Shikamoo Polisi, kwa hiyo siku anayokuja Tundu Lissu tusiende kupokea wageni wetu?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,817
Lamgambo limelia jamani, wamesikia wa ng'ambo, mwenye kukosa mtoto ama lieleke jiwe. Aliimba hayati Captain John Komba.
Tumesikia ngurumo na mipasuko ya radi kutoka mbali, kuwa shujaa wa Taifa yu aja.

Hii ni baada ya kukaa nje ya nchi kwa miaka mitatu. Aliondoka katika Hali ya ufu, anarudi akiwa vizuri zaidi ki afya, akili na kimtazamo, tayari kuichukua nchi kutoka kwa Mkoloni wa Kolomije.

Polisi wameutahadharisha umma wa Tanzania 🇹🇿 kuwa wasijaribu kuusogelea uwanja wa ndege wala kuukaribia ili Tundu Lissu asipate mapokezi ya heshima.

Polisi wameamua kutumia nguvu, mabavu na silaha za Moto kupambana na wafuasi wa Tundu Lissu watakaojitokeza uwanjani.

Abiria watakaoshuka happy uwanjani ni wengi, si Tundu Lissu peke Yake. Kuna wageni wanaokuja msibani, kuna wageni wa kifamilia, watalii etc

Je, hawa wote haki yao ya kupokelewa inaondolewa sababu ya mtu mmoja tu Tundu Lissu? Hivi mbona mnataka kulitia aibu Taifa letu?

Polisi, swallow your pride, be humble and diplomatic.

Imarisheni ulinzi, acheni Tundu Lissu apokelewe kwa amani, na sisi wengine tupige wageni wetu kwa amani.
Actions speak louder than words. Wageni wakiiona amani kwa vitendo wataenda kusimulia kwao.

Pia wakiiona vurugu ndio kitu watakachoondoka nacho, kuwa Tanzania ni nchi ya vurugu tu
 
Ushauri wangu polisi wasimamie ulinzi tu wakumbuke kauli ya mh rais pale dodoma siku ya uzinduzi wa majengo ya TAKUKURU kuwa "msifanye mambo mkidhani mnanifurahisha acheni kujipendekeza subilini nitoke madarakani ndio mjipendekeze"

Hayo maneno hayo mambo sasa ajichunge muda wa kampeni huu asijikute wanamtoa kafara apeleke askari wapige watu mh rais amuhoji kwanini kapeleka askari kulikuwa na shida gani akakosa majibu akatumbuliwa awe makini sana mambo sasa mda huu awambie askari wake wasiguse MTU

Yasije tokea ya kinondoni ya akwelina itakuwa picha mbaya sana kwa taifa
 
Jeshi la polisi Tanzania 🇹🇿 ni aibu ya Taifa, wacha Wakenya waendelee kutudharau na kutucheka kila uchao
 
Hatutaki mikusanyiko isiyo rasmi. Hatutaki maandamano
Hamtaki wewe na nani?

Mbona unaandika kwa kujitutumua sana na kujumuisha jumuisha wengine?

I am a psychologist, i can see you are very scared!

Eti "HATUTAKI".... hahahaha Doooh!
 
I am a psychologist, i can see you are very scared!
Huenda umepewa maagizo yenye masharti, ama huenda unaogopa kuonekana incompetent kwenye kazi yako, ama huenda umejawa tu na hofu ya kuogopa kushindwa!

Either ways, najua unafanya kazi yako!

Nimekokotoa kila pumzi unayoitoa kupitia maandishi unayoandika nikabaini wewe ni muoga!
 
Back
Top Bottom