Shilingi Bilioni 9 za walipa kodi zawekwa kibindoni na wajanja wachache. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shilingi Bilioni 9 za walipa kodi zawekwa kibindoni na wajanja wachache.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kachero, Dec 21, 2009.

 1. K

  Kachero JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MVUTANO uliojitokeza kuhusu kusuasua kwa utengenezaji wa barabara ya kilomita 64 ya Bagamoyo-Msata kwa kiwango cha lami, umeingia sura mpya baada ya kubainika kuwa raia mmoja wa Korea ndio kiini cha tatizo hilo.


  Habari za uhakika ambazo Mwananchi Jumapili imezipata zinaeleza kuwa chanzo cha mvutano huo ni baada ya Mkorea huyo aliyeingia nchini kama mwekezaji na 'kuwashika' baadhi ya vigogo serikalini kuchota Sh9 bilioni kati ya Sh13 bilioni zilizotolewa kwa kampuni kadarasi ya Tanzania Korea Partnership (Takopa) ambayo ni muungano wa kampuni za SUMA-JK inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), na kampuni ya Shinwoo na Chungmoo zote kutoka Korea.


  Pia kumpuni hizo zimeshindwa kutekeleza baadhi ya makubaliano ya mkataba, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuleta wahandisi na vifaa vya kufanyia kazi.


  Habari zinasema kuwa kupitia kampuni hizo, Mkorea huyo, ambaye anasemekana kuwa yupo karibu na vigogo serikalini, alijichotea kiwango hicho cha fedha na kukipeleka kwao.


  Takopa ndio iliyosaini mkataba wa miaka miwili wa kujenga barabara hiyo ambayo hadi sasa imejengwa kilometa moja tu. Barabara hiyo iliyotengewa Sh82 bilioni ni moja kati ya ahadi zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kuijenga.


  Kusimama kwa barabara hiyo kumeelezwa kunatokana na SUMA- JKT kuhoji mahali zilipo fedha hizo.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mgogoro huo ulianza baada ya Suma JKT kutaka kupewa maelezo ya kina ya jinsi Mkorea huyo alivyozichukua fedha hizo ambazo zilitolewa kama sehemu ya utaratibu wa mkataba wa malipo ya awali ya asilimia 15 ya gharama za ujenzi.


  Katika fedha hizo Suma JKT walichukua Sh4 bilioni kwa ajili ya kununulia vifaa vya kufanyia kazi ya ujenzi.

  Katika makubaliano ya mkataba wa ujenzi huo, Suma JKT pamoja na kampuni hizo za Kikorea walikubaliana kuwa kila kampuni itoe wataalam na vifaa vya kufanyia kazi ya ujenzi, lakini ni Suma JKT tu ndio waliotekeleza makubaliano hayo.


  Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, katibu mkuu wa Wizara ya Miondombinu, Dk Omari Chambo alikiri kwamba kuchelewa kukamilika kwa barabara hiyo kunatokana na makubaliano ya mkataba wa ujenzi huo kutokwenda kama ulivyopangwa.


  Alifafanua kwamba hali hiyo ilitokana na mshirika (kampuni za Kikorea) kushindwa kuleta wataalam pamoja na vifaa vya ujenzi.Siwezi kuingilia matatizo ya ndani ya Takopa, lakini ninachojua mimi ni kwamba tangu kusainiwa kwa mkataba hawa Wakorea ambao ni wabia na Suma JKT wameshindwa kuleta wataalam na vifaa vya kufanyia kazi,alisema Dk Chambo.


  Hata hivyo, habari za uhakika zinasema kuwa Suma-JKT ilifikia hatua ya kuuliza fedha hizo baada kugundua kuwa kuna mazingira tata na yasiyofuata utaratibu katika matumizi.


  Kutokana na mazingira hayo, Septemba 29 mwaka huu kikao cha kujadili suala hilo kilifanyika na kuhudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi pamoja na katibu mkuu wa wizara hiyo, Mkuu wa Majeshi, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Mkuu wa JKT, Waziri wa Miundombinu, Shukuru Kawambwa, Tanroads na pamoja na wawakilishi wa kampuni hizo za Kikorea.


  Katika kikao hicho Suma JKT ilitangaza uamuzi wa kujitoa katika ushirikiano huo pasipo kuandika barua ili kuifanya Takopa isivunjike kwa vile kwa kuandika barua ingekosa sifa za kuwa kampuni.


  Pia habari zilisema uamuzi wa kujiondoa pia ulichangiwa na majibu ya kebehi ya kuibana Suma JKT kuwa kwa nini inafuatilia zaidi fedha zilizochukuliwa na Wakorea katika mradi huo, kauli ambayo inadaiwa kuwa ilitolewa na mmoja wa vigogo wa kutoka Wizara ya Miundombinu

  Suma-JKT imejiondoa katika ushirikiano huo baada ya kugundua kuwepo kwa mazingira tata ya matumizi ya fedha ya Sh9 bilioni, lakini haikujiondoa kwa kuandika barua kutokana na ukweli kwamba ingefanya hivyo, fedha zote za Watanzania zingekwenda na maji kwa kuwa Takopa isingekuwepo,kilisema chanzo chetu.


  Na hali hii imetokana na Mkorea huyu kuwa na nguvu za ajabu serikalini, na amekumbatiwa na vigogo wakubwa.

  Waziri Kawambwa hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo baada ya simu yake kupokelewa na mtu aliyesema:Waziri Kawambwa ana kazi nyingi ofisini hivyo hawezi kuzungumza na wewe, acha ujumbe nitamfikishia.


  Mwananchi Jumapili ilikuwa imemtafuta kwa zaidi ya mara saba kabla ya kupata jibu kutoka kwenye sauti hiyo.

  Meneja wa Tanroads mkoani Pwani, Gabriel Mwikola alisema katika mradi huo Tanroads mkoani humo imehusishwa kwa kiwango kidogo.


  Ni kweli mradi huu upo katika mkoa wa Pwani, lakini sisi tumehusishwa kidogo... kwa majibu ya kina kuhusu mradi huu wasiliana na Tanroads makao makuu. Kwa upande wangu utakuwa unanionea kwa kuwa si mtu sahihi na sina majibu ya kina kuhusu sakata hilo,alisema Mwikola.

  Katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani hivi karibuni, wajumbe walitoleana uvivu na kutaka ukweli juu ya kusuasua kwa barabara hiyo inayotia doa ahadi za rais.


  Kutokana na kuibuka kwa malumbano katika kikao hicho kwa kila upande kumtupia mpira mwenzake, Mkuu wa Mkoa huo Hajjat Amina Saidi aliamua kuunda kamati ya watu saba ikiongozwa na Profesa Idrisa Mtulia ambaye ni mbunge wa Jimbo la Rufiji kutafuta ukweli wa sakata hilo.


  Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu, Profesa Mtulia alisema kamati yao bado haijaanza kazi kutokana na kukosa vielelezo vya nyaraka kuhusu sakata hilo.


  “Ninavyozungumza na wewe kamati yetu bado hajaianza kazi na hii ni kutokana na kwamba hatukujua tuanzie wapi kwa kuwa hatujapewa vilelezo vyovyote hadi sasa,alisema Profesa Mtulia.


  Profesa Mtulia alisema kamati yake inatarajia kukutana Desemba 22, mwaka huu ili kuangalia uwezekano wa kupewa nyaraka zitakazowasaidia kutafuta kiini cha ujenzi huo.

  Na ninafikiria hadi mwakani ndio tunaweza kuanza kufanya kazi na mara tutakapomalizia ripoti yetu tutaikabidhi kwa mkuu wa mkoa,alisema.

  Source:Mwananchi jumapili.
   
 2. K

  Kachero JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ufisadi utalimaliza taifa hili,haingii akilini kwa mkandarasi kutokukamilisha kazi huku ikibainika wazi kuwa fedha za umma kiasi cha bilioni 9 zimehamishwa kinyemela na kutumiwa na wajanja wachache walioko ndani ya serikali.

  Vyombo vinavyohusika vinasubiri nini kushughulikia suala hili?

  Kwa mwendo huu hata tuwe na miaka 5000 maendeleo Tanzania yatakuwa ni hadithi tuu hakutakuwa na kitu chochote cha maana kitakachofanyika.Hali hii inatia ghadhabu.
   
 3. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ametafuna pesa za barabara inayokwenda nyumbani kwa akina JK (Bagamoyo). Hapo tusikilizie mziki wake.
   
 4. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  vp wanajamii tukijichukulia nchi yetu maana sasa mambo yanatisha. tutagawana madaraka wenyewe.
   
 5. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mungu alinusuru taifa letu.
   
Loading...