Msemakweli Chakubanga
Member
- Dec 13, 2018
- 30
- 140
SHILINGI YA TANZANIA YAIMARIKA KWA 3% DHIDI YA DOLA YA MAREKANI.
Leo 13:15pm,10/03/2019.
Baada ya mwezi February shilingi kuporomoka dhidi ya dola kwa 2.15%,Sasa shilingi imeanza kuimarika kwa 3% katika wiki ya kwanza ya mwezi Machi, ukuaji wa kiuchumi ambao umeongozwa na Watalii na Wafanyabiashara toka Zambia, Malawi, Congo, Comoro,Rwanda na Burundi kuja kununua bidhaa katika Soko la Kariakoo kuingiza dola nyingi katika Serikali na utafiti umebaini kwamba mambo yamebadilika na sasa Taifa linategemea sekta mbalimbali kama Utalii, Biashara, Kilimo na Viwanda na kutoa nafasi nzuri ya upatikanaji kwa wingi wa fedha za kigeni.
Vifuatavyo ni viwango vya kubadilisha fedha za kigeni vinavyotumika tarehe 08 Machi, 2019. Tafadhali zingatia kuwa Viwango vya kuuza ni kwa ajili ya Maduhuli wakati Viwango vya Kununua ni kwa ajili ya Mahuruji.
Dolar ya Marekani inanunuliwa kwa Shilingi 2,277.495 kuuzwa kwa Shilingi 2,300.27
Pound ya Uingereza kununuliwa kwa Shilingi 2,992.4007 na kuuzwa kwa 3,022.5548
Euro ya Ulaya kununuliwa kwa 2,573.7972 na kuuzwa kwa 2,600.6853
Rupia ya India kununuliwa kwa 32.4259 na kuuzwa kwa 32.7347
Kwacha ya Zambia kununuliwa kwa 187.8933 na kuuzwa kwa 190.8938
Kwacha ya Malawi kununuliwa kwa 2.9106 na kuuzwa kwa 3.1089
Shilingi ya Kenya kununuliwa kwa 22.7977 na kuuzwa kwa 22.9797
Shilingi ya Uganda kununuliwa kwa 0.5763 kuuzwa kwa 0.6175
Faranga ya Rwanda kununuliwa kwa 2.5268 na kuuzwa kwa 2.5577
Faranga ya Burundi kununuliwa kwa 2.1806 na kuuzwa kwa 2.197
Dola ya Zimbabwe kununuliwa kwa 0.4262 na kuuzwa 0.4348
Randi ya Afrika kusini 161.
Utafiti pia unaonyesha Mataifa ya kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo ukuaji wao wa kiuchumi ulikuwa umeegemea Mataifa ya Magharibi mwa Afrika yaliyokuwa na Mafuta pamoja na bidhaa sasa ukuaji wa kiuchumi wa Mataifa ya kusini mwa Jangwa la Sahara unaanza kuegemea zaidi Afrika Mashariki na hasa Tanzania kwa kuwa bidhaa na mafuta yaliyokuwa yanapatikana katika Mataifa ya Magharibi mwa Afrika sasa bidhaa, na Mafuta vinapatikana Tanzania.
Taifa letu linakwenda vizuri, uchumi wetu unakua vizuri, mwaka jana umekuwa kwa wastani wa asilimia 7 na mwaka huu tunatarajia utakua kwa wastani wa asilimia 7.1, mfumuko wa bei umeendelea kuwa chini kwa wastani wa asilimia 4.
Baada ya Bureau za Kariakoo kufungwa utashuhudia mamia ya Wageni toka Congo, Zambia, Malawi, Msumbiji,Comoro,Rwanda na Burundi wakiingia katika benki mbalimbali pale Kariakoo kubadili dola nyingi kupata shilingi za Kitanzania kwa ajili ya kununua mizigo katika Soko la Kariakoo na kuipeleka katika nchi wanazotoka.
Bidhaa zinazouzwa nje unaweza kuzipima kutoka katika soko la Kariakoo na utagundua kuwa zimeongezeka.
Na dalili zote zinaonyesha mabadiliko ya kuingia kwenye viwanda kuwa makubwa licha ya kufanyika polepole.
Sehemu ya ukuaji na kuimarika kwa shillingi ya Tanzania inatarajiwa pia kuchangiwa na ongezeko la idadi ya wafanyabiashara wa kigeni watakaokuja kununua bidhaa mwezi huu Machi na April kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka na hapo baadae Sikukuu ya Idd.
Kwa Afrika Mashariki baada ya Uganda na Tanzania, Kenya ni ya kumi katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kukua kwa kasi zaidi mwaka 2026 ambapo ukuaji wake utakuwa asilimia kubwa zaidi.
Mataifa 15 ambayo yanayokadiriwa kuongoza kwa kasi ya ukuaji wa uchumi kufikia 2026
Nambari Taifa Ukuaji wa Uchumi kwa %
1 India 7.89
2 Uganda 7.46
3 Egypt 6.63
4 Tanzania 6.15
5 Indonesia 6.13
6 Kyrgyzstan 6.04
7 Pakistan 5.99
8 Vietnam 5.89
9 Mali 5.89
10 Kenya 5.87
11 Philippines 5.75
12 Madagascar 5.73
13 Senegal 5.7
14 Liberia 5.7
15 Turkey 5.57
Nimalizie kwa kusema ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni mzuri ukilinganisha na nchi nyingine zilizopo Afrika Mashariki, huku Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi za bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa.
Ukiachilia mbali sekta ya biashara na Utalii, bado kuna sekta zenye viwango vikubwa vya ukuaji katika kipindi cha sasa na kijacho zikiwemo shughuli za uchimbaji madini ambazo sheria zake zimerekebishwa na kuwekwa kwa maslahi Mapana ya Taifa,pia kuna shughuli za Usafirishaji na uhifadhi wa mizigo,Mawasiliano na Huduma za kifedha ambazo sasa zitaleta tija kwa Taifa kupitia mabenki mbalimbali yatakayokuwa yanabadili fedha hizo za kigeni.
Mfumuko wa bei umepungua kwa kiasi kikubwa na unatarajiwa kuendelea kubakia katika kiwango cha tarakimu moja katika siku zijazo na kubakia ndani ya lengo la muda wa kati la asilimia 5.0.
Matarajio hayo yatategemea kuendelea kutulia kwa bei ya nishati nchini kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya gesi asilia katika uzalishaji wa umeme,na ujenzi wa vyanzo vingine vya Umeme kama Kinyerezi na pia Ujenzi wa Bwawa kubwa la Rufiji (Stigglers Gorge) na mwendelezo wa Sera thabiti ya fedha na kibajeti, kutobadilika sana kwa bei za mafuta katika soko la dunia pamoja na kuendelea kuwepo kwa utulivu wa thamani ya Shilingi.
Shukrani za dhati kwa Serikali kwa kuimarika huku kwa thamani ya Shilingi kulikotokana na hatua mbalimbali za sera ya fedha zilizochukuliwa na Benki Kuu katika kusimamia hali ya ukwasi kwenye uchumi pamoja na kuimarika kwa urari wa bidhaa na huduma katika Sekta ya nje.Mungu ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Rais wetu, John Magufuli.
Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.