingi ikiporomoka maisha yanazidi kuwa magumu. Unaweza kurudi na magunia ya Shillingi lakini yakifika Tanzania usikae nayo hata wiki yameisha. Kuwa Great Thinker ndugu.
 
Hebu tumfikirie mtanzania wa kawaida mfanyakazi anayepokea 100,000, hivi anamudu vipi maisha kama haya? Laki ambayo mtanania wa kawaida anapata kwa mwezi inapukutika, sio inakwisha, kama mchezo. Mfikirie Mkulima anayetegemea kuuza ufuta wake hata laki hakamati mtu huyo inakuwaje na maisha haya.

Benki Kuu wanasema nini juu ya hilo?
 
Hatari kubwa sana ya kiuchumi inatusogelea, jioni ya leo baadhi ya maduka ya kubadili fedha za kigeni yalikuwa yananunua dolari kwa Tshs 1,700.

Sijui benki kuu ya Tanzania inachukua hatua gani madhubuti kujaribu kuzuia halii hii?

Huo ni mwanzo tu.., CCMU oyeee?!! Kikwetei oyeeeeeeeeeeeee!!!
 
Hebu tumfikirie mtanzania wa kawaida mfanyakazi anayepokea 100,000, hivi anamudu vipi maisha kama haya? Laki ambayo mtanania wa kawaida anapata kwa mwezi inapukutika, sio inakwisha, kama mchezo. Mfikirie Mkulima anayetegemea kuuza ufuta wake hata laki hakamati mtu huyo inakuwaje na maisha haya.

Benki Kuu wanasema nini juu ya hilo?

Mkuu,

Majuzi katika mkutano mmoja Ben Benarnke alisema there is little that the Central bank can do to save the country economy. Monetary policy bila ya kuwapo kwa sound fiscal policy ni vigumu sana kuokoa uchumi. Benki kuu itajitahidi kuzuia kuporomoka kwa shillingi kwa njia mbali mbali kama kupunguza pesa za kutoka kwenye mzunguko wa fedha, kuingiza fedha zaidi za kigeni nyingi katika mzunguko nk. But Shida ya monetary policy ni kwamba ni measures za muda mfupi kuokoa uchumi. Serikali inabidi ijitahidi kuokoa uchumi wa nchi kuanguka kwa kutatua tatizo la umeme, ufisadi, dollarisation nk. Bila ya strong fiscal policy BOT itabakia kama bubu kwani ikiingiza pesa zaidi katika mzunguko zitashusha thamani za fedha za kigeni kwa muda mfupi lakini baada ya miezi miwili thamani ya dollar itazidi mara mbili ya ilivyokuwa mwanzo na kuzidisha ugumu wa maisha.
 
Hatari kubwa sana ya kiuchumi inatusogelea, jioni ya leo baadhi ya maduka ya kubadili fedha za kigeni yalikuwa yananunua dolari kwa Tshs 1,700.

Sijui benki kuu ya Tanzania inachukua hatua gani madhubuti kujaribu kuzuia halii hii?
kuna sehemu hapa Arusha ni 1710
 
BoT governor’s word on shilling, recession fears Thursday, 06 October 2011 22:41 Tanzania has no plan to pump more dollars into the money market to steady its shilling, but will deal with the main economic fundamentals instead.The governor of the Bank of Tanzania, Prof Benno Ndulu, said this yesterday. He said although the local currency has hit a 17-year record low against the greenback as importers’ appetite for dollars continues to rise amid a scarcity of foreign exchange in the money market, the bank would not move to defend the falling shilling.“It won’t be to our benefit if we decide to artificially stabilise our currency…we would rather continue to deal with the main economic fundamentals,” he told The Citizen yesterday in a telephone interview.He was reacting to local experts who called on the country to swiftly move to defend the shilling, which has depreciated to the levels of hurting importers. According to him, the BoT has been selling the greenback on an average of $100 million per month for the past three months, for the purpose of controlling inflation.He said the move to stabilise the shilling would reduce the country’s competitiveness by negatively impacting on exporters as well as prompting tourists to opt to visit nearby countries with weaker shilling.The governor said the shilling has been weakening mainly because of the high inflation differential against the country’s trading partners and the mounting investors’ anxiety that has also distabilised other currencies.The country’s inflation rate climbed to 14.1 per cent in August on higher energy and food costs, the National Bureau of Statistics said last month.Commenting on projections by the experts that the continuing economic crisis in the Eurozone could trigger another economic downturn, double-dip recession, Prof Ndulu said the country was alert.hayo ni mawazo ya governor wetu!!!!!!!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom