Shigongo na wenye uelewa kama wake kuwa watanzania wa leo sio wa mwaka 1947 wanaejielewa asitumie umaarufu wake kupotosha umma juu ya msimamo wa Bunge

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mnamo tarehe 16/11/2018 zikiwa ni siku nne tu tangu nimetoka katika mkutano mkuu wa vijana wanaotokana na vyama vya kidemokrasia duniani ( International young Democratic Union) nilipata kuandika hivi.

"Nasisitiza tena uhusiano wa kidiplomaaia kati ya Tanzania na mataifa ya dunia ni mbaya katika nyakati za hivi karibuni.

Madhara yake hayachagui yawapate wapinzani na kuwaacha chama tawala. Hayabagui wanaoikosoa werikali na kuwaacha wanaoipongeza serikali hata kwa mambo yasiyostahili pongezi.

Hali kama hii iliwahi kuitokea serikali ya rais Robert Mugabe huko nchini Zimbabwe. Nasisitiza tena uhusiano wa Tanzania na nchi za jumuia za Ulaya sio mzuri kabisa.

Fuatilia tamko la Jumuia ya Ulaya. Msimamo wa nchi ya Denmark nk. Utagundua sasa tunaelekea kusikojulikana.

Wito wangu kwa vijana wenzangu sasa ni wakati wa kushikamana kuisimamia serikali na mamlaka zake kuhakikisha inairudisha nchi yetu katika msitari wake. La sivyo tujiandae kwa anguko kubwa la uchumi na maswala mengine mengi ya kijamii nchini".

Kwa bahati mbaya kabisa hali ilivyo sasa ni wazi kabisa taifa letu pendwa kabisa la Tanzania limepasuka vipande vipande. Katika hili wapo walioanzisha kampeni inayoitwa ninasimama upande wa Rais.

Masalani nimemshuhudia mwandishi nguli kabisa Erick Shigongo akiandika nanukuu " KATIKA HILI NACHAGUA KUSIMAMA NA RAIS WANGU"

Akaendelea kuandika, "Nimesoma barua ya maazimio 15 ya Bunge la Ulaya ( European Union) kwa serikali yetu ya Tanzania. Maazimio hayo yanabeba mashariti magumu kwa sababu kwenye barua yao wanazungumzia ushoga. Lakini pia kuna mambo ya mengine yametajwa kwenye mazimio hayo kama demokrasia na kutetereka kwa Haki za binadamu.

Wacha nimuhoji kidogo shigongo na wengine wenye uelewa kama wake.

1. Nchini mwetu Tanzania ni serikali ya chama gani iliyosaini mikataba inayohalalisha ushoga nchini. Atanijibu kuwa zilikuwa ni awamu zilizopita namkumbusha tena rejea barua ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki ya tarehe Novemba 4, 2018 Inayosema kupinga ushoga ni msimo ninafsi wa Paul Makonda na si msimamo wa serikali.

So kauli hiyo nini maana yake?? Serikali haipingi ushoga so inakubali ushoga kulingana na mikataba iliyokwisha kusaini.

2. Kutetereka kwa haki za binadamu. Ulaya inataka Tanzania iimarishe kusimamia haki za binadamu so unasimama upande wa rais kwamba Tanzania isiheshimu haki za binadamu???

3. Kwamba ulaya inataka Tanzania iheshimu misingi ya demokrasia kwamba unasimama upande wa rais unamaanisha kuwa rais haheshimu misingi ya tawala za kidemokrasia?

Inamaana Shigongo hajui kuwa kinyume cha demokrasia ni udikteta???

Mwisho, Shigongo anasema"Tayari waziri wa fedha na Mipango Dr. Philip Mpango amesema kama nchini tutapita kwenye wakati mgumu kidogo kwani tutakosa ushirikiano kutoka kwa wahisani kutokana na msimamo wetu".

Shigongo anataka kutuambia kuwa msimamo wetu ni kinyume na mapendekezo ya Eu ambayo ni kama ifutavyo wacha ninukuu kidogo andiko la mwanaharakati *Mwanakijiji Mwanakijiji Lugosi*

USIKUBALI KUPOTOSHWA HAYA NDIYO MAAZIMIO YA BUNGE LA ULAYA EU

Waziri wa mambo ya nje asema awezi kuzungumzia azimio hilo anasubiri Raisi atoe tamko

>>>Utawala wa sheria
>>>Haki za binadamu
>>>Kamata kamata ya wapinzani
>>>Elimu
>>>Afya
>>>Haki ya kupata habari
>>>Sheria kandamizi na matamko
>>>Mikutano ya kisiasa kupigwa marufuku
>>>Kuandamwa kwa watetezi wa haki za binadamu
>>>Kufungiwa vyombo vya habari
>>>Kuandama watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja

BUNGE HILO LIMETAKA PIA HAYA YATEKELEZWE

>>>Kuachiliwa wafungwa wote wa kisiasa
>>>Kurekebisha baadhi ya sheria ikiwemo ya makosa ya mtandao , sheria ya vyombo vya habari
>>>Kuachia uwanja kwa watetezi wa haki za binadamu kufanya shughuli zake

LIMETAKA PIA HAYA YAWEPO

>>>Tume huru ya kuchunguza kutekwa na kuakamatwa kwa waandishi wa habari na watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha
>>>Hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wale wataobainika kuvunja haki za binadamu.

Shigongo rafiki yangu uzarendo si kusimama upande wa rais hata kama haenendi kizarendo. Uzarendo ni kusimama upande wa taifa hata kama utakuwa peke yako katika hili mimi ninachagua kusimama upande wa Tanzania iliyojeruhiwa.

Tujisahihishe kama taifa. Eu imesima kama kiyoo kutueleza udhaifu wetu. Kazi yetu sio kuvunja kiyoo bali kurekebisha makosa yanayoonekana ambayo ndiyo taswira yetu harisi katika kiyoo.

Wasalaam.
Mwl, John Pambalu.
Mhe. Diwani (K) Butimba Mwanza.
Makamu mkt Bavicha Tanzania bara.
 
Hakuna mwenye mamlaka ya kuiamuru nchi iliyo huru ibadili sheria zake. Huwezi kuja na tamko la kulazimisha nchi huru kama Tanzania ibadili sheria eti kisa misaada. Marekani imefanya uhalifu mwingi kwenye nchi za kiarabu mbona hawakutoa matamko? Leo wanadai eti wanasiasa wanafungwa kwa sababu za kisiasa, wapi hao wakati tunashuhudia wakifanya jinai waziwazi? Leo wanalazimisha wachunguzi wa kimataifa, waje kufanya nini kwenye taifa lililo huru?

#Istandwiththepresident #ukoloniuliishamwaka1961
 
Huyo shigongo utashi wake kisiasa ni mdogo sana.anashindwa kujua serikali ya magufuli imehalalisha mikataba ya kimataifa na kupelekea anguko la mahusiano mazuri na mataifa ya magharibi.rais na serikali yake ni wafungwa wa mawazo mbadala.
 
Huyo abakie tu kuandika hadithi zake za kusadikika aachane na siasa. Ameona watu hawasomi tena hadithi zake na sasa amehamia kujikomba komba ili arudi tena kwenye line.

Zama hizi zimeshabadilika hivyo namshauri aje kivingine ila kwa haya ya kujipendekeza aache. Akazane kuboresha hadithi zake za sungura na ndizi huenda watoto wa sekondari wakazipenda tena
 
Hakuna mwenye mamlaka ya kuiamuru nchi iliyo huru ibadili sheria zake. Huwezi kuja na tamko la kulazimisha nchi huru kama Tanzania ibadili sheria eti kisa misaada. Marekani imefanya uhalifu mwingi kwenye nchi za kiarabu mbona hawakutoa matamko? Leo wanadai eti wanasiasa wanafungwa kwa sababu za kisiasa, wapi hao wakati tunashuhudia wakifanya jinai waziwazi? Leo wanalazimisha wachunguzi wa kimataifa, waje kufanya nini kwenye taifa lililo huru?

#Istandwiththepresident #ukoloniuliishamwaka1961
Usipobadili kwa hiyari utalazimishwa kubadili kwa nguvu.
 
Back
Top Bottom