Shida ya kupenda usipopendwa!

molwe

JF-Expert Member
Jan 10, 2015
398
410
Mama mkwe kamfukuza mka mwana nyumbani, mume kaungana na mama yake! Jamani kuna sababu ya mke kung'ang'ania ndoa hiyo??
 
Huyo mama mkwe kamfukuza mkwewe nyumbani kwa nani???

Kama mume anaungana na mama yake hapo Mungu asimamie tu lakini ndoa inalega lega hiyo
 
Mama mkwe kamfukuza mka mwana nyumbani, mume kaungana na mama yake! Jamani kuna sababu ya mke kung'ang'ania ndoa hiyo??
kwanza inategemea walivyooana na nguvu ilikuwaje ya kuhakikisha wanaoana, kwamaoni yangu mimi binafsi ni kwamba unaweza ukakuta mwanamke alilazimisha ndoa wakati mwanaume hakuwa tayari kwa wakati huo , au mwanamke alimwambia mwanaume nina ujauzito wako jitahidi unichukue au vinginevyo maana sio kawaida mwanaume kuamua kuwa upande wa mama yake acha niseme hivi, sisi wengine ambao tulipendwa sana na mama zetu ninapotaka kuoa huwa naongea na mama nayeye huwa anafanya tafiti kujua mke ni mwenye tabia zipi na wazazi wake wana tabia zipi na kupata historia ya ukoo wa mchumba, yapo mengi mama anaweza kuamua kunishauri nisioe na kutaka niache sasa unakuta msichana anakwambia "FULANI KWANI WANAOA WAO AU, WEWE NDIO UNAYEOA USIWASIKILIZE BHANA TUANZE MAISHA YETU" hapo sasa...
 
Mpaka mume anaungana na mama mkwe inawezekana huyo mke anamatatizo mpaka imekuwa kero.Hata kama hana matatizo hana budi kujiongeza kwani mume hamtaki na ukweni hatakiwi.
Aunge safari ajipange upya kimaisha.
MPE pole yake
 
Makosa mkubwa kuolewa kukaa kwa wakwe.
Na km ma mkwe kaingilia ndoa na mwanae wameungana jione km familia imejikusanya na wewe huna chako. Jiongeze ondoka hapo kaanze maisha yako.
 
Pengine shida sio kupenda pasipopendwa bali ni hali ngumu ya maisha,mama mkwe anaona vyuma vimekaza hivyo hawezi kuendelea kulisha mwana na mka mwana na pengine mume naye anajijua pia hana pato la kumtunza mkewe hivyo ni bora aungane tu na mama yake katika kubana matumizi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom