Shilingi ya Tanzania imeshuka kwa 20% kulinganisha na Franca ya Burundi

deepsea

JF-Expert Member
Aug 10, 2013
3,288
939
Haya ameyasema muda mfupi bungeni mh James Mbatia akiwakilisha maoni ya kambi ya upinzani bungeni,na akasema kwenye soka dhidi ya pesa za kigeni imedoka kwa 35%. Serikali hii inatupeleka wapi?hata burundi walioko kwenye mapigano huku wengine kati waliotufikisha hapa wanakimbilia ikulu?
 
nasikiliza bunge hapa serikali ya vibaka wizara ya fedha inasema mradi wa umeme wa kititimo singida unaelekea kufutwa wizara ya viwanda na nishati inasema mradi unaendelea kama kawaida
 
makampuni ya simu na makampuni ya madini yameigomea serikali kujisajili kwenye soko la hisa la Dsm na serikali imekubali sababu kodi yao halisi itajulikana ila mama ntilie na machinga wakigoma wanapigwa-Kafulila
 
Nasubiri ifike 3000 nichenji tudola twangu, maana na huu uchaguzi akili za ccm zitahamia kwenye uchaguzi tu
 
Attachments

  • 1433672390908.jpg
    1433672390908.jpg
    38.5 KB · Views: 150
Mheshimiwa Waziri wa Fedha pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ni AIBU kubwa kwa fedha ya Tanzania kushuka kwa 20%. Fedha ya Kenya imepanda kwa asilimia ndogo sana. Hivi kuna tatizo gani. Kasi ya ujenzi imepungua sana kutokana na vifaa vya ujenzi kupanda maradufu. Juzi nilienda kununua vifaa vya ujenzi kwa idadi niliyonunua miezi miwili iliyopita kwa Tshs.3,000,000. Juzi nimeenda kununua bidhaa kama hizo kwenye duka lile lile nikaambiwa kuwa nilipe Tshs.4,000,000. Chukueni hatua za haraka vinginevyo ukuaji wa uchumi kwenye sekta ya ujenzi utapungua sana.
 
makampuni ya simu na makampuni ya madini yameigomea serikali kujisajili kwenye soko la hisa la Dsm na serikali imekubali sababu kodi yao halisi itajulikana ila mama ntilie na machinga wakigoma wanapigwa-Kafulila

Hao hao wanaosajili ndo wanaoenda kupokea rushwa toka kwa hayo makampuni
 
Mheshimiwa Waziri wa Fedha pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ni AIBU kubwa kwa fedha ya Tanzania kushuka kwa 20%. Fedha ya Kenya imepanda kwa asilimia ndogo sana. Hivi kuna tatizo gani. Kasi ya ujenzi imepungua sana kutokana na vifaa vya ujenzi kupanda maradufu. Juzi nilienda kununua vifaa vya ujenzi kwa idadi niliyonunua miezi miwili iliyopita kwa Tshs.3,000,000. Juzi nimeenda kununua bidhaa kama hizo kwenye duka lile lile nikaambiwa kuwa nilipe Tshs.4,000,000. Chukueni hatua za haraka vinginevyo ukuaji wa uchumi kwenye sekta ya ujenzi utapungua sana.

hiyo hali hata mimi jana nilikutana nayo kusema ukweli ccm wameshindwa ndio maana mwenyekiti wao anaziita madafu
 
Shillingi imeshuka thamani dhidi ya US Dollar kwa asilimia 30.Napata wasiwasi jinsi ilivyoshuka thamani ghafla.Waziri wa fedha ametangaza semina ya wabunge kuwasomesha sababu ya kushuka thamani ya shillingi.Tanga awali alipoteuliwa mama huyu sikuwa na imani na utendaji wake.Uchumi unadorora na sasa tunatupwa nyuma kabisa na nchi zingine!
 
Back
Top Bottom