Shikamoo Makonda, hatimaye shisha yatoweka Dar es Salaam

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,673
Usiku huu nikiendelea na mizunguko yangu ya usiku ya kumalizia weekend nilikuwa pia nafanya uchunguzi wa kimya kimya kuhusu agizo la mwenye Dsm yake Mh Paul Makonda kuhusu uvutaji wa shisha.

Mpaka sasa sehemu zote nilizotembelea sijaona kitu inaitwa shisha ikiuzwa. Nimepita KB paradise tabata, nikachungulia Fourty Fourty pub tabata bima sijaona ata vile vidubwasha vya shisha. Nikaendelea na mizunguko Samaki mpaka Qbar kote huko sijaona shisha ikivutwa wala kuuzwa.

Ama kwa hakika watu sasa wanaheshimu serikali. Nakuhaidi Mh Makonda kama utafanikiwa kuyaondoa mashoga kuna madawati kumi nitakuchangia kiroho safi.

Heshima kwako!
 
Yan minasubiri hayo madawati halafu nakushauri uyatoe katika Mkoa wa Dsm itakuwa bora zaidi.
 
nakuomba upite pite na mtaani Mkuu ufanye utafiti khs wavuta fegi je wanavuta hovyo au wametengewa maeneo wanavuta huko!!?asante.
 
Mkuu mimi sipo instagram ila mashoga uwa nayaona kinondoni tena siku hizi yameanza kuvaa nguo za kike naamini Makonda atatuondolea hii laana. Ila kwenye shisha kwa niliyoyaona ni mafanikio makubwa tofauti na nilivyofikiri mwanzoni kuwa itakuwa na ugumu.
Tatizo la Tanzania hii hakuna agizo la kudumu, tunaendeshwa kwa matukio, baada ya mwezi hayo yote yatakuwa yamesahaulika na yataendelea kama kawa, ni kama dokta kigwangala alivyowapiga stop kina dk mwaka, but sahivi wamerudi kwa fujo
 
Kila la heri bwana masifa Makonda! Kupambana na Mashoga na Makahaba! Angalia usipoteze focus hizo zote hazimo kwenye ilani ya ccm! Na wengine ni wana ccm wenzako! Yale maumbile yao yanasukumwa na hormone zaidi sio utashi wao! Tupa ile computer ya apple!
 
Usiku huu nikiendelea na mizunguko yangu ya usiku ya kumalizia weekend nilikuwa pia nafanya uchunguzi wa kimya kimya kuhusu agizo la mwenye Dsm yake Mh Paul Makonda kuhusu uvutaji wa shisha.

Mpaka sasa sehemu zote nilizotembelea sijaona kitu inaitwa shisha ikiuzwa. Nimepita KB paradise tabata, nikachungulia Fourty Fourty pub tabata bima sijaona ata vile vidubwasha vya shisha. Nikaendelea na mizunguko Samaki mpaka Qbar kote huko sijaona shisha ikivutwa wala kuuzwa.

Ama kwa hakika watu sasa wanaheshimu serikali. Nakuhaidi Mh Makonda kama utafanikiwa kuyaondoa mashoga kuna madawati kumi nitakuchangia kiroho safi.

Heshima kwako!

Kuna mawili,kama wewe si kibaka,basi utakuwa kahaba mzoefu hapa mjini,haiwezekani mtu uzurule kiasi hicho tena usiku.Hata hivyo kutokuyaona hayo unayojaribu kutuhadithia,hakumaanishi watumiaji wa "hiyo kitu" wameacha kuitumia.
 
Hatuwezi kutumia pesa za umma kutibu vifua vilivyooza. Big up Makonda.sasa lala nao hawa wanaodhani ushoga ni jambo la kujianika hadharani
 
Hata madawa ya kulevya ni marufuku lakini bado yanauzwa na kuvutwa...Watabuni njia nyingine iliyobora ya kuvutia hiyo kitu.
 
viwanja vya VIP tunaendelea kupata huduma kama kawaida ila bei imepanda kwa kasi
 
Ni neno la kiarabu ila sio sisha ni ASHISH maana yake ni BANGI au MAJANI
Umeamua kupotosha au? Maana shisha ni shisha na hashiish ni bangi vitu viwili tofauti kabisa kama shisha inavutwa middle East as ganja basi wana mushkel
 
Back
Top Bottom