Shigongo: Baada tu Hayati Kupumzika Wamepandisha Bei ya Umeme, Unit 2400

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
665
1,000
Akiwa Bungeni, mbunge Shigongo amelalamikia wananchi kutoka jimbo lake la Buchosa, visiwa vya Zilagula na Maisonga kununua unit moja kwa Tshs 2,400 kutoka kwa kampuni binafsi za Power Gen

Amesema kampuni hizo zilipewa maagizo na waziri kuuza umeme kwa Tshs 100 lakini baada ya Rais Magufuli kufariki wamepandisha bei kufika 2,400 na amedai wanasema aliyekuwa anawasumbua ameondoka na kuwasikitia kutojua mama Samia ni moto wa kuotea mbali.

Kwenye hoja hiyo ya umeme, Mbunge wa viti maalum, Esther Matiko amelalamikia gharama kubwa za umeme Tanzania akitolea mfano watu wanaoishi Kagera na kupokea umeme kutoka Uganda wananunua unit 80 za umeme kwa Tshs 10,000 ilhali kwa Tanzania unapata unit 28 pekee.

 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,787
2,000
LCoE ya umeme kutoka kwenye kampuni hizo ni kiasi gani!? Tukijua hilo, itatuwia raihisi sana kujua kama hiyo bei ya 2400 ni halali ama la!!
 

chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,115
2,000
Wangepandisha ukawa unapatikana muda wote tungevumilia, sasa wamepandisha na bado wanakata na mara nyingi wanakata makusudi ili wapate pesa za kufanya kazi nje ya ofisi (ndivyo inavyosemekana). TANESCO ni viumbe wa kichefuchefu sana.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,311
2,000
Huyu hajui kwamba mashirika yote nchini yapo chini ya CCM, sasa nani kapandisha umeme bila idhini ya chama chetu? Ajiangalie maana kadi yetu anayo alijue hilo..
 

ZAK ZAK

JF-Expert Member
Mar 2, 2018
263
250
Kuna wapumbavu hawaoni makosa ya Marehem hapa ya kuendesha nchi Kwa kumuogopa mtu mmoja badala ya kujenga taasisi imara
Hayo maneno umemezesha na wajasiasiasa na vibaraka wa mabereru eti " jenga mfumo imara" ikiongee neno mfumo imara unaonekana ni unaakili. Acha kuwahadaa wasio na elimu mfumo imara ni nchi tajiri na zenye watu wachache kama US, UK, Sweden, Norway.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,376
2,000
Akiwa Bungeni, mbunge Shigongo amelalamikia wananchi kutoka jimbo lake la Buchosa, visiwa vya Zilagula na Maisonga kununua unit moja kwa Tshs 2,400 kutoka kwa kampuni binafsi za Power Gen...
Shigongo muongo huko madongo kuporomoka kuna mwenye uwezo huo wa kununua unit 2400? Au anamanisha 240?
 

Tata

JF-Expert Member
Dec 3, 2009
5,800
2,000
Hayo maneno umemezesha na wajasiasiasa na vibaraka wa mabereru eti " jenga mfumo imara" ikiongee neno mfumo imara unaonekana ni unaakiri. acha kuwaadaa wasio na elimu mfumo imara ni nchi tajiri na zenye watu wachache kama US, UK, Sweden,norway,
Kuna nchi zilizoendelea zenye watu wengi na zenye watu wachache. Ila zote zina mifumo imara. Kwa ulizotaja USA ina watu 300+ million (GDP $22 Trln), UK ina watu 68+ million (GDP £1.96 Trln), Sweden ina watu 10+million (GDP $529 bln) na Norway ina watu 5+ million (GDP $ 360 bln) Tanzania ina watu 59+ min (GDP $50 bln)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom