Shilingi Milioni Mia Mbili Zimetafunwa Na ' Panya' Mbarali!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Juzi usiku kwenye TBC1 iliripotiwa kuwa shilingi milioni mia mbili hazijulikani zilipo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Kamanda wa Takukuru mkoani Mbeya alionekana kwa uchungu kuzungumzia kashfa hiyo huku akiahidi kufanya uchunguzi na kuja na ripoti ndani ya kipindi kifupi. Kamanda huyo alisikitishwa na upotevu huo wa fedha za wananchi.

Kama shilingi milioni mia mbili zinapotea kwenye Halmashauri basi ina maana kuwa kuna ' panya' wanaotafuna fedha za wananchi kwenye halmashauri husika.

Kuna wenye kutakiwa kutolea ufafanuzi zilikokwenda fedha hizo. Wanajulikana. Na kwa vile imethibitisishwa kuwa kuna ' panya' wametafuna fedha za wananchi, basi, hao ni watuhumiwa uhalifu mpaka watakapothibitishwa vinginevyo.

Naam, vihenge ( Vya kuhifadhia mazao) vya WanaMbarali vimeingiliwa na panya. Chonde WanaMbarali, tukicheza na ' panya' waliovamia vihenge vyetu, tutaambulia pumba.

Tunasubiri hatua za vyombo vya dola zitakazofuata.
 
Majjid haya yote yanakuja kutokana na system ya kulindana. Kama sheria ingekuwa kali hali isingekuwa hivi watu wanakwiba fedha za umma kirahisi na wanahoja nyepesi kabisa kwani mkaguzi akija yeye hapendi pesa? Kutokana na hilo kujikuta wanafanya watakavyo.
 
Story ya matumizi ya hela za umma kwenye halmashauri ni ya kuhuzunisha. Inakatisha tamaa. Karibu halmashauri zote zinakula bila kuchukuliwa hatua fedha za umma.
 
Marejesho,

Sumu yao wanayo WanaMbarali wenyewe. Iko jikoni wanaichemsha, kwa moto wa kuni.

Maggid
Iringa.

Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo

Kwan hawapanya walipelekwa na Mgeni huko Mbarali ili wafugwe? Au Wanambarali wenyewe ndio waliwachagua na kuwafuga? Na hapa ndipo Watanzania wanaponishangaza!. Panya wale wale, waliosababisha madhara wakirudi kwa kupitia mlango mwingine na masalia ya noti midomoni wanawafungulia milango.

Nail them Up
 
Tumeshazoea kuambiwa hela zimepotea na uchunguzi huwa unafanywa but inaeleweka watanzania huwa ni wepesi kusahau na serikali ina take advantage. :A S-frusty2:
 
Back
Top Bottom