Shilingi ya Tanzania ina tatizo gani kwenye suala la thamani?

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,914
Kwa ukanda wa EAC pesa ya Tanzania ina thamani dhidi ya pesa ya Uganda pekee yake kwa sasa.

Kwenye suala la thamani kuna shisa sana kwa Shilingi ya Tanzania, fikiria hadi Pesa ya Burundi imetupita, Rwanda ndo usiseme, Uganda wako jirani kutupita, Kenya wako juu yetu, Sudani Kusini wako juu.

Zambia ndo balaa tupu kwa sasa kwacha 1 ni sh 142 ya Tanzania, Kwacha ya Malawi still nayo iko far.

Tungekuwa tunazalisha sana tungesema hii ni faida kwetu ila sisi sio wazalishaji hata sisi ni Importer na hapa maana yake unapo import kutoka nchi yenye sarafu strong maana yake biadhaa zinakuwa ghari sana.


Screenshot_20220710_131154_com.android.chrome.jpg
Screenshot_20220711_172918_com.android.chrome.jpg
Screenshot_20220710_131900_com.android.chrome.jpg
 
Hapo zamani shilingi ya Kenya na Tanzania zilikuwa sawa, baada ya Nyerere kutofautiana na IMF ndiyo ikaanza kuporomoka.

Hata hivyo kwacha ya Zambia ilikuwa juu sana kwa sababu ya uzalishaji wa Copper. Kwenye miaka ya themanini kwacha ilikuwa juu kuliko US dollar ila nayo imeporomoka.

Francs huwa zinawekwa thamani na Wafaransa na ndiyo maana hawafurukuti kwa lo lote. Na hii ni kwa nchi zote zilizokuwa tawala za ufaransa na ubelgiji.

Hayo ni maoni yangu tu.
 
Tukizalisha kwa wingi na kuuza nje, mambo yatakaa sawa; ukiwa na wingi wa fedha za kigeni= fedha yako lazima iwe imara
 
Back
Top Bottom