Shilingi Moja Kwa Sekunde Masaa 24 na Kuichangia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shilingi Moja Kwa Sekunde Masaa 24 na Kuichangia CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanangwa, Oct 13, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Siku zote nilikuwa nikijiuliza, hivi hawa wenye makampuni ya simu wanapata vipi faida kwa mtindo wa shilingi moja kwa sekunde katika kipindi hiki ambapo karibu kila mtu ana simu (mijini) na cha zaidi Mchina anatengeneza simu zenye line mbili? Na je, kwa mwendo wa vocha za 300, 500, na nipige tafu faida itapatikana wapi?

  Baada ya kuzagaa kwa taarifa za ujumbe unaohusu "kuichangia CCM kwa lazima", sasa naweza kujua kwa nini tunadanganywa gharama za kupiga simu zimeshuka. Kuna uwezekano mkubwa kwamba CCM wamewalipa makampuni ya simu pesa ya kutosha kabisa ili makampuni yashushe bei na kwa hiyo, kimya-kimya watumiaji wa mitandao wanakatwa salio bila kujua.


  Inakuwaje CCM wanatapatapa namna hii jamani? Siri zote tunazipata kutoka huko huko kwenu CCM. Fanyeni ghiliba zote. Tutazinyaka. Hata mfanyie kuzimu. Tutazinyaka.

  Kila nafsi itaonja mauti jamani. Tulieni.
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Hivi huu ujumbe wako una uhusiano na huu ujumbe? Kama ni kweli basi naomba MODS muunganishe huu ujumbe ili ulete mtiririko mzuri. Tunaomba watu wajulishwe ili wajitoe na ikiwezekana siku ya Nyerere Day basi Mawakili wayashitaki haya mashirika kwa niaba ya Watanzania woote ili waipate habari yao.

   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Ndiyo mkuu
   
Loading...