"Shikamoo" baina ya wanandoa: Je kuna umuhimu?

Pretty

JF-Expert Member
Mar 19, 2009
2,576
552
Habari zenu wana Jf,
Kuna hili jambo huwa najiuliza, sijapata jibu. Labda wana ndoa wanaweza kusaidia.
Je kuna umuhimu wa wanandoa au wapenzi kumpa shikamoo mwenzake aliyemzidi umri?
 
Habari zenu wana Jf,
Kuna hili jambo huwa najiuliza, sijapata jibu. Labda wana ndoa wanaweza kusaidia.
Je kuna umuhimu wa wanandoa au wapenzi kumpa shikamoo mwenzake aliyemzidi umri?
Shikamoo kwa wanandoa naona ni uzushi tu. Na kwa ujumla, ni salamu inayonikera sana mimi. Nikikupa itabidi ujisifu!
 
Habari zenu wana Jf,
Kuna hili jambo huwa najiuliza, sijapata jibu. Labda wana ndoa wanaweza kusaidia.
Je kuna umuhimu wa wanandoa au wapenzi kumpa shikamoo mwenzake aliyemzidi umri?

Nimeshasikia hili lipo, lakini kwa maoni yangu mke na mume hata kama kuna gap kubwa kiumri kati yao haipendezi mmoja kumpa shikamoo mwingine.
 
...hivi kuna ubaya gani kuamkiwa jamani?

...utawasikia wenyewe "unanipa shikamoo unata kuninyima nini", au wengine kwa shingo upande wanaijibu shikamoo kwa "ahsante!"

...pretty shikamoo!...
 
Habari zenu wana Jf,
Kuna hili jambo huwa najiuliza, sijapata jibu. Labda wana ndoa wanaweza kusaidia.
Je kuna umuhimu wa wanandoa au wapenzi kumpa shikamoo mwenzake aliyemzidi umri?

Binafsi sidhani kama inastahili bwana.. mtu kama ni mume/mke nadhani salamu ya kujuliana hali umeshindaje? umeamkaje? mzima mpenzi inapendeza kuliko shikamoo, halafu hilo neno shikamoo halina maana nzuri
eti niko chini ya miguu yako? ukoloni mind set! siipendi kwakweli!

Bora wanandoa msalimieni kwa kilugha chenu.. walau salaam ina make sense! Kama mu lugha tofauti fundishaneni
 
Last edited:
Shikamoo ni unazi. SHIKAMOO-MARAHABA!Then what? hii salamu haina maana yoyote nigefurahi kama ingefutiliwa mbali. Kwa swali lako jibu ni hilohilo...salamu hii ni ya kikoloni isiyo na maana zaidi ya kumshusha hadhi mtu mwingine na haipendezi hata kwa wanandoa.
 
Mimi nitapenda kama nitamzidi mzee umri anipe shikamoo yangu ila akinizidi sitaweza kumwamkia. Japokuwa hamna umuhimu sana kuamkiana, inategemea na katiba ya nyumbani yenu.
 
Mimi nitapenda kama nitamzidi mzee umri anipe shikamoo yangu ila akinizidi sitaweza kumwamkia. Japokuwa hamna umuhimu sana kuamkiana, inategemea na katiba ya nyumbani yenu.

Mbona wewe huniamkia ama ni for a short term?
 
...hivi kuna ubaya gani kuamkiwa jamani?

...utawasikia wenyewe "unanipa shikamoo unata kuninyima nini", au wengine kwa shingo upande wanaijibu shikamoo kwa "ahsante!"

...pretty shikamoo!...
Marhaba! Hujambo ww?
 
kila siku nilikuwa najiuliza hili swali, maana kuna mama mmoja alikuwa anampa shikamoo mmewe, sasa mie nilikuwa nashangaa watu wanalala kitanda kimoja na kufanya mchezo halafu tena utoe shikamoo kwa mume, wala haifai kweli.
 
Hakuna shida,ila ni mfumo dume tu kwamba SHIKAMOO maana yake ni nipo chini ya miguu yako-sina uhakika nalo,ila kama ndivyo MWANAMKE ANATAKIWA AMWAMKIE MUME.
My take,kwa aina hiyo ya kuamkiana hakuna usawa,sasa je TUNATAKA USAWA ktk Ndoa AU LA?
 
neno shikamoo halina maana nzuri

eti niko chini ya miguu yako? ukoloni mind set! siipendi kwakweli!

Tuko pamoja, ingelikuwa amri yangu nisingeliamkia wala kuamkiwa kutokana na 'outdated' history ya salam yenyewe. Kwa nini tupige vita mila potofu halafu tuiache hii salam? Umefika wakati kwa wanaharakati kuimulika hii salam na ikiwezekana kuivalia njuga ikome kabisa, ni kinyume cha haki za bindadamu na inaendeleza unyonge tu miongoni mwa watanzania. Ikumbukwe baadhi ya mababu zetu walilazimika kuvaa upupu kujikinga dhidi ya watoza kodi ya kichwa, ni haki leo kuiendeleza mbinu hii ya kivita dhidi ya TRA? La hasha, shikamoo imepitwa na wakati...
 
Sio lazima, lakini mke akiamua kufanya hivyo sio vibaya!!!

Na je kama mke ndiyo kamzidi umri bado amwamkie mumewe?
Nadhani "shikamoo" kama salamu ina maana ya kumnyeyekea mtu... kuonyesha kuna ambaye yuko juu ya mwingine - kiumri, kicheo, n.k. Sasa kwenye ndoa kuna hiyo hierachy? au kwa vile imani nyingine zinasema mume ni kichwa?
Inapendeza heshima iwe ya hiari na siyo ya kulazimisha.. na kwa wanandoa salamu yenye kuonyesha mapenzi ni bora zaidi kuliko ile yenye kuonyesha matabaka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom