Shilingi bilioni 8 kutumika kwenye ruzuku ya wachimbaji wadogo

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Benki ya Dunia (WB) imeahidi kutoa Dola za Marekani milioni 4 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 8, kwa ajili ya Ruzuku katika shughuli za uchimbaji mdogo wa madini nchini.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kumaliza kikao na watendaji Wakuu wa Benki ya Dunia wanaosimamia Miradi ya Sekta ya Madini.

Profesa Muhongo alisema kuwa sehemu ya fedha hizo za Ruzuku ambayo ni ya Awamu ya Tatu zitatolewa mwezi Septemba, 2016.
Aliongeza kuwa fedha hizo zitatumika kufadhili uendelezaji wa vituo Saba vya mfano vya utafutaji na uchimbaji mdogo wa madini ambavyo vitachaguliwa na Wizara baada ya kufanya tathmini ya maeneo yanayoweza kuwekwa vituo hivyo.

“Sio hivyo tu, Fedha hizi za Benki ya Dunia zinalenga kuwafadhili wanawake kwenye shughuli za uchimbaji mdogo wa madini, ukataji na uchongaji wa madini ya vito ili idadi ya wanawake wanaojishughulisha na Sekta ya Madini iongezeke,” alisema Profesa Muhongo.

Aidha, Profesa Muhongo alitoa wito kwa wataalam wote wanaosimamia miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia katika Sekta ya Madini kuhakikisha kuwa utekelezaji wa miradi hiyo uende kwa kasi ili kuleta matokeoyaliyotarajiwa.
Benki ya Dunia kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeendelea kutoa Ruzuku katika Uchimbaji madini mdogo ambapo katika mwaka wa Fedha 2015/16 zilitengwa takribani Shilingi bilioni 7.2 ambazo zilitolewa kwa vikundi 111 vya wachimbaji wadogo na watoa huduma mbalimbali katika sekta ya uchimbaji madini mdogo.

Vilevile, katika mwaka wa Fedha 2013/2014, Fedha za Ruzuku zilizotolewa kwa Wachimbaji Wadogo zilikuwa ni Dola za Marekani 500,000 sawa na takribani Shilingi Bilioni 1 zilizotolewa kwa waombaji 11. Fedha hizi ziliwalenga wachimbaji madini wadogo pekee tofauti na awamu zilizofuata.

Utoaji huo wa Ruzuku unaenda sambamba na utoaji wa elimu na mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini waliopata ruzuku husika ili kuhakikisha kuwa shughuli zilizopata ufadhili zinaleta tija.
 
Safi sana Muhongo.

Moja ya mambo uliyoyaanzisha mara tu ulipoingia wizarani kabla ya ishu ya Escrow haijatibua mambo, ilikua ni kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wote wanapewa ruzuku ya Millioni 80 ili kujiendesha, ulipoondoka ukamuachia Simbachawene akaua mpango huu.

Sasa naona tena umeamua kuurejesha upya, Mungu akubariki sana.
 
Hii habari tamu sana. Wazungusha mikono bado wapo na raisi wao wa mioyo aliye poteza direction.
 
Back
Top Bottom