Shilingi 200/= Yaleta Kifo MANZESE

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,972
3,830
Kifo cha kusikitisha kimetokea Manzese Midizini, Shilingi 200 ikiwa ni sababu.

Mtu mmoja ameuawa kwa kuchomwa kisu maeneo ya shingoni, mashuhuda wameeleza kuwa kijana mmoja (marehemu) akiwa anafahamiana na mwenzake (muuaji) wakati ametoka shule/chuo alipita mahali walipo rafiki zake. Ndipo mmoja akamfata na kumuomba/kumlazimisha ampe shilingi mia mbili.

Marehemu akatoa elfu moja ili akate mia mbili anayohitaji. Kwa namna isiyoeleweka kwa urahisi bila marehemu kuleta purukashani zozote mwenzake akamchoma kisu.

Baada ya kuona damu nyingi huku marehemu akilalama kwa kumtaja na jina (dying declaration) "fulani unaniua kwa sababu ya 200?" Ndipo kijana huyo wa kipemba akaomba amsamehe kwani hakukusudia kumfanyia hivyo.

Waliokuwa karibu wakataka kumshambulia kijana huyo wa kipemba marehemu akawasihi wasimpige, Kulikuwa na gari karibu aina ya NOAH ( ya Man-rasta) marehem akawaishwa hospitali na muuji kujisalimisha polisi Magomeni.

Marehemu amepelekwa kuzikwa Morogoro (Dumila/Dakawa).
 
kifo cha kusikitisha kimetokea manzese midizini, shilingi 200 ikiwa ni sababu.
Mtu mmoja ameuwawa kwa kuchomwa kisu maeneo ya shingoni, mashuhuda wameeleza kuwa kijana mmoja (marehemu) akiwa anafahamiana na mwenzake (muuaji) wakati ametoka shule/chuo alipita mahali walipo rafiki zake. Ndipo mmoja akamfata na kumuomba/kumlazimisha ampe shilingi mia mbili. Marehemu akatoa elfu moja ili akate mia mbili anayohitaji. Kwa namna isiyoeleweka kwa urahisi bila marehemu kuleta purukashani zozote mwenzake akamchoma kisu.
Baada ya kuona damu nyingi huku marehemu akilalama kwa kumtaja na jina (dying declaration) "fulani unaniua kwa sababu ya 200?" ndipo kijana huyo wa kipemba akaomba amsamehe kwani hakukusudia kumfanyia hivyo. Waliokuwa karibu wakataka kumshambulia kijana huyo wa kipemba marehemu akawasihi wasimpige, kulikuwa na gari karibu aina ya noah ( ya man-rasta) marehem akawaishwa hospitali na muuji kujisalimisha polisi magomeni.
Marehemu amepelekwa kuzikwa morogoro (dumila/dakawa)
​inasikitisha sana mkuu,
 
Dah......hatari sana.....
sasa sababu ya kumchoma kisu na hela alikwisha pewa ni nini..........?.......
 
Imenisikitisha sana hasa marehemu alipoomba muuaji asipigwe! Mungu amrehemu.
 
......HABARI ZAIDI.....
1. Muuaji amekuwa akisikika mara kwa mara kuwa ipo siku atauwa mtu
2. Maeneo haya haya mwaka 2014 tarehe kama hizi yalitokea mauaji kama haya
3. Muuaji alikuwa akicheza kamari na wenzake
4. Muuaji mara nyingi/zote hutembea na kisu ama pis pis (Bisbisi)
 
Hii habari ni ya uongo. Lete uthibitisho kamili. Na huyo muhusika alieua umejuaje kama ni Mpemba?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom