The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,229
- 116,840
Wakati anafungua daraja la Kigamboni Rais Magufuli alisema..
washauri wake walimshauri daraja la Kigamboni liitwe 'daraja la Magufuli' ila yeye akaona sio busara..ndio akaja na jina la Nyerere.
Niliposikia hayo kwa kweli sikushangaa.
Watu wamesahau tu hata Kikwete alipoenda kufungua Uwanja wa Taifa wa mpira
'wapambe ' pia walimshauri auite uwanja wa Kikwete, ingawa uwanja ulijengwa na Mkapa kama ambavyo daraja la kigamboni limejengwa na Kikwete.
Sasa why wapambe wanakuwa namna hii?
Wanashauri kwa style ya kujipendekeza na kujikomba kwa marais?
Hivi mangapi ambayo hatuyajui ambayo wamemshauri Rais?Kikwete na Magufuli
wote wameingizwa mkenge mara ngapi na wapambe?
Magufuli juzi tu alimchagua mtu TRA (Eliakim Maswi) akalazimika kumtengua baada ya mwezi mmoja tu.
Ukweli ni kuwa shida ya nchi zetu hizi za kiafrica inaanzia hapo
Hatujui hasa washauri wa Rais ni kina nani, wana qualify vipi kumshauri
ni wasafi kiasi gani! Mara zote tunategemea tu 'busara' za Rais mwenyewe..
Huku wapambe wako gizani wakizidi kufanya mambo yao kimya kimya..
Tunaweza kumhukumu Kikwete leo na Magufuli kesho lakini bila kubadili mfumo
unapelekea Rais kuzungukwa na watu 'sahihi' tutabaki na mshangao kila mara na maamuzi.