Shilingi 40,000 Chato hadi Mwanza kwa ndege za ATCL. Vipi mikoa mingine? ATCL mtufikirie

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,305
15,033
ATCL

Tafadhali kama mnavyofanya Chato hiyo mara mbili kwa wiki kwa nauli hiyo hiyo na mikoa mingine mtufikirie walau hata ndege tu pande.

Mtafanya jambo jema sana mkifika na mikoa mingine kwa nauli ya kawaida sio mbaya.

Tafadhali sana mtufikirie ninyi ndio shirika tunalojivunia na kuwategemea.
 
Ukitoka Chato kwenda Mwanza kwa bus; nauli yake ni sh 10000 tu na ni masaa sita tu unakuwa umeishaingia Mwanza. Ina maana hapo utakuwa umesave sh 30000. Ukiweka ya kutumia njiani kama utapenda (kwa wale kula kula) sh 5000! Bado utabakiwa na sh 25000.

Je, hiyo 25000 ni sawa na kilo ngapi za nyama? Na itachukua siku ngapi hizo kilo za nyama kuisha? Chukulia ni familia ya watu wanne tu, kupanga ni kuchagua! Na kuchagua ni kuamuwa. Kwa heli.
 
Ukitoka chato kwenda mwanza kwa bus; nauli yake ni sh 10000. Tuu. Na ni masaa sita tuu unakuwa umeishaingia mwanza. Ina maana hapo utakuwa umesave sh 30000. Ukiweka ya kutumia njiani kama utapenda ( kwa wale kula kula ) sh 5000! Bado utabakiwa na sh 25000 . Je hiyo 25000 ni sawa na kilo ngapi za nyama?? Na itachukua siku ngapi hizo kilo za nyama kuisha??. Chukulia ni familia ya watu wanne tuu..kupanga ni kuchagua! Na kuchagua ni kuamuwa. Kwa heli.
Na sisi wa mikoa mingine tunataka tupate uloda kama huo
 
Yani imefika hatua ATCL nauli 40,000 ili kulazimisha safari
Punguza ujinga,shirika lipo si tu kwa sababu ya biashara isipokua pia kutoa huduma kwa wananchi,ndiyo lengo la serikali yoyote ile duniani,sasa unakejeri utadhani wewe umeyaweza hata maisha yako tu na kumbe unaweza kua unanuka tabu na shida,wa-Tanzania wengi hamna uzalendo na jambo jema la nchi yenu, mko mko tu wengine hata hamjielewi.
 
Mleta ndege safari fupi nauli huwa ndogo sana mfano Dar Zanzibar kwa meli ni shilingi elfu 25 na unatumia saa moja na nusu kufika nauli ya ndege ni elfu 60 lakini watu unakuta wengine hawapandi ndege kwa nini? Jibu ni kuwa reporting time ni masaa mawili kabla ya ndege kuondoka sasa wewe unapoendelea kusota hayo masaa mwawili airport Yule wa Meli anakuwa keshafika Zanzibar muda mrefu

Mfano Arusha na Moshi pote kuna viwanja vya ndege kwa gari ni mwrndo wa dakika arobaini nauli ya ndege ni ndogo Mon lakini unakuta wapangaji wachache. Safari za ndege kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine hisa zipo sio ikiwemo za binafsi za abiria ni wewe tu kupenda usikodolee macho ATCL tu ziko kibao mfano Dar wana hadi kiwanja chako pale terminal one
 
Hiyo nauli hailipi na ni hasara,ila mzee kasema ngoja twende....
"Nasema uongo ndugu zanguuuuu"....
Tupe mchanganuo gharama ni kiasi gani za hiyo safari ambazo ndege inatumia na abiria inapakia wangapi

naona unongea hesabu tu vitu vya kufikirika kama mwehu wala takwimu hapa
 
Back
Top Bottom